Lishe Ya Mama Mwenye Mimba: Ratiba Ya Lishe Ya Mama Mwenye Mimba

Lishe Ya Mama Mwenye Mimba: Ratiba Ya Lishe Ya Mama Mwenye Mimba

Vyakula hivi ni bora kwa mama aliye na mimba.

Lishe yenye afya ni muhimu kwa kila mtu, ila kwa mama mwenye mimba, mimba itahitaji lishe yenye afya kwa wote mama na mtoto. Chakula kingi cha kiafrika kina wingi wa virutubisho; kuna kitu cha kila ladha, hata kama ni wakati nyeti wa ujauzito wako. Hiyo ndiyo sababu kwa nini tumetayarisha ratiba ya lishe ya mama mwenye mimba; kukusaidia kuangazia lishe yenye afya unapokuwa na mimba. Na iwapo hauna mimba na unajua mtu aliye nayo, tafadhali wajulishe haya. Ratiba hii ya wanawake wenye mimba ni ya kila mama mwenye mimba Afrika kote.

food time table for pregnancy in nigeria

Hii ndiyo ratiba yetu ya lishe ya mama mwenye mimba

SIKU  JUMATATU JUMANNE JUMATANO ALHAMISI IJUMAA JUMAMOSI JUMAPILI
KIAMSHA KINYWA  Akamu na akara kwa maziwa Mayai yaliyo kaangwa na ndizi za kuchemsha Custard na mkate na maziwa Viazi vilivyo chemshwa na yai Chai na mkate na moi moi  Supu ya kuku wa pilipili na wali Akamu na mkate
CHAMCHA Supu ya egusi na (eba, fufu, semo, ama yoyote ile) Supu ya mboga na sima Supu ya Oha soup na swallow Supu ya Afang na wali wa swallow Efo riro na swallow ama wali SUpu nyeupe na mhogo Mchele wa jollof na kuku wa kukaanga
CHAJIO Maharagwe Moi-moi Mhogo wa kuchemsha na supu Wali na nyama ya mbuzi Maharagwe na chapati Moi moi na chai Spaghetti na suya

Tafadhali ng'amua: Unapaswa kuhakikisha kuwa matunda ni sehemu kubwa ya lishe yako. Kula tunda angalau moja kila siku. Epuka cheese na mayai mbichi na papai.

Ratiba hii ya lishe ya mama mwenye mimba itakusaidia kusawasisha lishe yako unapokuwa na mimba!

Hizi ndizo sababu kwa nini unahitaji ratiba hii ya lishe unapokuwa na mimba

ratiba ya lishe ya mama mwenye mimba

Vyakula huenda vikawa na bei ghali, na unaweza kuwa na wosia iwapo utaweza kununua lishe yenye afya yako na mtoto wako. Habari njema ni kuwa sio lazima utumie pesa nyingi kupata virutubisho vifaavyo. Unahitaji kula vitu kadha wa kadha kupata lishe bora na yenye afya.

Vidokezo vya kula lishe yenye afya ya ujauzito
1. Usile chakula cha watu wawili

Katika ratiba hii ya lishe ya mimba, tuna kuhimiza kuepuka kula chakula kingi kiwango cha watu wawili. Kwani utakuwa na njaa nyingi kwani una mimba, ni rahisi kuanguka kwa majaribio ya kula zaidi.

Kulingana na makala yaliyo chapishwa kwenye Livestrong, kula chakula cha watu wawili huenda kikaanza matatizo kama vile kisukari cha gestational ama kiungulia na kuto kuwa na starehe, uzito mwingi wa mtoto na kuongeza uzito mwingi wa mama.

2. Angazia usafi ufaao wa lishe

Unahitaji kuosha matunda na mboga vizuri ili kutoa uchafu, mchanga na viini. Wanawake wenye mimba wasio chukua muda kuosha vyakula vyao vizuri wako katika hatari ya kupata toxoplasmosis.

Toxoplasmosis huenda ikasababisha uharibifu wa moyo, macho, ubongo na hata mapafu. Na kilicho kibaya zaidi kuathiri mtoto aliye tumboni mwa mamake kwa kupitia kwa placenta.

Pia, sio salama kula vyakula ambavyo havija pikika vizuri hasa nyama na samaki unapokuwa na mimba. Hakikisha kuwa mayai, nyama ya ng'ombe, kuku na vyakula vingine vime iva vizuri.

ratiba ya lishe ya mama mwenye mimba

3. Tupilia mbali sukari na vyakula ambavyo vina mafuta nyingi

Kila mtu ana mara ambapo anataka kula vyakula vyenye sukari, ila lazima uchunge ulaji wako wa sukari unapokuwa mjamzito. Sukari ime husishwa na ongezeko la uzito na kuharibu meno. Pia, vyakula vyenye mafuta vinaweza ongeza cholesteroli mbaya kwenye damu yako na baadaye kusababisha maradhi ya moyo.

Maendelezo ya ratiba ya lishe ya mimba: Vidokezo vya afya.

4. Kula bidhaa za maziwa unapokuwa na mimba

Bidhaa kama vile maziwa, maziwa ya bururu na cheese ni muhimu sana unapokuwa mjamzito. Unafaa kuongeza bidhaa nyingi za maziwa zisizo na ufuta mwingi kwenye ratiba yako ya lishe unapokuwa na mimba. Mtoto wako anahitaji kalisi na virutubisho vingine ambavyo utapata kwenye maziwa na bidhaa za maziwa.

5. Protini katika ujauzito

Kuna vyakula vingi vilivyo jazwa na protini. Unapaswa kula maharagwe, samaki, mayai, njugu, kuku na nyama ya ng'ombe. Unapaswa kula protini kila siku unapokuwa na mimba.

6. Kula matunda na mboga kwa wingi unapokuwa mjamzito

Mboga na matunda ni muhimu sana katika ratiba yako ya lishe unapokuwa na mimba. Matunda kama vile maembe, mandizi, mananasi, na machungwa yana wingi wa vitamini na madini.

Kwa mboga, unaweza kula mboga za ugu ama malenge, cucumbers, afang, mboga za oha, matawi ya editan, karoti na kunde. Mboga hizi zitakusaidia kuchakata chakula na kuepuka kukosa maji mwilini unapokuwa na mimba.

Kama tulivyo taja hapo awali, unahitaji kuosha matunda na mboga zako vyema kuepuka maambukizi na maradhi.

7. Kula vyakula vya wanga unapokuwa na mimba

Kwa bahati nzuri, vyakula vyenye wanga ni maarufu zaidi hasa Afrika. Ni muhimu kuhusisha wanga kwenye ratiba yako ya chakula kwa sababu vyakula hivi vinakufanya uhisi umeshiba na kukupa nishati unayo hitaji.

Unapaswa kula wanga kama vile viazi, ugali, mahindi, wali, mihogo, na kadhalika.

Ni vyema kula vyakula vya wanga ambavyo havija chakatwa, yenye maana kuwa kununua vyakula hivi vikiwa freshi kutoka sokoni.

Kumbukumbu: NHS

Livestrong

Healthline

WebMD

Soma pia: How to stop fibroids from growing during pregnancy

Written by

Risper Nyakio