Matatizo Ambayo Wanafunzi Wa Kike Wanakumbana Nayo Wanaposhuhudia Hedhi

Matatizo Ambayo Wanafunzi Wa Kike Wanakumbana Nayo Wanaposhuhudia Hedhi

Hedhi inapaswa kuwa muda mwema kwa wasichana ila kwa watoto wa kike kutoka madongoporomoka nchini wana tupilia mbali masomo kwa sababu ya kipindi hiki.

Mary Asigi, mwanfunzi wa shule ya msingi ya Damascus iliyoko kwenye madongoporomoka ya Dandora ana miaka 17 na katika darasa la saba. Kwake na wanafunzi wa kike wenzake, ni jambo la kawaida kukosa kuhudhuria darasa siku chache kila mwezi. Je, kisa na maana ni nini? Jiunge nasi tukupashe zaidi katika safari yetu ya kuangazia period poverty in Kenya.

Umasikini wa Hedhi Nchini: Period Poverty in Kenya

period poverty in kenya

Picha shukrani kwa shutterstock

Binti anapofikisha umri wake wa utu uzima, anaanza vipindi vyake vya hedhi ambavyo hutendeka kila mwezi. Katika sehemu za madongoporomoka nyingi nchini, familia nyingi zina tatizika kukidhi mahitaji yao ya kimsingi. Kama vile kuwa na nyumba nzuri, kuwa na nguo tosha, kulipa karo ya shule, ama kununua lishe. Kwa familia nyingi zinazo ishi katika sehemu hizi, wana tatizika hasa kununua chakula cha kutosha cha wanafamilia. Na kwa kawaida kwa siku wanatumia chini ya shilingi 100. Kudhibitisha hali yao ya umasikini.

Je, ikiwa wana tatizika kununua chakula, itakuwaje kuhusu kununua shodo/ vitambaa vya hedhi? Ni vigumu kwa wasichana wanao ishi katika sehemu hizi kuwatajia wazazi wao kuhusu kununua shodo. Ni ngumu kuenda shuleni wanapokuwa kwenye vipindi hivi. Na mara nyingi kuwalazimisha kubaki nyumbani wanapo shuhudia hedhi yao. Ili kuepuka kufanyiwa mzaha na wanafunzi wa kiume shuleni. Kuna visa vya wasichana ambao walitupilia masomo yao mbali baada ya kufanyiwa mzaha na kuchekelewa na wanafunzi wa kiume shuleni walipo shuhudia hedhi yao.

Jambo hili linapelekea katika matokeo duni kwa wanafunzi wa kike. Unapokosa kuenda shuleni siku hadi 7 kwa mwezi kwani u-katika hedhi yako. Kwa mwaka wanakuwa wamepoteza siku 165. Nchi ya Kenya ina watu milioni 50 na miongoni mwa hawa, zaidi ya wanafunzi milioni 1.2 nchini hutupilia masomo mbali. Jambo la kusikitisha zaidi kwani masomo ni hitaji la kimsingi kwa kila mtu. Ila baadhi ya wazazi wanasshindwa kutimiza takwa hili. Serikali pia inapaswa kuhakikisha kuwa hakuna mtoto nchini anaye kosa  haki yake ya masomo.

Mara nyingi, ukosefu huu wa shodo, umepelekea wanafunzi hawa wa kike kuwasaidia marafiki wao na vitambaa ambavyo wametumia. Jambo la kusikitisha na kughadhabisha zaidi kwani wanaihatarisha afya yao na pia haizingatii usafi wa mwili. Idadi kuu ya watu wanao ishi sehemu hizi, asilimia 12 ya watu hawa wanaugua virusi vya ukimwi.  Kwa hivyo kuwa weka katika hatari ya kuambukizwa virusi hivi.

