Njugu: Sababu Kwa Nini Moyo Wako Una Hitaji Ule Njugu Zaidi

Njugu: Sababu Kwa Nini Moyo Wako Una Hitaji Ule Njugu Zaidi

Njugu zina bidhaa inayo linda endothelium (kuta ya arteries) na pia arginine na phenolic. Kulingana na utafiti, njugu zina boresha kubana na kupanuka kwa kuta za mishipa ya damu.

Kula njugu ni muhimu kwa afya yako na pia kwa kuhakikisha kuwa moyo wako una fanya kazi vyema. Makala haya yana kuelimisha jinsi njugu zinavyo saidia afya ya moyo wako. Watu wengi wana fahamu manuu ya njugu kama kuwa na protini tu, pia ina virutubisho vingine muhimu.

Masomo tofauti yameonyesha kuwa njugu zina ufuta ulio rahisi kutumika mwilini na ambao ni mzuri kwa moyo wako. Una ona sababu kwa nini unastahili kula njugu zaidi?

Njia ambazo njugu zina dumisha afya ya moyo:

afya ya moyo

  1. Njugu zina madini ya magnesium na potassium zinazo saidia kudhibiti shinikizo yako ya damu (ambayo ni hatari kuu ya ugonjwa wa moyo). Ili kudhibiti shinikizo la damu, kula njugu zisizo na chumvi.
  2. Njugu zina bidhaa inayo linda endothelium (kuta ya arteries) na pia arginine na phenolic. Kulingana na utafiti, njugu zina boresha kubana na kupanuka kwa kuta za mishipa ya damu, na kuepusha athari ya kuwa ngumu.

kuchelewa kwa kipindi chako cha hedhi

3. Watu wengi hufikiria magonjwa ya moyo na kisukari kama matatizo ya kiafya yasiyo husikana. Lakini ukweli ni kuwa, kuwa na kisukari kuna ongeza hatari zako za kuugua ama kufa kufuatia magonjwa ya moyo. Utafiti umeonyesha kuwa kula njugu na njugu zilizo siagwa ama siagi ya njugu kume husishwa na hatari ya chini ya aina ya pili ya kisukari.

Soma Pia: Fahamu Faida Za Kula Mayai Kwenye Lishe Yako

Written by

Risper Nyakio