Hali ya preeclampsia ni tatizo katika ujauzito linalo dhibitishwa na shinikizo la juu la damu. Viungo vingine vya mwili kama mafua, maini na moyo huenda vika athiriwa pia. Kwa wanawake wengi, hali hii huanza wanapo fikisha muda wa wiki 20 katika mimba. Preeclampsia katika mimba isipo dhibitiwa huwa na matokeo hasi kwa mama na fetusi inayo kua tumboni.
Vyanzo vya preeclampsia

Kuna sababu nyingi zinazo sababisha hali ya preeclampsia. Kulingana na wataalum, hali hii huanza kwenye placenta. Inayo kuwa na jukumu la kulisha mtoto na kumpitishia virutubisho muhimu na hewa. Mwanamke anapo tunga mimba, mishipa mipya ya damu huibuka kupitisha damu kwenye placenta. Kwa wanawake walio na hali ya preeclampsia, mishipa hii haikui wala kutekeleza majukumu yake. Kwa sababu hii, damu haifiki kwenye placenta, ama kiwango kinacho fika ni kidogo sana. Ukuaji wa mishipa hii una athiriwa na geni za mama, kuharibika kwa mishipa ya damu, na matatizo katika mfumo wa kinga.
Ishara za preeclampsia
- Maumivu makali ya kichwa
- Mabadiliko kwa uwezo wako wa kuona, kuto ona vizuri
- Kuhisi kichefu chefu
- Maini kuto fanya kazi vyema
- Kutatizika kupumua
- Maini kuto fanya kazi yanavyo paswa
- Kukwama kwa maji kwenye mafua
Walio katika hatari ya kupata preeclampsia

Wanawake wenye hali hizi wako katika hatari zaidi ya kuugua hali ya preeclampsia.
Wanawake walio katika familia ambapo kuna historia ya kuugua preeclampsia wana hatari zaidi ya kuugua ugonjwa huu.
Mwanamke aliye katika mimba yake ya kwanza ako katika hatari zaidi ya kuugua hali hii.
Wanawake wanao tunga mimba wakiwa na umri wa zaidi ya miaka 35 wako katika hatari zaidi ya kuugua ugonjwa huu.
Hatari ya ugonjwa huu ni zaidi kwa wanawake walio na uzito mwingi wa mwili.
- Mimba ya mtoto zaidi ya mmoja
Kwa wanawake wenye ujauzito wa mtoto zaidi ya mmoja, hatari ya kupata ugonjwa huu iko juu.
Mwanamke anapo pata mimba na mchumba tofauti, anajiweka katika hatari ya kupata hali hii.
Ni muhimu kwa mama mwenye mimba kufuata ratiba ya kliniki bila kukosa. Kwa njia hii, daktari atafanya vipimo kila mara kuangalia iwapo mama ana matatizo ama hali zinazo ibuka. Kwa mama aliye shuhudia hali ya preeclampsia katika mimba anapaswa kuwasiliana na daktari kabla ya kutunga mimba tena. Hakikisha kuwa una jitunza ukiwa na mimba ili kuwa na safari salama ya mimba.
Soma Pia: Je. Kuna Uwezekano Wa Mayai Kupevuka Mapema Katika Mimba?