Je, Kuna Tatizo Katika Ulezi wa Kisasa Nchini Kenya?

Je, Kuna Tatizo Katika Ulezi wa Kisasa Nchini Kenya?

Kadri miaka inavyo zidi kupita, ndivyo ulezi unavyo zidi kubadilika. Maisha na mambo yanayo tendeka yana badilika. Na hivi kufanya wazazi wa badili mfumo wao wa ulezi ili uafikiane na wakati tunaoishi. Kume kuwa na sababu nyingi zinazopelekea katika mabadiliko ya uzazi. Kama vile ngezeko la gharama ya maisha, kuyaiga mambo ya ugenini, usasa na mengineyo. Watu wengi wametoka mashinani na kuhamia mitaani. Na kuwaacha wavyele wao vijijini. Unapata kwamba hakuna anaye watunza mjini na kuhakikisha kuwa wana fuata maagizo muhimu waliyo funzwa wakikua. Tuna angazia parenting in Kenya.

parenting in kenya

Familia ya kisasa. Picha shukrani kwa shutterstock

Sababu zinazo fanya ulezi nchini kubadilika: Parenting in Kenya

Muingiliano

Tofauti na hapo awali ambapo watu waliishi mahali waiko zaliwa mpaka wakakua, siku hizi mambo ni tofauti. Watu wanatoka sehemu mbali mbali nchini na kuishi mjini. Kila mmoja ana mila na itikadi tofauti na pia wanalivyo lewa ni tofauti. Unapata kuwa kutokana na kuingiliana huku, watu wana iga tabia tofauti na pia kuanza kuamini na kutenda mambo yaliyo tofauti na waliyo zoea. Muingiliano una athari chanya kama vile kupata marafiki wapya na kujua njia yao ya maisha. Pasi na mipaka, unapata kuwa watoto hawa wana iga hata mambo yasiyo faa. Ni muhimu kuwa huru na mtoto wako na kumwelezea mambo yalivyo bila fiche ili wawe na maarifa ya mambo mema ya kuiga na yasiyo faa.

Teknologia

Miaka ya kale, hakukua na teknologia nyingi. Watoto walikua wakiamini walicho ambiwa na wazazi wao na kufuata njia za kuishi zilizo kubalika kwenye jamii na kijiji. Tabia njema na nidhamu zilipewa kipau mbele na kuangaziwa. Hivi sasa, teknologia imepaa, kila mtu, wakubwa kwa wadogo wanao ishi mashinani na walio mijini wote wanaitumia teknologia. Teknologia ina athari hasi na chanya. Zote ambazo zina athiri ulezi na jinsi kila mzazi anaingiliana na watoto wake. Siku hizi teknologia ina athiri kwa vikuu unavyo walea watoto wako. Huenda ukamfunza mtoto wako tabia njema na heshima ila kwa kupitia mtandao, anajua mambo tofauti na kuanza kuziiga tabia hizi zisizo faa.

Ni muhimu kwa kila mzazi kuwa na mazungumzo wazi na watoto wake na kuwaeleza kinaga ubaga jinsi mambo yalivyo. Jaribu kadri uwezavyo kuwalea vyema ipasavyo na watakumbuka ushauri wako hata wakiingiliana na wanarika wao wenye tabia zisizo kubalika kwa jamii.

parenting in kenya

Picha shukrani kwa shutterstock

Wazazi kupatia kazi kipau mbele

Kumekuwa na mabadiliko mengi, kama vile gharama ya maisha kuenda juu. Hivi kufanya vitu vingi kuwa na bei ghali zaidi. Inabidi wazazi wafanye kazi mchana na usiku ili wakimu mahitaji ya wanao na kuhakikisha kuwa hawakosi mahitaji yoyote wanayo taka. Hata kama ni vyema kufanya kazi kwa bidii ili kuwalisha na kuwavisha wanao, ni muhimu kuhakikisha kuwa tabia za mtoto zina undwa anapokuwa nyumbani. Kuwa makini zaidi na watoto wako na uhakikishe kuwa unateka wakati tosha ili uweze kuwa na watoto wako. Pia waeleze na uwafanye waamini unachofanya na kuwa unajaribu kuwatafutia maisha mema. Usikubalishe kazi yako iingie kati yako na watoto wako.

Aina ya mzazi

Kuna aina ya wazazi tofauti. Kama vile, wanao sikiza, wa masharti, wazazi huru. Aina ya mzazi uliye ina adhiri pakuu ulezi wako na jinsi mtakavyo husiana na mtoto wako. Wazazi wa kusikiza, huwa sikiza watoto wao kisha kuwashauri. Wazazi wa masharti hawaingiliani vyema na watoto wao kwani wanataka watoto wao wafuate masharti yao bila kusikiza ama kuulizwa maswali. Wazazi huru wamewaachilia watoto wao wafanye mambo yote watakayo bila kujali. Mtoto hana dhibiti yoyote ya mambo ayafanyayo kwani wakati mwingi wako kazini ama wana shughuli zao wanazo fanya. Watoto kama hawa unapata kuwa wana fanya na kuiga tabia zozote zile wanazo pata zikifanywa na marafiki wao. Wazazi wao hawatengi muda kuongea nawao na kuwashauri. Ni muhimu kwa kila mzazi kujua ulezi bora zaidi na ahakikishe kuwa wanaongea na watoto wake, na pia mara kwa mara, ni vyema kuwa adhibu kulingana na umri wao. Wasije wakamea pembe sana.

parenting in kenya

Wazazi wa kuadhibu. Picha shukrani kwa shutterstock

Ni bayana kuwa, kuna tatizo la ulezi nchini kwa kimombo parenting in Kenya. Watoto wanakosa nidhamu wanapokosa ushauri kutoka kwa wazazi na walezi wao. Ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha kuwa anawaangalia watoto wao na wanapo kosa kufanya mambo yanayo takikana, unawalinda ili wafanye mambo mema.

 

Chanzo: Standard media

Written by

Risper Nyakio