Orodha Ya Dakika Ya Mwisho Kabla Ya Kuenda Hospitali Kujifungua

Orodha Ya Dakika Ya Mwisho Kabla Ya Kuenda Hospitali Kujifungua

Mwongozo muhimu kabla ya kumkaribisha mwanao!

Je, uko tayari kabisa kumkaribisha mtoto wako? Kabla ujazwe na hofu nyingi, hapa kuna ujauzito dakika ya mwisho orodha ya vitu vya kufanya kabla maisha yako yabadilike kabisa. Twakutakia mema!

Uko hapa, siku chache fupi kabla siku yako kuu ifike na uwe na hofu nyingi zaidi. Sherehe ya kumkaribisha mtoto imeisha, umeanza likizo yako ya kujifungua na kila kitu kinaonekana kufuata utaratibu kabla mtoto wako kufika.

Iwapo uko moja kati ya wamama wengi ambaye hajifungui kabla ama katika siku tarajiwa, mchezo wa kungoja huenda ukawa wenye uchungu mwingi. Kwa hivyo, badala ya kujitesa kwa kuhesabu kila dakika, tizama hii dakika ya mwisho orodha ya kufanya kuhakikisha uko tayari asilimia 100.

pregnancy last minute list

List Orodha ya dakika ya mwisho ya ujauzito

Osha nguo zote za mtoto wako

Hata kama ni mpya kutoka dukani, nguo zote za mtoto zinapaswa kuosha kabla ya mtoto kuzivalia. Watu wengi wamegusa nguo hizi kabla yako kuzinunua na ni vyema kuwa salama.

pregnancy last minute list

Eua chupa za mtoto wako

Hatua hii kwa mara nyingi hupuuzwa ama kuto zingatiwa kwa sababu tunafikiria kuhusu kuosha chupa baada ya kuwa na uchafu unao onekana ama baada ya kutumika. Walakini, kama nguo, hata chupa mpya huwa zimeguswa na mikono mingi na ni vyema kuwa salama.

pregnancy last minute list

Nunua padi za chuchu

Baadhi ya wamama wa mara ya kwanza hawajui kuwa hizi zinahitajika - ila ni muhimu sana. Padi za chuchu hulowa maziwa ya mama yoyote yanayo baki ama kumwagika. Zinafanya tofauti kubwa kati ya sharti kuwa na unyevu na kutokuwa nao.

Angalia betri iwapo zinafanya kazi

Kiti ulicho mnunulia mtoto wako kilikuja na betri ama bado kinazihitaji? Na bouncer yake je? Simu ya kitanda chake je? Ni vyema kuto puuza na kudhani kuwa betri zote zinafanya kazi. Huenda ukajipata kwenye hali ambapo huwezi tumia kiti chake unapo kihitaji zaidi.

Buy car seats

Kiweke kiti chake cha gari

Weka kiti chake cha gari na uhakikishe kimefungwa ipasavyo na kiko salama. Jaribu kukitoa na kukirudisha kama vile ambavyo utakavyo fanya mara milioni kwenye miaka michache ijayo. Kwa hivyo ni jambo la busara kustareheka unapolifanya jambo hili.

Begi ya hospitali

Angalia mara mbili kuhakikisha kuwa uko na kila kitu unachohitaji kwenye begi yako ya hospitali. Usipuuze vitu kama chaja ya simu, camera na betri na vitu vinginevyo. Iwapo wewe ni mzazi wa mara ya kwanza, huenda ukaweka vitu vingi zaidi. Usijali, ni sawa. Ni vyema zaidi kuwa na vitu vingi badala ya kusahau kitu muhimu.

Pumzika

Jaribu na kutilia maana jambo lingine tofauti na kujifungua kwa mtoto wako kunako karibia. Najua ni vigumu sana, ila, jaribu tu. Ufurahie muda wako kama mume na mke kabla ya maisha yenu kubadilika.

orodha ya dakika ya mwisho ya ujauzito

Pelekwa mahali pema ule, soma kitabu, lala ama hata uende upate masi kabla ya kujifungua. Unapaswa kufurahia wakati wako peke yako, kadri uwezavyo - maisha kama ujuavyo yako karibu kubadilika - yawe mazuri bila shaka!

 

Soma Pia: All You Need To Know About C-Section Recovery: Care And Tips

Makala haya yaliandikwa na Prianka na kuchapishwa tena na idhini ya theAsianparent kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio

Written by

Risper Nyakio