Utafiti umevumbua njia za uzazi wa mpango kwa wanaume za kutumia tembe ya kupanga uzazi. Tembe hii ya uzazi wa mpango ya wanaume imepita majaribio kuonyesha iwapo ni salama kwa matumizi ya binadamu.
Inatumika mara moja kila siku na ina homoni zinazo komesha uwepo wa manii ama mbegu za kiume. Kwa hivyo hata mwanamme anapofanya kitendo cha ndoa, hakuna uwezekano wa mwanamke kupata mimba. Hapo awali, mbinu za kupanga uzazi kwa waume zilikuwa mbili tu, kutumia kondomu ama kupasuliwa mirija ya uzazi, kwa kimombo, vasectomy. Hata hivyo, mbinu ya kutumia tembe za uzazi kwa wanaume haija pitishwa bado. Hata kama utafiti umedhihirisha kuwa ni salama katika hatua zote, huenda ikachukua muda wa hadi miaka kumi kuidhinishwa na kutumia mbinu hii.
Athari za tembe za uzazi za kiume

Kwa walio tumia tembe hizi walishuhudia upungufu wa azma ya hamu ya kufanya mapenzi. Ila hilo haliku athiri utendaji katika kitendo chenyewe. Hata hivyo wanaume wengi wako wazi kutumia tembe hizi zinapo patikana.
Kutokana na homoni zilizoko kwenye tembe hizi, seli mpya za shahawa huundwa kwenye kibofu cha mwanamme. Na kuzuia kwa kipindi ili kupunguza viwango vya manii.
Lakini utafiti zaidi bado unafanyika na majaribio kufanywa kuhusu athari zote za tembe hizi.

Kwa wanaume walio tumika kufanya majaribio, ingawa baadhi walikisia kupungukiwa na hamu ya kufanya tendo la ndoa, huku wengine wakitatizika kufanya tendo hilo, shughuli hiyo haikupunguka. Na tembe hizi zilionekana kuwa salama kwa matumizi ya wanaume.
Tembe hizi zitasaidia sana kudhibiti uzalishaji kwa kupungua kiwango cha manii kinacho tengenezwa mwilini mwa mwanamme.
Njia za uzazi wa mpango kwa wanaume zina zidi kuvumbuliwa. Utafiti ungali unafanyika huko umarekani kudhibitisha ikiwa ni salama kwa matumizi ya binadamu na athari zake kwa waume. Hata baada ya kupita hatua zote za usalama, inasemekana kuwa huenda ikachukua kipindi cha hadi miaka kumi kabla ya tembe hizi za uzazi za kiume kupitishwa.
Chanzo: WebMD
Soma Pia:Utumiaji, Manufaa Na Athari Za Limau Katika Kuzuia Mimba