Ungependa Msaada Kukipanga Chakula Chako? Tazama Ratiba Hii Ya Chakula Cha Nigeria

Ungependa Msaada Kukipanga Chakula Chako? Tazama Ratiba Hii Ya Chakula Cha Nigeria

Tizama mwongozo huu wa lishe bora!

La kuhuzunisha ni kuwa, teknolojia yetu ya njia katika dunia hii imefanya karibu iwe vigumu kwa familia za wana Nigeria kula vyakula vya afya pamoja katika manyumbani mwao wakati wote. Ratiba kali zina walazimisha wazazi kula kiamsha kinywa na chamcha kwenye hoteli za kazini. Mara nyingi, watoto hula chamcha shuleni ama kwenye hoteli za vyakula vya kubeba. Wengine hula chakula cha jioni kwenye magari yao kwa sababu wame kwama kwenye trafiki. Hii ndiyo sababu tumetengeneza mwongozo wa ratiba ya chakula cha Nigeria; ikiwa ungependa ratiba yako mwenyewe.

nigerian meals time table

Kwa kutumia ratiba yetu ya chakula cha Nigeria, utakuwa ukila vyakula tofauti vyenye afya.

Tatizo lingine kuu linalo athiri jinsi tunakula huku Nigeria ni kuwa tuna kula chakula kimoja kwa muda mrefu. Familia nyingi zinabaki kula wale, maharagwe, eba. Hayo ni yote. Ni vigumu kwao kuongeza hiari kama vile soya, kunde, mtama, wanga wa gunea kwenye lishe zao. Iwapo wewe ni m-Igbo, unabaki kula chakula cha ki-igbo. Ni vigumu kumpata mtu akijaribu vyakula vya tabaka zingine.

Kulingana na World Cancer Research Fund International, tabia hizi za kula lishe isiyo na afya zili sababisha ongezeko katika maradhi sugu na hata vifo vilivyo sababishwa na kisukari, shinikizo la juu la damu na maradhi mengine.

Kwa familia nyingi zinazo fanya kazi, ni vigumu kula kiamsha kinywa, chamcha na chajio nyumbani hadi pale wikendi inapo fika. Ila, hili halimaanishi kuwa familia haziwezi nufaika kutokana na ratiba ya chakula cha Nigeria iliyo pangika.

Tazama sampuli hii ya ratiba ya chakula cha Nigeria zinazo liwa sana

nigerian meals Time Table

Nigeria ina utajiri mwingi wa kilimo. Mashamba yana rutuba, na ni vigumu kukupambana na janga za kiasili. Kuna vyakula vingi vilivyo na utajiri huku Nigeria hasa upande wa Kaskazini. Kwa kujaribu vyakula vya kitamaduni vya kabila zingine, tunaongeza na kutajirisha lishe zetu kwa njia nyingi.

Kwenye makala haya, tuna angazia ratiba ya chakula cha Nigeria cha familia zinazo taka kula lishe bora na yenye afya.

Bakshishi: Ni sawa kupika vyakula vyako na kuvihifadhi kwenye chombo ili ule unapokuwa ofisini ama shuleni. Kwa njia hii, unaweza hakikisha kuwa familia yako inalishwa lishe bora na zenye afya.

Bila shaka, ratiba hii ya chakula cha Nigeria ya wiki sio takatifu na wala sio lazima. Kadri iwezekanavyo, kuwa mbunifu na lishe zako, kwa kutumia mwongozo huu wa ratiba.

Chochote utakacho kifanya, hakikisha kuwa lishe yako ina aina zote za chakula. Wana Nigeria wengi kwa mara nyingi hula wanga sana na matunda na mboga kidogo. Ratiba iliyo na ujumbe mwingi kwenye orodha yako inapaswa kuifanya iwe rahisi kwa familia zinazo taka kula lishe bora.

Kula vyakula vyenye afya kunahusisha zaidi ya kufuata ratiba tu, Pia inahusisha kula viwango sawa vya mboga, matunda na kuhakikisha unatimiza malengo yako ya kila siku ya vinywaji.

Lishe zetu za Nigeria za kawaida zinaendelea na bakshishi za kula za afya kwa familia za ki Nigeria:

nigerian meals time table

 1.  Kula matunda mengi. Kuwa na uraibu wa kuijaza nyumba yako na matunda. Anzisha matunda kwa watoto wako na uwahimize kula lishe bora.
 2. Kunywa glasi ya maji punde tu unapo amka. Unaweza endelea na ule kiamsha kinywa na bakuli yenye matunda tofauti baada ya kumaliza. Ukikunywa maji na kula matunda asubuhi, uko sawa kuanza siku yako. 
 3. Kula lishe yako ya mwisho kabla ama saa moja za usiku. Iwapo utahisi njaa hapo baadaye, kunywa chai ama chokleti moto na ule matunda.
 4. Kunywa maji dakika 30 kabla ama baada ya lishe yako.
 5. Iwapo lazima uchukue kinywaji unapo kula, kunywa maji badala ya pombe ama vinywaji vitamu. Ina saidia kukichakata chukula tumboni.
 6. Glasi yako ya maji sio lazima yawe baridi zaidi. Kunywa maji yenye joto ya chumbani.
 7. Kupika kwa kutumia kiasi kidogo cha mafuta.
 8. Fanya kila kitu kwa utaratibu. Kiasi kingi ama kidogo cha chakula, matunda ama maji huenda kika kufanya uwe mgonjwa.
 9. Chai na kahawa ni bora zaidi kuepukika lisaa limoja kabla ama baada ya lishe yako.
 10. Kula ukiwa umekaa wima. Usilale unapo kula.
 11. Tafuna pole pole kabla ya kumeza ili kuufanya utaratibu wa mchakato wa chakula hicho tumboni kuwa rahisi.

Kumbu kumbu: World Cancer Research Fund International 

Soma pia: Tips for mums travelling with multiple kids

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio