Kunyonyesha ni mojawapo ya njia asili za kuzuia mimba. Mara nyingi, mama anaye nyonyesha miezi ya kwanza mitatu baada ya kupata mtoto huwa salama kufanya ngono bila kupata mimba. Kumbuka kuwa mama anastahili kungoja hadi pale anapo pona baada ya kujifungua kabla ya kujitosa kwenye tendo la ndoa. Kuna nyakati ambazo mama licha ya kuwa ana nyonyesha anaweza kupata mimba. Je, mama anaweza kutumia njia za kuzuia mimba baada ya kujifungua?
Ni vyema kwa mama kujilinda dhidi ya kupata mimba ingine anapo nyonyesha.
Kupata mimba mama anapo nyonyesha

Kwa kawaida, ni vigumu kwa mama kutunga mimba angali yuwa nyonyesha hasa katika miezi ya kwanza michache baada ya kujifungua. Anapo nyonyesha, kuna homoni inayo tolewa inayo zuia yai kupevuka, na kukosa kupata kipindi cha hedhi kwa miezi michache. Hata hivyo, mama angali ana nafasi ya kutunga mimba. Na ndiyo sababu kwanini daktari humshauri mwanamke jinsi ya kuzuia mimba kabla ya kutoka hospitalini.
Njia za kuzuia mimba baada ya kujifungua
- Kutumia tembe ama vidonge vya kupanga uzazi
Mama hashauriwi kutumia tembe za uzazi wa mpango baada ya kujifungua. Kwani zina mchanganyiko wa vichocheo ambavyo huenda vika athiri na kupunguza utoaji wa maziwa ya mama. Utoaji wa maziwa yasiyo tosha ya mama kuta athiri ukuaji wa mtoto.
Hata hivyo, ni salama kwa mama kutumia tembe zilizo na aina moja ya kichocheo cha progesterone.
Kwa wanandoa wasio weza kungoja hadi miezi mitatu kuisha kabla ya kurejelea tendo la ndoa, wanaweza tumia mbinu hii. Mwanamme anamwaga manii nje baada ya kufika kilele katika tendo la ndoa.

Njia hii ni salama kwa mama na bora zaidi. Ina ufanisi wa asilimia 99 wa kulinda dhidi ya mama kupata mimba angali ana nyonyesha. Pia, mama ana kingwa dhidi ya kupata magonjwa ya zinaa kama vile herpes, kwani kipindi hiki afya yake ni dharura sana na nyeti.
Hizi ni baadhi ya njia za kuzuia mimba baada ya kujifungua ambazo mama anaweza kutumia. Kupata mimba mama anapo nyonyesha kuna athari kwa afya yake na ya mtoto anaye kua tumboni. Ni vyema kuzuia kupata mimba katika miezi ya kwanza michache baada ya kujifungua.
Soma Pia: Njia Tofauti Za Kuzuia Mimba Kama Vile Kwa Kutumia Chumvi!