Ratiba ya chanjo kwa mtoto mchanga katika nchi ya Kenya

Ratiba ya chanjo kwa mtoto mchanga katika nchi ya Kenya

Chanjo ni muhimu sana kwa mtoto mchanga. Mama anapaswa kufuata ratiba ya chanjo aliyopewa hospitalini kwa umakini zaidi. Ili kuhakikisha kuwa mtoto anakua ipasavyo bila ya kuadhiriwa na magonjwa.

Kujua ratiba ya chanjo kunamsaidia mzazi kujua wakati bora kumpeleka mtoto hospitalini. Chanjo zinasaidia mtoto kukua ipasavyo na kuepukana na magonjwa yanoweza kumuathiri. Ama kusababisha kifo chake katika umri mdogo. Kuna baadhi ya wazazi ambao hawaamini katika chanjo. Wana imani za kale, kuwa chanjo zitakuwa na athari hasi katika maisha ya mtoto, ambayo si kweli. Serikali ya nchi ya Kenya inafanya juhudi nyingi kuhakikisha, kuwa wamama wana wapeleka watoto wao wapewe chanjo katika vituo vya afya vilivyo karibu nawao. Ina wasiliana na wizara ya afya nchini ili kuwaelimisha wazazi kuhusu umuhimu wa chanjo na matukio yanayo kusudiwa iwapo watoto hawapati chanjo hizi wakati unaofaa. Pia wana wahimiza wamama kuhakikisha kuwa hawakosi chanjo hata moja.

Kanuni ya kimsingi ya chanjo ni kumpa mtu aliye na afya bora chanjo itakayo msaidia kuto pata maradhi tofauti. Kuna aina tofauti ya chanjo, huenda ikawa uhai iliyo wekwa wazi (measles, BCG, Rubella, OPV), iliyo uliwa ama hazifanyi kazi (IPV, Hib), Viumbe vidogo na iliyo safishwa sumu (tetanus). Chanjo nyingi zinaweza kuapeanwa wakati mmoja. Jambo hili ni muhimu kwani hujui wakati utakapo mwona mtoto yule mchanga tena. Chanjo za BCG, OPV, DPT-HeB-HiB na measles zinaweza pewa kwa mtoto kwa kufuatanishwa mtoto anapo fikisha umri unaofaa na kama hajapewa chanjo hapo awali. Mtoto anaye ugua kwa sana na anahitaji kulazwa hospitalini, anapaswa kupewa chanjo zinazo faa anapo pona.

Cha muhimu kukumbuka:

  • Chanjo zina haribiwa kwa urahisi na joto na zina kosa kufanya kazi
  • Zingatia kutupa sindano zilizo tumika kwa njia inayo faa. Usiziache mahali popote pale kwani mtoto wako anaweza kudungwa
  • Zingatia kuhifadhi chanjo mahali palipo na baridi, zingatia maagizo ya kuhifadhi inavyo paswa
  • Mwagize mama kumrudisha mtoto kwa chanjo inayo fuata tarahe iliyo andikwa kwa kijitabu chake
  • Mwagiza mama kuwa anabeba kijitabu cha chanjo anacho pewa wakati wote wanapo mpeleka mtoto hospitalini
  • Kuwaelimisha wazazi umuhimu wa kuwa peleka watoto wao wapewe chanjo. Joto kidogo ama kuugua hakupaswi kuwa zuia kuwa peleka watoto wao wapewe chanjo

Ratiba ya chanjo kwa mtoto mchanga katika nchi ya Kenya

Ushauri Kwa Wamama

Kifaduro: Ugonjwa unaoweza kuenezwa kwa watu.  Mtoto hukua na kikohozi kisicho isha, kutapika na inaweza sababisha kifo cha mtoto chini ya umri wa mwaka mmoja.

Diphtheria: Ugonjwa ulio rahisi kuambukiza, una enezwa kupitia matone. Dalili zake ni kama vile, matatizo ya kupumua, kumeza na shingo iliyo refuka.

Tetemusi: Husababishwa na vidonda vilivyo wazi. Dalili ni kama vile mtoto kushindwa kunyonya, kukauka, uchungu kwa misuli. Mama anapo pewa chanjo hii, inasaidia mtoto wake kuwa salama. Ugonjwa huu husababisha vifo vingi.

Poliomyelitis: Ugonjwa unao enzwa kupitia mawasiliano kama vile chembe za mate. Dalili zake ni kama vile kijoto, kutapika na kuhisi uchungu. Kwa wingi ugonjwa huu unaweza fanya mtoto kupooza viungo vya mwili ama kusababisha kifo chake.

Hepatitis B: Ugonjwa unaoenezwa kwa urahisi kwa wakati mwingi kupitia wazazi.  Unaenezwa kupitia kugusana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kupitia mate, vidonda vilivyo wazi, damu na sehemu za uke. Pia unaeza enezwa kupitia kwa watoto kwani wao ndo wanaugua zaidi. 

Chanjo mpya

Hizi ni baadhi ya chanjo mpya ambazo wauguzi wanapaswa kuwapa watoto wachanga na muda wanapo paswa kupewa chanjo hizi.

  • Mafua ya haemophilus {Haemophilus influenza type B conjugate Vaccine (Hib)}
  • Chanjo ya homa ya manjano ( Yellow Fever)
  • Recombinant DNA Hepatitis B vaccine (HepB)

Ratiba ya chanjo Kenya

Chanjo Umri Ushauri
BCG Polio (O PV O) Anapo zaliwa Punde tu mtoto anapo zaliwa
DPT-HeB-Hib Dose Polio(OPV 1) Wiki 6( miezi 1 ½) Mama anapo tembea hospitalini mara ya pili
DPT-HeB-Hib Dose POLIO (O PV 2) Wiki 10 ( miezi 2 ½ ) Wiki 4 baada ya chanjo ya DPT na O PV 1
DPT-HeB-Hib DOSE POLIO (O PV 3) Wiki 14 (miezi 3 ½ ) Wiki 4 baada ya chanjo ya DPT 2 na O PV 2
Measles Miezi 9 Kutoka miezi 6-9 iwapo mtoto analazwa hospitalini kwa magonjwa yoyote yale

 

Ni muhimu kwa wauguzi kuhakikisha kuwa mikono yao ni safi wanapo wapa watoto chanjo hizi ili kuhakikisha kuwa hawapati magonjwa zaidi. Pia chanjo hizi zina paswa kuwekwa baridi, kwani joto hufanya zipoteze nguvu zake kwa hivyo zina kosa kutimiza umuhimu wake. 

Read Also: What happens when you miss a vaccination?

Written by

Risper Nyakio