Likizo Ya Watoto: Jinsi Ya Kuhakikisha Kuwa Watoto Wako Wanaburudika Nyumbani

Likizo Ya Watoto: Jinsi Ya Kuhakikisha Kuwa Watoto Wako Wanaburudika Nyumbani

Likizo za shule ambazo kwa mara nyingi zinazo julikana kama likizo ndefu ziko nasi. Tuta fanya nini na watoto wetu wenye nishati nyingi kwa muda wa miezi miwili? Sio siri kuwa watoto wanapenda michezo na kuwa na kitu cha kufanya, hata kama huenda ikawa vigumu kuwa nao wakati wote. Na usaidizi wa baadhi ya wamama, tumetengeneza ratiba ya likizo kukusaidia kuhakikisha kuwa wewe na watoto wako mna jambo la kufanya.

Iwapo wewe ni mama unaye fanya kazi kutoka nyumbani ama mama wa kukaa nyumbani, kuna maana kuwa ratiba itabadilika, kwa hivyo ratiba ya wakati wa likizo itakusaidia sana. Unaweza ichapisha na kuiweka kwenye mlango wa nyumba, chumbani ama kwenye mlango wa friji.

Kutakuwa na siku ambapo ratiba hii haita fuatwa, na hiyo ni sawa.

Hapa kuna mifano ambayo unaweza fuata.

Tafadhali fahamu kuwa huu ni mwongozo tu na unaweza rekebisha wakati na mambo ambayo ungependa ili kupendeza watoto wako.

Ratiba ya likizo ya kuhakikisha watoto wako wana kitu cha kufanya

ratiba ya likizo ya watoto

 

Ili kuongeza kazi ambazo mtoto wako ameratibishwa kufanya na kutengeneza uzoefu wa kusoma, Tomilola Olatunde wa @thecuddleblog anashauri kuwa "Wamama wanaweza tumia siku moja kwa wiki kwenda za ziara uwanjani." Pia anashauri kuwa kugawanya wiki za likizo ziwe na mada. "Kwa mfano, unaweza kuwa na chakula, maua, usafirishaji, wanyama, familia ama wadudu kama mojawapo ya mada ambazo watoto wako wanaweza angazia.

Atinuke  Atilade kutoka @mumconfessions anawashauri wazazi kununua vitabu vingi na vidoli vya masomo. "Hata kama ni wakati wa kupumzika, ni muhimu kuhakikisha kuwa watoto wanasoma, na kusoma hakupaswi kuboeka kwani watoto husoma wanapo cheza." Pia alisisitiza haja ya kuhakikisha nyumba yako ina vitamu tamu. "Wana njaa zaidia wanapokuwa likizoni."

Tuna tumai kuwa tumeweza kukupatia mawazo tosha ya jinsi ya kuifurahia likizo na watoto wako nyumbani na iwapo una mawazo zaidi ungependa kutujulisha, tuwachie ujumbe hapa chini!

 

Pia unaweza penda kusoma makala haya: Things  To Do With Kids This Summer

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Syreeta Akinyede kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio