Ratiba Ya Vyakula Vitakavyo Kusaidia Kukata Uzito Wa Mwili

Ratiba Ya Vyakula Vitakavyo Kusaidia Kukata Uzito Wa Mwili

Ratiba hii ya vyakula vya kukata uzito wa mwili itakusaidia kutimiza lengo lako la kuwa na uzito wa mwili unao kupendeza. Na pia vyakula hivi ni rahisi kupata.

Hakuna jambo fiche kuhusu hesabu za kukata uzito wa mwili. Njia ya pekee ni kupoteza kalori unazo tia mwilini. Tafuta njia ya kupata usawa na utajipata ukikata uzito wa mwili kwa urahisi. Ila, chochote ufanyacho, haupaswi kujinyima chakula ili upoteze uzito. Ratiba ya vyakula vya kukata uzito wa mwili, ikizingatiwa na maisha hai, itakusaidia kupata usawa bora na wenye afya na kuhimiza kuwa na uzito unao faa wa mwili.

Zaidi, kwa lugha nyepesi, unatumia kalori 1600 hadi 2000 kila siku hata bila kufanya chochote. Na huu ni wakati ambapo haufanyi kazi nyingi. Nambari inaongezeka iwapo unafanya mambo tofauti kwa siku. Kwa hivyo, ili kupoteza uzito wa mwili, kwa njia yenye afya, unapaswa kuelewa jinsi unavyo paswa kufanya kazi na kuwa hai siku yote na wala sio kukaa ama kulala tu. Kisha utafute njia ya kutumia kalori zaidi ya za wastani kwa kila siku. Ila sio sana kwani mwili wako huenda ukaanza kuwa na upungufu wa kalori za kutimiza majukumu yako ya kila siku.

Nigerian food timetable for weight loss

Ratiba ya vyakula vya kukata uzito

Siku Kiamsha kinywa Cha mchana Cha jio
Juma pili 1 Ndizi ya kuchemsha 1 kipande cha samaki freshi na sugu ya mboga 2 vipande vya kuku wa kuchemsha, na 1 tufaha
Juma tatu 1 Yai la kuchemsha na 1 tufaha  Salad na kuku wa kukaanga ama kuchoma Supu ya samaki na 1 tufaha
Juma nne 2 Tufaha na maji mengi 1 kikombe cha maharagwe na maji Supu ya samaki wa pilipili na 1 tufaha
Juma tano  1 Yai la kuchemsha na kiazi kitamu 1 bakuli ya mboga za kijani Ndizi kwa nyama 
Alhamisi 1 cucumber na nyanya 2 Supu ya kuku wa pilipili Samaki wa kukaanga na supu ya mboga
Ijumaa 1 ndizi ya kuchemsha na 1 yai Supu ya nyama wa pilipili na 1 tufaha   Salad kwa samaki
Jumamosi Salad ya mboga Kuku na supu wa mboga Nyama ya ng'ombe na 1 tufaha

Ratiba hii ya kukata uzito sio ya wanawake walio na mimba, wanao nyonyesha ama watu wagonjwa. Iwapo uko miongoni mwao, tafadhali, ratiba hii si bora kwako.

Soma pia: 5 Things Not To Say To Your Spouse About Weight Loss

Chanzo: Naija Food Therapy

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Lydia Ume kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio