Ratiba Ya Chanjo Kenya : Mwongozo Kwa Wazazi

Ratiba Ya Chanjo Kenya : Mwongozo Kwa Wazazi

Makala haya yana angazia mwongozo wa ratiba ya chanjo Kenya. Na pia kuelezea umri ambao watoto wanapaswa kupata kila chanjo.

Chanjo dhidi ya magonjwa huenda ikatazamiwa kuwa ya dharura zaidi ikilinganishwa na matibabu ya ugonjwa. Kuepuka ugonjwa ni bora kuliko kutibu, Chanjo sio muhimu tu kwa mtoto bali kwa jamii yote kwani ina epusha kusambaa kwa maambukizo. Magonjwa mengi huwa vigumu kusambaa kwa jamii. Kwa sababu ya chanjo, magonjwa kama vile polio na smallpox yameweza kuthibitiwa. Ratiba ya chanjo Kenya imekuwa ikiangaziwa kutoka mwaka wa 1980.

Bila shaka, chanjo ni njia ya kufanya mwili uwe na nguvu na uwezo wa kukumbana na magonjwa.

Ratiba ya Chanjo Kenya

Immunization Schedule In Kenya

Serikali ya Kenya imehusisha ratiba nyingi za chanjo, zinazo julikana kama Kenya Expanded Programme Immunization Schedule. Ambayo ime boreshwa kutoka kwa ratiba asili ya chanjo iliyo anzishwa mwaka wa 1980 Kenya. Ratiba asili haikuwa na baadhi ya magonjwa.

Hapa chini kuna ratiba kulingana na maradhi.

Chanjo ya BCG (Bacillus Calmette–Guérin 

Chanjo hii hupatia kinga dhidi ya tuberculosis na mtoto ana dungwa anapo zaliwa.

Chanjo ya Oral Polio (OPV)

Chanjo hii ina ina kumbana dhidi ya poliomyelitis (polio) mtoto anapo zaliwa, na nyingine katika wiki yake ya 6, 10 na 14. Polio inajulikana kuwalemaza watoto na kusababisha misuli dhaifu. Chanjo hii inapatiwa kwa kupitia kwa sindano, kwa mguu ama mkono. Dosi tatu za chanjo hii zinalinda mwili dhidi ya aina tatu za polio.

ratiba ya chanjo Kenya

DPT-HepB-Hib(Diphtheria, Pertussis, Tetanus, na Hepatitis B na Haemophilus influenza type b)

Ishara za Diphtheria  ni kama vile kuumwa na koo, kufura koo, joto jingi. Hii ni kwa sababu Corynebacterium diphtheriae inayo sababisha diphtheria ina athiri mfumo wa kamasi. Bordetella pertussis ndiyo bakteria inayo sababisha Pertussis,  ugonjwa wa mfumo wa kupumua unao sababisha kukohoa kwa nguvu na kufanya iwe vigumu kupumua. Clostridium tetani inasababisha Tetanus.  Bacteria hii ina athiri mfumo wa neva na kusababisha misuli kupunguka hadi kwenye shingo. Hatimaye, virusi vya Hepatitis B, vinasababisha Hepatitis B, inayo athiri mfumo wa neva.  Haemophilus influenza type b  huja na ishara kama vile pneumonia na meningitis kwa watoto walio na umri chini ya miaka 5. Ugonjwa huu unaweza sambazwa kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine kwa kupitia kwa kupumua.

Chanjo ya magonjwa haya inajulikana kama Pentavalent Vaccine, inayo patiwa mtoto akiwa katika wiki ya 6, 10, na 14.

Chanjo ya Pneumococcal (PCV 10)

Chanjo hii inapatiwa ili kuepuka maradhi ya sepsis, penumonia, na meningitis. Inapatiwa mtoto anapokuwa kwa wiki ya 6, 10 na 14.

Chanjo ya Measles 

Virusi vya measles husababisha measles ambayo ni maradhi yanayo weza kuambukizwa kwa urahisi. Chanjo hii inapeanwa katika miezi tisa kuepuka kusambaa kwa maradhi ya measles. Mgonjwa anaanza kupata ishara za macho yaliyo fura, joto jingi, na homa baada ya siku 10-12 za kuambukizwa.

Chanjo ya Yellow Fever 

Ishara za yellow fever huwa kama vile kutapika, uchungu kwenye misuli, joto jingi na kukosa hamu ya kula. Chanjo hii inapatiwa mtoto anapokuwa wa miezi tisa ila kuepuka kupata yellow fever.

ratiba ya chanjo Kenya

Chanjo yaTetanus (TT)

Ishara za tetenusi huanza na uchungu kwenye shingo, mgongo na taya. Inaweza athiri makalio, kifua, na misuli. Wamama wenye mimba na watoto wa umri wa miaka 7 hadi 14 wanapata chanjo ya tetenasi. Wakati wa umri wao mdogo, watoto wana tarajiwa kupata dosi tano na moja ya zaidi wanapokuwa wazima.

Vitamini A

Vitamini A huegemeza uwezo wa kuona, kinga mwilini, kujulikana, kujifungua, ukuaji na maendeleo. Vitamini hii inapatiwa mtoto akiwa na miezi 6, 12, 18, 24, 30, 36, 42, 48, 54 na miezi 60. Wamama walio jifungua chini ya miezi sita hupata chanjo hii pia.

Mahali pa kupata chanjo Kenya

Hospitali zote za umma nchini Kenya hupatiana chanjo, kwa kuongeza, pia baadhi ya hospitali za kibinafsi kuwa na huduma sawa.

Soma pia: See Nigeria's Current Immunization Schedule

Chanzo: Kenya Pharm Tech, WHO

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Lydia Ume kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio