Ratiba Ya Chakula Cha Wiki Moja Cha Familia Yako

Ratiba Ya Chakula Cha Wiki Moja Cha Familia Yako

Kwa bahati mbaya, teknolojia imeifanya kuwa vigumu kwa familia nyingi kula lishe zenye afya kwa pamoja wakati wote. Ratiba za kazini zina walazimisha wazazi wengi kula kiamsha kinywa kazini ama hotelini. Watoto kwa mara nyingi hula chamcha shuleni. Baadhi ya wakati, huenda wazazi waka kula chajio magarini mwao kwa sababu ya foleni ndefu za magari wanapo elekea nyumbani. Hii ndiyo sababu kwa nini tume tayarisha mwongozo wa ratiba ya chakula cha wiki moja ukuongoze, iwapo hauna wakati tosha wa kutengeneza ratiba yako.

ratiba ya chakula cha wiki moja

Tatizo lingine linali athiri tabia zetu za lishe ni kuwa familia nyingi zinapenda kula kitu kimoja. Watu wengi wanapenda kula wali, maharagwe ama ugali na sukuma wiki. Sio wengi wanao amua kuongeza hiari kama vile kunde, ama mboga za kienyeji kwenye lishe zao. Wengine wanapenda kula nyama kila siku ambako haku shauriwi kwani nyama huchukua muda mrefu kuchakatwa tumboni.

Kulingana na World Cancer Research Fund International, tabia hizi zisizo za afya vime husishwa na ongezeko la magonjwa ya muda mrefu na hata kusababisha vifo, kisukari, shinikizo la damu na magonjwa mengine.

Kwa familia nyingi zinazo fanya kazi, ni vigumu kula kiamsha kinywa, chamcha na chajio manyumbani mwao siku rasmi. Ila haku maanishi kuwa familia hizi haziwezi faida kutoka kwa ratiba ya lishe iliyo pangwa vizuri.

Angalia sampuli ama mfano huu wa ratiba ya chakula cha wiki moja

nigerian meals Time Table

Afrika ina lima vyakula vingi. Shamba zina mchanga mzuri wa kulima na sio rahisi kuathiriwa na janga za mazingara. Kujaribu kulima baadhi ya vyakula vinavyo fanya vyema upande unao ishi kunasaidia kuboresha lishe yako.

Katika makala haya, tuna angazia ratiba ya lishe ya wiki moja kwa familia inayo taka kula lishe yenye afya.

Kidokezo: Ni vyema kupika vyakula vyako mapema na kuvi weka kwenye friji viliwe unapo enda shuleni ama kazini. Kwa njia hii, una hakikisha kuwa familia yako ina lishwa vyema.

Bila shaka, ratiba hii sio lazima ifuatwe ilivyo. Kadri uwezavyo, unaweza badili vyakula tofauti kwa kutumia ratiba hii kama mwongozo wako.

Chochote unacho amua kufanya, hakikisha kuwa lishe zako zina aina tofauti za virutubisho. Huenda ukapata baadhi ya familia zina kula chakula chenye wanga mwingi bila kuhusisha matunda ama mboga. Ratiba hii kwenye orodha yako inapaswa kufanya iwe rahisi kwako kutengeneza lishe iliyo sawasishwa virutubisho.

Kula vyakula vyenye afya kuna husisha yafuatayo kwenye ratiba yako. Pia kuna husisha kula viwango vifaavyo vya mboga, matunda na kuhakikisha kuwa una kunywa viwango tosha vya maji kila siku.

Ratiba yetu ya chakula cha wiki moja inaendelea na vidokezo muhimu vya kula vya wanafamilia:

ratiba ya chakula cha wiki moja

 1. Kula matunda kwa wingi. Zoea kununua matunda nyumbani mwako. Waanzishie watoto wako matunda na uwahimize kula vyakula vyenye afya.
 2. Kunywa glasi moja ya maji punde tu baada ya kuamka kisha uendelee kuchukua kiamsha kinywa chako na bakuli ya matunda. Hata ukinywa maji na bakuli ya matunda, uko tayari kuanza siku yako. Hii itaku saidia kuanzisha mfumo wako wa kuchakata chakula.
 3. Kula lishe yako ya mwisho kabla ya saa moja za usiku. Ukihisi njaa usiku, kunywa chai ama kikombe cha chokleti na tunda.
 4. Kunywa maji dakika 30 kabla ya lishe yoyote ile.
 5. Iwapo lazima unywe vinywaji unapokula, kunywa maji badala ya pombe ama vileo vingine. Ni muhimu sana katika uchakataji wa chakula.
 6. Glasi yako ya maji sio lazima iwe baridi kama maji ya barafu. Wakati wote kunywa maji yaliyo na joto ya kawaida. 
 7. Pika chakula chako na kiasi kidogo cha mafuta.
 8. Fanya kila kitu kwa wastani. Kiwango kidogo sana cha chakula, matunda ama maji huenda kikakufanya ugonjeke.
 9. Zuia kunywa chai na kahawa lisaa limoja kabla ya kula.
 10. Kula ukiwa umekaa wima, usilale ukikula.
 11. Usile kwa mbio ama haraka. Chukua muda utafune kwa utaratibu ili kuharakisha uchakataji wa chakula.

Kumbukumbu: World Cancer Research Fund International 

Written by

Risper Nyakio