Nyimbo Maarufu Na Za Kusisimua Za Kuwafunza Watoto Wako

Nyimbo Maarufu Na Za Kusisimua Za Kuwafunza Watoto Wako

Kuna orodha kuu ya nyimbo za ibada za kuwafunza watoto. Kuwasaidia watoto kutengeneza makumbusho ya umri wao walipokuwa watoto. Kuna hisia nzuri na za mapenzi unapo kuwa na watoto wadogo wakiimba nyimbo za ibada. Na jambo la kusisimua zaidi wanapo sakata densi na kuimba nyimbo hizi.

Muziki si wa kujiburudhisha tu. Kupitia kwa nyimbo, watoto wanaweza soma vitu muhimu sana maishani. Ama huenda ikawa ni chanya cha kuhakikisha kuwa wana jambo la kufanya wakati wa likizo. Uwezo wa watoto hutofautiana. Unapo chagua nyimbo za ibada, ni muhimu kuangazia kwa makini umri wa mtoto wako. Unaweza pata nyimbo za kusisimua za ibada, ambazo ni rahisi kwa mtoto kuimba.

Orodha ya nyimbo za ibada za kuwafunza watoto

Na orodha inayo fuata hapa chini, ni makumbusho ya nyimbo za hapo awali. Kuna uwezekano mkubwa kuwa uliimba moja wapo ya nyimbo hizi ulipokuwa mdogo.

  1. Imela wimbo ulio imbwa na Nathaniel Bassey

 

Wimbo huu maarufu wa Imela ni maarufu kwa watu wengi na unawafaa watoto.

Ni wimbo wa ibada ulio andikwa na Nathaniel Bassey na ulio achiliwa mwaka wa 2014. Umejulikana sana na kuimbwa katika kanisa nyingi.

2. Father Abraham ulio imbwa na Pierre Kartner

 

Huu ni mojawapo ya nyimbo zinazo pendwa zaidi na watoto. Pierre Kartner ni mwana muziki wa Dutch, ni mwandishi wa nyimbo na pia ana jukumu la kutoa nyimbo. Jina lake la ki usanii ni Vader Abraham (father Abraham). Anajulikana sana kwa jina hili baada ya kuandika wimbo maarufu wa Dutch wa Baba Ibrahimu alikuwa na vijana saba. Alipo kuwa na ndevu refu na kofia na hii ikawa kama kitambulisho chake.

3. This Little Light of Mine ulio imbwa na Harry Dixon

Hata kama mtu mzima, huenda ikawa vigumu kwako kuwa hujawai kusikia kuhusu wimbo huu hasa kama unatoka Nigeria. Wimbo huu wa This Littel Light of Mine ime imbwa kwa njia tofauti kwa miaka iliyo pita. Unaweza changanya kidogo mnapo imba na watoto. Wimbo huu uliandikwa katika miaka ya 1920 na Harry Dixon Loes na baadaye ukachukuliwa na Zilphia Horton.

4. Excess Love wimbo wa Mercy Chinwo

 

Kuna ushuhuda mwingi sana ulio ibuka kutokana na wimbo huu. Ni kumbusho muhimu la mapenzi ya Mungu kwa watoto wake. Watoto pia wanapenda wimbo huu kwa sababu ya urudiaji ulio nao.

5. He's got the Whole World in his Hands wimbo wa Laurie London

 

Wimbo huu ulipata umaarufu wa kidunia katika mwaka wa 1957-58 kwenye rekodi ya mwimbaji wa kimombo, Laurie London. Uli ibua matamshi ya wa-marekani wa kiafrika na umekuwa moja wapo ya nyimbo zinazo julikana na kupendwa zinazo imbwa na wazee kwa vijana kila mahali. Wimbo huu una tofauti nyingi kwenye matamshi na maandishi kama nyimbo zingine zinazo ibuka kwenye matamshi ya kitamaduni.

6. I know who I am wimbo ulio imbwa na Sinach

Huu ni wimbo wenye nishati sana, watoto wanapenda kusakata. Pia ni wimbo mkuu unao wapatia watoto ujasiri mwingi.

Soma pia: Nigerian Worship Songs: Songs to teach your kids

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Lydia Ume kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

 

Written by

Risper Nyakio