Sote tunapenda pongezi, siyo? Haijalishi iwapo ni ofisini ama nyumbani kwa kuwa mzazi mzuri, mtoto ama mchumba mwema. Angalau, hiyo ndiyo picha ambayo wengi wetu tunayo akilini. Pongezi inadhihirisha kazi yako ina kubalika. Inaonyesha kuwa watu kando yako wana thamini juhudi zako. Na wakati ambapo hutafanikiwa wakati wote, pongezi itakupatia motisha ujaribu kufanya vyema zaidi. Wakati ambapo tunapenda pongezi, je, tunachukua muda kuwapongeza wengine? Ni mara ngapi tunawapongeza wanawake walio maishani mwetu? Wanawake wengi wanatarajia maneno chanya kutoka kinywani mwako. Soma zaidi kuhusu pongezi ambazo wanawake wanapenda kusikia.
Pongezi ambazo wanawake wanapenda kusikia

- Wewe ni mama mzuri
Baada ya miaka mingi ya juhudi na kujitolea, kukosa usingizi, na kukutunza. Ni rahisi kusahau juhudi zote alizotia katika ukuaji wako, lakini unaweza samehewa unapo mpongeza. Haijalishi iwapo wewe ni mzee ama mchanga. Atafurahia.
2. Wewe ni fahari yangu
Iwapo ni mama anayefanya kazi, mke, dada ama hata rafiki. Waambie hivi mara kwa mara. Ni mojawapo ya pongezi ambazo wanawake wanapenda kusikia. Hasa kwa dunia ambapo wanaume wengine wanaweza penda kupuuza juhudi za wanawake. Unawapatia motisha kuzidi kutia juhudi kazini zao na maishani pia.
3. Napendelea unavyofikiria
Baadhi ya wakati, ni rahisi kunyamazisha mtu kwa sababu hawaonekani kuwa na maarifa. Cha kuhuzunisha ni kuwa tumefanywa kufikiria kuwa wanawake ndiyo watu hao. Lakini tunafahamu kuwa wanawake ni watu shupavu sana. Haijalishi iwapo ni ofisini ama nyumbani. Fanya juhudi ya kuwapongeza mara kwa mara.
4. Napenda ulivyo na motisha

Baadhi ya wanawake hupenda mazuri zaidi kwa familia zao. Haijalishi iwapo ni mamako ama bibi yako, atakaye fanya kila kitu nyumbani kuhakikisha kila kitu kiko shwari. Baada ya kazi zote, atakuwa amechoka na kukwazwa kimawazo, hii ndiyo sababu kwa nini maneno machache ya pongezi yataboresha motisha yake.
5. Nasoma kutoka kwako kila siku
Uhusiano ni kuhusu kufanya kazi kama timu. Mnabadilishana mawazo, kazi, na kucheka pamoja. Kufanya hivi kunakusaidia kukua kama mtu binafsi. Mchumba wako anapaswa kukuegemeza wakati wote. Kwa hivyo mwambie kuwa unafurahia juhudi zake na anachofanya maishani mwako.
Hakikisha kuwa unamwambia asanti mara kwa mara. Watu wanapoishi pamoja kwa muda na kuzoeana, ni rahisi kuona kana kwamba anachokufanyia ni haki yako. Hilo sio kweli. Kumshukuru kutafanya aone kuwa anathaminiwa na atie juhudi zaidi kwa anayofanya.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Njia Tofauti Za Uzazi Wa Mpango Ambazo Wanandoa Wanaweza Kutumia