Kama mzazi mzuri, unamtakia mwanao mazuri, na mazuri haya huja na gharama. Mavazi, chakula, vitabu, vidoli, mazoezi, elimu bora na vinginevyo. Kitita kikubwa cha pesa za kifamilia kinatumika kwa watoto wako. Watoto ni gharama kubwa. Njia pekee ya kuto kwama unapowalea ni kwa kutenga asilimia fulani ya pesa ya siku za usoni. Kuwa tayari kwa mahitaji yajayo kunamaanisha kupanga kwa usiyoyatarajia leo. Huenda ukashinda kitita cha pesa kesho, ama huenda mwenzio akapoteza kazi yake na mkabaki bila hela. Lakini ukiwa na mfumo mzuri wa kuhifadhi pesa, mambo yasiyotarajiwa ya kimaisha hayawezi kuathiri watoto wako na urithi unaotengeneza.
Ni njia zipi bora kwa wazazi kupangia maisha ya usoni ya watoto wao walio na gharama chungu nzima.
Utaratibu huu utakusaidia kuhifadhi fedha ambazo mtoto wako atahitaji kuanzisha maisha yao ya kujitegemea kifedha.
Pesa Za Kifamilia: Mbinu Za Kuhifadhi Pesa

Jinsi unavyo hifadhi pesa kwa miaka mingi, ndivyo utakavyo kuwa na pesa nyingi. Ni muhimu hasa kama pesa ulizo nazo zitakuwezesha kuwaelimisha watoto katika chuo kikuu. Katika kesi hii, kuanza mapema sio chaguo. Inapofika kwa kuhifadhi pesa na kuziwekeza, wakati bora ni hivi sasa. Hakuna wakati sawa wa kuanza. Kuanza sasa kunazipatia pesa zako muda zaidi wa kukua. Unaweza hifadhi kiwango kidogo kila wiki ama mwezi. Usingoje hadi unapokuwa na pesa nyingi.

Kiwango unachoamua kutenga kila mwezi ama wiki, hakikisha kuwa kinatosha kukimu hitaji moja ama zaidi ya watoto wako. Pia, kuwa na uhakika kuwa unastarehe kutenga kiwango hicho, kwani hakuna haja ya kutenga kiwango kikubwa kisha unapokuwa na suala, unakimbilia pesa hizo. Pia, kiwango hiki hakipaswi kuingilia kati mpango wa kuhifadhi pesa ulio nao wa kibinafsi.
- Badili mfumo wa kuhifadhi pesa mara kwa mara
Nini kinacho fanyika mtoto wako anapoamua kuwa hataki kujiunga na chuo kikuu? Huenda wakawa wangependa kuwa wapishi kama njia ya kukimu mahitaji yao. Dunia inabadilika na badala ya kutafuta makazi, watu wengi wanafungua biashara ndogo. Kuna njia tofauti za kuwekeza ambazo unaweza tumia kama kununua shamba ambayo dhamani yake itazidi kuongezeka ama kwa treasury bills.

Bidii zako za kuhifadhi pesa ni fursa ya kumfunza mtoto wako kuhusu pesa. Katika kipindi kimoja maishani, watakuwa peke yao, kwa hivyo, mbona usiwaelimishe mapema? Wafunze dhamana ya pesa na uwasaidie kuwa na matarajio yanayotimizika. Wahusishe katika mchakato wa kuhifadhi pesa. Anzia mapema kwa kuwanunulia piggy bank, watakapokuwa wakirusha visenti vichache.
Kuchukua hatua hizi za kuhifadhi pesa za kifamilia kutamsaidia mwanao kuwa na uchaguzi zaidi maishani na kutimiza uhuru wa kifedha.
Chanzo: Woman's Day
Soma Pia: Jinsi Ya Kufunza Watoto Kuhusu Pesa Na Jinsi Ya Kufanya Bajeti