Sukari inayoongezwa inapatikana kwenye vyakula vingi hasa vilivyochakatwa. Sasa hivi, kiwango kikubwa cha watu kinakula chakula kingi kilichochakatwa. Vitamu tamu ambavyo watoto wanalishwa pia vina sukari ya kuongezwa. Je, unafahamu athari hasi za sukari? Sukari inahusishwa na aina nyingi za magonjwa ya kisasa. Tazama sababu kwa nini kula sukari nyingi kuna athari hasi kwa afya yako.
Athari hasi za sukari iliyoongezewa
- Kusababisha ongezeko la uzito

Idadi ya watu walio na uzito wa kupindukia wa mwili inaendelea kuongezeka kila uchao. Baadhi ya sababu kuu zinazosababisha jambo hii ni sukari nyingi. Vinywaji vilivyo na sukari nyingi kama vile soda na sharubati zilizochakatwa. Watu walio na uraibu wa kunywa vinywaji vyenye sukari nyingi wana uzito wa juu ikilinganishwa na watu wasiochukua vinywaji vyenye sukari. Soda inahusishwa na ongezeko la ufuta katika sehemu ya tumbo na ufuta huu husababisha matatizo ya kiafya kama vile ugonjwa wa moyo na kisukari.
2. Kupata chunusi kwenye uso

Lishe na vinywaji vyenye sukari iliyoongezewa vimehusishwa na nafasi ya juu ya kupata chunusi kwenye uso. Watu walio na uraibu wa kula vyakula vilivyo na sukari nyingi hasa vilivyo chakatwa pamoja na soda wana nafasi zaidi za kutatizika kutokana na chunusi kwenye uso.
3. Kuongeza nafasi zako za kuugua ugonjwa wa moyo

Lishe zenye sukari nyingi zinaongeza nafasi ya kuugua ugonjwa wa moyo. Sukari hasa ya kuongeza inayopatikana kwenye vinywaji kama soda inahusishwa na ongezeko la uzito wa mwili na shinikizo la damu, zote ambazo zinasababisha ugonjwa wa moyo. Kulingana na utafiti, watu wanaotumia vinywaji vyenye sukari nyingi wako katika asilimia 38 zaidi ya kupata ugonjwa wa moyo.
4. Kuongeza hatari ya kupata kisukari
Idadi ya watu wanaougua kutokana na kisukari imeongezeka mara dufu kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita. Hata kama kuna sababu nyingi zinazosababisha ugonjwa huu, sukari huchangia pakubwa.
Kunywa sukari nyingi pia kunaongeza hatari za kupata ugonjwa wa saratani, kuzeeka kwa kasi, ngozi kuzeeka na hata kusombwa kimawazo.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Jinsi Ya Kupunguza Uzito Wa Mwili Kwa Kutumia Lishe Ya Alkaline