Rais wa tatu wa nchi ya Kenya, Emilio Mwai Kibaki afariki. Kifo chake kimetangazwa na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika press briefing siku ya Ijumaa Aprili tarehe 22 mwaka wa 2022.
Picha: The Nation
“Ni siku ya huzuni kwetu kama nchi. Tumepoteza kiongozi mkubwa, raisi wa zamani mzee Mwai Kibaki, rais Uhuru Kenyatta alisema.
“Alikuwa mtu wa heshima na hadhi ambaye maisha yake yatazidi kuwahamasisha wananchi wa Kenya muda katika siku zao za usoni. Tunakumbuka maadili aliyofuata maishani, heshima yake, uangalifu wake, kuhusika kwake kuhusu ustawi wa wakenya wote. Kama mmojawapo ya watu walioongoza nchi baada ya kupata uhuru, rais Mwai Kibaki alipata heshima na mapenzi kutoka kwa wananchi na nchi zingine duniani kote. Daima atakumbukwa kama mtu mashuhuri katika siasa za Kenya ambaye weledi, ujasiri na maarifa yake yalishinda kila siku, muda baada ya mwingine,” rais Uhuru alizidi kusema.
Picha: The Nation
Kamwe hatasahaulika kwa yote aliyochangia alipokuwa waziri wa fedha, mdogo wa rais na rais wa nchi ya Kenya. Katika uongozi wake kama rais wa nchi, uchumi ulishuhudia ustawi mkubwa, ambao kamwe haujaweza kudhihirika muda baada ya uongozi wake.
Kama rais, aliapa kuondoa utoaji rushwa uliokuwa umeharibu ustawi na uchumi wa nchi, uliokuwa umefanya nchi za nje kutosaidia Kenya. Kibaki aliongoza nchi kutoka mwezi wa Disemba mwaka wa 2007 hadi Aprili mwaka wa 2013.
Marehemu raisi wa zamani Mwai Kibaki atakumbukwa kwa mengi aliyotimiza alipokuwa rais, weledi wake, utulivu wake, ujasiri wake katika uongozi wake na bila shaka ucheshi wake.
Amefariki akiwa na miaka 90. Lala pema peponi rais Mwai Kibaki.
Chanzo: Citizen
Soma Pia:Harusi Ya Kufana Ya Rita Dominic na Fidelis Anosike