Lishe Ya Ujauzito: Ratiba Ya Chakula Cha Ujauzito Cha Nigeria

Lishe Ya Ujauzito: Ratiba Ya Chakula Cha Ujauzito Cha Nigeria

Hivi ndivyo vyakula unavyo paswa kula unapokuwa mjamzito.

Lishe bora ni muhimu kwa kila mtu, ila kwa wanawake wajawazito, ujauzito utahitaji lishe bora kwa mama na mtoto. Chakula cha Nigeria kina wingi wa virutubisho; kuna kila kitu cha kila ladha, hata katika wakati dharura wa ujauzito. Hii ndiyo sababu tumetayarisha ratiba ya chakula cha ujauzito cha Nigeria; kukusaidia kula lishe bora wakati wa ujauzito wako. Na iwapo hauna mimba na unajua mtu aliye mjamzito, tafadhali watumie makala haya wasome. Ratiba hii ya chakula cha ujauzito cha Nigeria ni ya kila mwanamke aliye na mimba.

food time tablefor pregnancy in nigeria

Here's our food time tablefor pregnancy in Nigeria

DAYS  MONDAY TUESDAY WEDNESDAY THURSDAY FRIDAY SATURDAY SUNDAY
BREAKFAST  Akamu and akara with milk Fried eggs and boiled ripe plantains Custard with bread and milk Boiled potatoes and egg sauce (no raw eggs) Tea and bread with moi moi  Chicken pepper soup with rice Akamu and bread
LUNCH Egusi soup with swallow (eba, fufu, semo, or any swallow of your choice) Vegetable soup with swallow Oha soup with swallow Afang soup with swallow of choice Efo riro with swallow or rice White soup and pounded yam Jollof rice and fried chicken
DINNER Beans pottage Moi-moi Boiled yam and stew Rice and goat meat pepper soup Beans and dodo Moi moi and tea Spaghetti and suya

Tafadhali fahamu: Unapaswa kufanya matunda sehemu kubwa ya lishe yako. Kula matunda angalau mara moja kila siku. Jibini laini na mayai mbichi yanapaswa kuepukwa kabisa pamoja na papai mbichi.

Utaratibu huu wa lishe na ratiba ya chakula cha ujauzito cha Nigeria itakusaidia kula lishe bora unapokuwa na mimba.

Hii ndiyo sababu kwa nini unahitaji ratiba hii ya chakula cha ujauzito cha Nigeria

food time table

Vyakula vina bei ghali Nigeria na huenda ukawa na shaka kuwa hutakuwa na uwezo wa kununua lishe yenye virutubosho tosha kwako na mwili wako. Habari njema ni kuwa hauhitaji kutumia pesa nyingi kupata virutubisho vifaavyo. Unahitaji kula aina tofauti ya vyakula kupata lishe bora.

Vidokezo vya kula kwa afya kwa lishe yako ya ujauzito
1. Usile chakula cha watu wawili

Katika ratiba hii ya chakula cha Nigeria cha ujauzito, tunakuhimiza kuepuka kula chakula cha watu wawili. Kwa sababu bila shaka utahisi njaa kwani una mimba, na ni rahisi kuanguka kwa mtego kwa kula zaidi.

Kulingana na makala haya yaliyo chapishwa kwenye kurasa ya Livestrong, kula chakula cha watu wawili huenda kukasababisha matatizo kama vil gestational diabetes, kiungulia na matatizo mengine, uzito mwingi wa mtoto wako na uzito mwingi kwa mama.

2. Angazia usafi wa mwili

Unahitaji kuosha matunda na mboga zako kwa makini ili kutoa uchafu wote, mchanga na viini. Wanawake wajawazito wasio chukua muda wako kuosha vyakula vyao vizuri wako katika hatari ya kupata toxoplasmosis.

Toxoplasmosis huenda ikasababisha kuharibika kwa moyo, macho, ubongo na hata mafua. Na cha zaidi ni kufanya mtoto aliye tumboni mwako kuathiriwa kupitia kwa placenta.

Pia, sio salama kula nyama na samaki ambayo haijapikika wakati wa ujauzito wako. Hakikisha kuwa mayai, nyama ya ng'ombe, kuku na vyakula vingine vimepikika vyema.

food time tablefor pregnancy in nigeria

3. Punguza sukari na vyakula vyenye ufuta mwingi

Kila mtu mara kwa mara ana jino tamu, ila unapaswa kuangalia viwango vyako vya sugari wakati wa ujauzito wako. Sukari imehusishwa na kuongeza uzito mwingi na kuharibika kwa meno. Pia, vyakula vyenye ufuta mwingi huenda vikaongeza cholestrol mbaya kwenye damu yako na mwishowe kusababisha ugonjwa wa moyo.

Ratiba ya chakula cha mimba cha Nigeria: Vidokezo vya afya vinaendelezwa.

4. Kula vyakula vya maziwa ukiwa na mimba

Maziwa, maziwa ya bururu na jibini ni muhimu katika ujauzito. Unapaswa kuhusisha vyakula visivyo na viwango vya juu vya maziwa katika ratiba yako ya chakula cha Nigeria cha ujauzito. Mtoto wako anahitaji kalisi na virutubisho vingine utakavyopata kutoka kwa maziwa na bidhaa zingine za maziwa.

5. Protini katika ujauzito

Nigeria ina vyakula vingi vilivyo na wingi wa protini. Unapaswa kula maharagwe, samaki, mayai, njugu, kuku, nyama ya ng'ombe na kadhalika. Unapaswa kula protini kila siku ukiwa katika ujauzito wako.

6. Kula matunda na mboga ukiwa na mimba

Matunda na mboga ni muhimu sana katika ratiba ya chakula cha Nigeria cha ujauzito. Matunda kama vile maembe, ndizi, mananasi, tikiti, na machungwa yana wingi wa vitamini na madini.

Kwa mboga, unaweza kula matawi ya ugu ama malenge, cucumbers, afang, matawi ya oha, matawi ya editan, mchicha, karoti. Mboga hizi zinasaidia kuchakata chakula na kuepuka kukosa maji tosha mwilini wakati wa ujauzito.

Kama tulivyo sema hapo awali, unahitaji kuosha matunda na mboga zako kwa makini ili kuepuka kupata maradhi na maambukizo.

7. Kula vyakua vyenye wanga wakati wa ujauzito wako

Kwa bahati nzuri, vyakula vya ndivyo vinaliwa zaidi katika Nigeria. Ni muhimu kuongeza wanga kwenye ratiba yako ya chakula cha Nigeria cha ujauzito kwa sababu vyakula hivi vitakufanya uhisi kushiba na kukupa nishati nyingi.

Unapaswa kula vyakula vya wanga kama fufu, eba, viazi, noodles, wali, mkate, mhogo, cocoyams na mtama.

Ni vyema zaidi kula wanga ambao hauja chakatwa, yenye maana ya kuwa unapaswa kununua vyakula freshi kutoka sokoni.

kumbukumbu: NHS

Livestrong

Healthline

WebMD

Soma pia: How to stop fibroids from growing during pregnancy

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio