Ratiba Ya Chakula Ya Kutayarisha Kwa Muda Wa Wiki Moja

Ratiba Ya Chakula Ya Kutayarisha Kwa Muda Wa Wiki Moja

Kuwa na ratiba ya chakula cha kila siku itakusaidia kuhakikisha kuwa na uamuzi dhabiti kuhusu chakula utakacho tayarisha.

Ni mara nyingi ambapo huenda unafika nyumbani bila uamuzi dhabiti ya chakula utakacho kitayarisha usiku huo. Hasa unapokuwa na kazi inayo kukwaza, watoto, uhusiano na mambo mengine ambayo huenda yaka chukua muda wako mwingi. Ni wakati mgumu zaidi unapokuwa na watoto ambao lazima uwachukue kutoka shuleni, kuwasaidia kufanya kazi zao za ziada, kuwatayarishia mavazi ya siku ifuatayo na mambo mengineyo. Usipokuwa na ratiba ya chakula, huenda ikawa vigumu kufanya uamuzi wa chakula cha kutayarisha siku hiyo.

Ratiba Ya Chakula Ya Kutayarisha Kwa Muda Wa Wiki Moja

Tulipokuwa wachanga, mara kwa mara wazazi wetu walitu uliza kile ambacho tungependa kula na kingetayarishwa usiku huo. Kuwa na ratiba ya lishe kuna kupunguzia vikwazo vingi kwani unajua kabla, kile ambacho utakitayarisha.

Unapo tengeneza ratiba yako ya chakula, ni vyema kutia akilini kuwa unapaswa kula vyakula vyenye afya vitakavyo saidia mwili wako na kukupa virutubisho vifaavyo. Epuka kula vyakula vilivyo chakatwa kwani havisaidii mwili pakubwa. Lishe yako inapaswa kuwa na kiwango kikubwa cha mboga na matunda na kiwango kidogo cha wanga hasa wakati wa usiku.

Ili kukusaidia kuwa na wakati rahisi unapo tayarisha chakula chako, tume kutengenezea mfano wa ratiba ya chakula ambayo unaweza tumia kupanga chakula cha familia yako cha wiki moja.

ratiba ya vyakula vya kukata uzito

Siku Kiamsha Kinywa Chamcha Chajio
Jumatatu Mihogo kwa chai ya maziwa Pilau na mboga za kabichi Omena kwa ugali na chungwa
Jumanne Uji

na chungwa

Matoke kwa maini

na ndizi moja

wali kwa maharagwe ya nazi
Jumatano Nduma kwa Kahawa ama chai Chapati kwa nyama Githeri na sukuma

na parachichi

Alhamisi Chai kwa mayai Ugali kwa maini Mboga kwa baazi na tufaha moja
Ijumaa Viazi vitamu kwa chai Wali kwa kunde Biryani ya kuku
Jumamosi Mkate na mayai kwa maziwa nyama kwa ugali wali kwa mboga za kijani na ndizi moja
Jumapili Chai kwa mkate Matoke kwa nyama Chapati kwa nyama na kabichi

Una uhuru wa kubadilisha ratiba hii ikufae ama hata kutengeneza ratiba itakayo kupendeza. Angazia vidokezo tulivyo taja vya kutengeneza ratiba ya chakula. Hakikisha kuwa una kunywa maji tosha kila siku ili kurahisisha uchakataji wa chakula na pia kuwa na afya bora.

Kumbukumbu: Kenyayote

Soma pia: Ratiba Ya Vyakula Vitakavyo Kusaidia Kukata Uzito Wa Mwili

Written by

Risper Nyakio