Kutengeneza ratiba mwafaka ya lishe nyumbani nchini Kenya

Kutengeneza ratiba mwafaka ya lishe nyumbani nchini Kenya

Kuwa na ratiba ya vyakula unavyo tengeneza kila siku nyumbani mwako ni muhimu sana. Inasaidia kupunguza mawazo mengi ya kutatiza unapo fika nyumbani na uchovu na hujui utakacho kutayarisha.

Ratiba ya lishe bora ni muhimu kwa kila familia. Mara nyingi unapo ishi peke yako, kuna uwezekano wa kushindwa utacho pika. Wakati mwingine unakosa hamu ya kupika kwani uko peke yako ama unajipata ukikula chakula sawa kila siku hadi unaboeka nacho. Pia kwa wanandoa, huenda mkawa na maoni tofauti kuhusu chakula mtakacho kipika kila siku. Kwa familia huenda ikawa mume na mke wana toka kazini wakati mmoja. Wanapo fika kwa nyumba, wote wamechoka na kila mmoja anataka kupumzika. Ni kawaida kwa mume kwenda kujipumzisha ila ana tarajia kuwa bibi yake atabaki na awatayarishie chakula. Unapata kuwa bwana ana mwuliza mkewe watakacho kula jioni siku hiyo. Anasahau kuwa wametoka kazini wote na kila mmoja alikuwa na mawazo ya kazini yaliyo jaa akilini mwake siku yote. Wanafaa kukaa chini na kujadiliana watakacho kula na pia amsaidie kutayarisha chakula hicho na wala si kumwachia kazi yote kwani wawili hao wamechoka.

Kuna vyakula vingi nchini Kenya ambazo wananchi wana vipenda. Kila aina ya chakula huwa na sehemu ya nchi inapotambulika zaidi. Kama vile githeri (maharagwe na mahindi) sehemu ya kati ya nchi. Wali na kuku sehemu ya magharibi mwa nchi. Maziwa ya ngamia, sehemu ya kaskazini mwa nchi. Sima na samaki sehemu ya Nyanza wanako vua samaki. Nazi na wali sehemu ya kusini mwa nchi, vyakula vya uswahilini ni vingi huku kama vile pilau na biryani vinavyo pendeza kwa kweli. Wananchi wa Kenya wana hamu nyingi ya chakula na wana penda kuvila vyakula vitamu vilivyo tengenezwa kwa umakini na ustadi. Sima kwa ugali na mayai pia ni chakula kinacho kuliwa katika sehemu zote za nchi. Ni rahisi kutayarisha na inachukua muda kidogo. Chakula hiki kina husishwa hasa na vijana ambao bado hawajapata jiko.

Baadhi ni vitu muhimu unavyo paswa kuzingatia unapo fikiria utakacho pika ama unapo tengeneza ratiba ya lishe bora nyumbani

Kutengeneza ratiba mwafaka ya lishe nyumbani nchini Kenya

Mboga za kijani:

zina virutubisho ambavyo ni muhimu kwa mwili. Pia ni muhimu sana kwa mama aliye na mimba na watoto. Zina saidia katika utengenezaji wa damu mwili, unapo kosa, huenda ukapata anaemia. Baadhi ya mboga hizi ni sukuma wiki, majani ya kunde, spinachi na kadhalika.

Protini:

Hakikisha kuwa chakula unachokila kina protini kama vile, nyama ya ng’ombe, nyama ya mbuzi, samaki, mayai, kuku, uyoga na kadhalika.

Matunda: 

Hakikisha kuwa chakula chako kina tunda angalau mara moja kwa siku. Matunda yana ongeza vitamini zinazo faa mwilini. Na kusaidia katika kutengeneza macho, ngozi, nywele na zinginezo. Baadhi ya matunda ambayo unaweza kula ni machungwa, papai, maembe, limau na mengineo.

Maji:

Hakikisha unakunywa angalau glasi moja ya maji baada ya kukila chakula chako.

Ni muhimu kuhakikisha kuwa mlo wako una viungo vyote vinavyo hitajika.  Ili mwili wako upate nafuu ikiwa una ugua ama pia mwili ukue jinsi inavyo faa na uwe na afya bora. Muhimu zaidi ni kuhakikisha kuwa kama kuna mama mja mzito anapata lishe bora, kwake na kwa mtoto aliye tumboni. Kwa wanao taka kupunguza uzito, ni muhimu pia kuangalia vyakula wanavyo kula. Waepuke kula nje na wajitengenezee nyumbani ili watayarishe vyakula vilivyo bora kwa mwili.

Ratiba ya lishe ni muhimu na inakupunguzia mawazo mengi ama kusumbuka kuhusu utakacho pika ukienda nyumbani usiku huo ama wakati wa mchana na kiamsha kinywa. Unaweza kutayarisha viungo vya chakula utakacho pika kabla ya giza kuingia. Pia unapo pata wageni, hauna hofu kuwa utashangaa utakacho watayarishia.  Baadhi ni ratiba ambazo unaweza tumia katika nyumba yako.

 

Siku ya wiki Kiamsha kinywa/ uporo Chamcha Chakula cha jioni
Juma tatu Yai, mkate (slici mbili),maji ya machungwa Wali, kipande cha kuku na mboga Sima kwa sukuma wiki
Juma nne Mkate na mboga, na chai/ kahawa Wali kwa mboga na vipande vya nyama ya ng’ombe Matoke kwa nyama ya mbuzi na tunda
Juma tano Oats na maziwa na tunda moja Viazi kwa kabeji na maharagwe/ kunde Viazi vitamu kwa kuku na mboga za kunde
Alhamisi Viazi vitamu na chai/kahawa Mukimo kwa supu ya mboga na chungwa Githeri na Viazi na sukuma wiki na avocado
Ijumaa Mikate ya sinia na chai na tunda moja Viazi vitamu na supu ya mboga Wali kwa nyama ya ng’ombe na kabeji
Juma mosi Maziwa na matunda Wali kwa maharagwe Sima kwa samaki
Juma pili Mkate na maji ya machungwa Nyama ya kuchomwa kwa sima Maharagwe ya nazi kwa chapati

Read Also: Smoothies For Toddlers: 3 Recipes Your Kids Will Love

Written by

Risper Nyakio