Hatua za Serikali Kuu Kukumbana na Period Poverty in Kenya

Matatizo Ambayo Wanafunzi Wa Kike Wanakumbana Nayo Wanaposhuhudia Hedhi

Dawati kubaki bure baada ya wasichana wengi kukosa kwenda shuleni. Picha shukrani kwa shutterstock

Licha ya wanafunzi hawa kutatizika hivi vyote, wana hamu ya kusoma na kutimiza ndoto zao za kuisaidia familia yao nan chi yao. Ila je, familia na serikali wanayo taka kusaidia wakimaliza masomo yao inawasaidia kweli? Serikali ya Kenya imechukua hatua kuhakikisha kuwa inakumbana na tatizo hili. Miaka michache iliyopita, Kenya ilipitisha sera ya kuto lipisha kodi kwa vifaa vyote vya shodo za wanawake na wasichana. Serikali iliapa kutoa shilingi milioni 3 ili kusaidia kuhakikisha kuwa wanafunzi wa kike kutoka kwa familia maskini wanapata shodo kila mwezi. Serikali ilianza mradi mnamo mwezi wa Aprili mwaka wa 2018 wa kupeana shodo milioni 140 kwa wasichana milioni 4.2 walioko nchini kote.

Ila, mradi huu uliendelea kwa muda wa miezi mine tu kisha ukafilisika na kuisha, na mtindo wa wanadada kukosa kwenda shuleni kama hapo awali ukarejea.

Sababu kwa kufilisika kwa mradi huu wa serikali

Kuna sababu tofauti zilizo ufanya mradi huu kutoka kuwa na mafanikio. Baadhi ya sababu hizi ni kama vile:

Wasambazaji walio zawadiwa kazi hii kuto tekeleza wajibu wao.

Ilikuwa vigumu kwa serikali kupata watu wengine wa kupata wasambazaji wengine na kufanya mradi huu kusimama. Kisa kingine ni kama vile kusambazwa kwa idadi ndogo ya shodo chini ya kiwango kilicho hitajika. Na kuwafanya wasichana kupata vipande vidogo vya vitambaa hivi, wakati ambapo wengine walivikosa. Jambo kuu lililo ufanya mradi huu kufilisika ni kiwnago cha juu cha ufisadi kinacho shuhudiwa nchini. Baadhi ya vipande vya shodo hizi zilizo kusudiwa kusambazwa kwa wasichana kutoka kwa familia zisizo jiweza, ni kuibiwa kisha kuuzwa kwa shodo hizi.

Matatizo Ambayo Wanafunzi Wa Kike Wanakumbana Nayo Wanaposhuhudia Hedhi

Picha shukrani kwa shutterstock

Ufisadi uliokidhiri mipaka

Serikali inapaswa kukumbana na tatizo la ufisadi na kuangalia jinsi raslimali zilizo tengwa kwa mradi wa kusambaza shodo kwa wanafunzi wa kike. Ili kuhakikisha kuwa wasichana wote nchini wanapata shodo hizi kila mwezi na hawakosi kwenda shuleni. Ili wapate masomo, na waweze kutimiza lengo na ndoto zao maishani. Pia ni muhimu kuwafunza wanafunzi wa kiume kuhusu hedhi na jinsi wanapaswa kuwasidia dada zao shuleni iwapo kipindi chao kianze wakiwa darasani. Pia, kuto wacheka na kutowafanyia mzaha wana dada wanao shuhudia hedhi yao.

Serikali kuto wajibika

Ni jambo la kawaida kuhakikisha kuwa baada ya kuanza mradi fulani, unafuatilia kuhakikisha kuwa mambo yote yako shwari. Kuwa kila mtu aliye patiwa kazi katika mradi huo anafanya wajibu wake. Ila, baada ya kuanza mradi huu, serikali haukufuatilia kuhakikisha kuwa mambo yote yako shwari.

Mary mwanafunzi wa shule ya msingi ya Damascus anakaa kwenye dawati lake na kuhuzunika, “Laiti ningekuwa mtoto wa kiume, singewai kosa darasa ama shule. Ningecheza na wanarika wangu kwa uwazi na kufanya vema kwenye mitihani yangu kisha nijiunge na jeshi la wanamaji, ili niisaidie familia na nchi yangu.” Alisema huku huzuni imetanda usoni mwake.

 

Chanzo: Aljazeera

Written by

Risper Nyakio