Kubishana katika ndoa na uhusiano ni kawaida. Lakini inaweza kuwa na afya inapofanyika kwa njia inayofaa, wanandoa wanahitaji kutia bidii kuzungumza na kutatua masuala yao. Unagundua wewe na mchumba wako mnapopigana kuhusu vitu sawa muda baada ya mwingine? Katika makala haya, tuna zungumzia masuala matatu makuu kwa nini wanandoa hupigana.
Sababu kwa nini wanandoa hupigana
- Pesa

Hili ni tatizo kubwa, hasa kwa ndoa ambapo mchumba mmoja ndiye aliye na kazi. Huenda akataka kuwapeleka watoto wake katika shule za bei ghali, wakati ambapo mchumba mwingine haoni haja, huenda akadhani kuwa bibi yake anatumia pesa nyingi kununua vyakula ama huenda bibi akamchukia bwana kwa kutokuwa na pesa za kutosha.
Wanandoa wanaweza kuepuka matatizo haya kwa kuzungumza kuhusu pesa zao na kuto ngoja hadi pesa zao zinapokuja kuzungumza kuhusu matatizo yao ya kifedha. Kuwa na bajeti pia na kuelewana ni muhimu.
2. Kazi za kinyumbani
Hili ni suala kubwa katika nyumba ambapo wazazi wote wanafanya kazi, na hata kwa mama wanaobaki nyumbani kuwalea watoto wao kwani wanazidiwa na kazi za kinyumbani, kuitunza nyumba na familia zao. Huenda wakabishana mara kwa mara na wachumba wao wanapohisi kuwa hawaegemezwi. Na kuwa hata suala kubwa wakati ambapo viwango vyenu vya usafi vinatofautiana. Mmoja huenda akawa na furaha, wakati ambapo mwingine anaona hakuja safika.
Kugawana kazi za kinyumbani ama kutafuta mfanya kazi kunaweza kusaidia kutatua suala hili. Kwa njia hii, kila mtu atafahamu anachotarajiwa kufanya.

3. Familia
Baadhi ya wanandoa hubishana kuhusu wanavyo wapatia watoto wao nidhamu. Wengine hubishana kuhusu wakwe zao. Haya yote ni kawaida- nyote ni watu tofauti wenye mitazamo tofauti kwa hivyo bila shaka mtakuwa na tofauti zenu.
Chochote kinachofanyika, fanya uwezavyo kutatua tatizo kama timu moja hasa inapofika kwa watoto wenu na familia zenu. Kuwa na majadiliano kwa kisiri na mchumba wako na myatatue masuala yenu bila kuathiri uhusiano wenu.
Soma Pia: Tendo La Ndoa Ni Bora Kwa Afya Na Uhusiano Wako: Kwa Njia Hizi