Sababu ya chuchu kutoa maziwa huwa kumnyonyesha mtoto. Kunyonyesha ni hali ambapo mwanamke anatoa maziwa ya mama kupitia kwa chuchu zake kumlisha mtoto. Kwa wanawake waliojifungua hivi majuzi, kutoa maziwa ni kawaida. Vichocheo mwilini huashiria matiti ya mama kutoa maziwa ambayo ni chakula cha mtoto mchanga. Ila, mtu asiye na mimba wala mtoto mchanga anapotoa maziwa, hii siyo hali ya kawaida. Hali hii kwa Kisayansi inafahamika kama galactorrhea. Inasababishwa na mambo tofauti.
Sababu Ya Chuchu Kutoa Maziwa

Hali ya galactorrhea hata kama ni maarufu kwa wanawake, huenda ikawafanyikia wanaume pia. Ishara za hali hii ni kama vile:
- Kutoa maziwa kwa chuchu katika wakati usio wa kawaida
- Kichefuchefu
- Kupata chunusi usoni
- Tishu za maziwa kuwa kubwa
- Kukosa hamu ya kufanya mapenzi
- Ukuaji wa nywele usio wa kawaida
- Kutatizika kuona
- Kukosa hedhi ama vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida
Vyanzo vya chuchu kutoa maziwa
- Matatizo ya kiafya
- Kutumia aina fulani ya dawa
- Kuwa na uvimbe
- Kuchechemua matiti zaidi
- Matatizo ya kiafya
Matatizo ya kiafya kama kuwa na uvimbe, ugonjwa wa maini na figo, kusombwa na mawazo, uvimbe ama viwango vya juu ya kichocheo cha estrogen hasa katika watoto husababisha hali hii.
2. Matumizi ya dawa
Kutumia dawa za kulevya kama vile cocaina na marijuana kunawaweza chochea utoaji wa maziwa bila kuwa na mimba. Unapotembelea kituo cha afya kupata usaidizi kufuatia galactorrhea, mjulishe daktari kuwa unatumia dawa.
3. Kuchechemua matiti
Kuna baadhi ya watu ambao wanaweza pata hali ya galactorrhea kufuatia kuchechemua zaidi matiti. Kunaweza kuwa kupitia mavazi yasiyofaa, sindiria kubwa ama ndogo zaidi na kusababisha msuguano kati ya nguo na chuchu. Pia, kupitia kwa matendo ya kimapenzi.
Suluhu la chuchu kutoa maziwa

- Valia mavazi yanayokutosha. Epuka kuvalia mavazi yanayokubana zaidi
- Punguza kuchechemua matiti zaidi katika vitendo vya kimapenzi
- Kutumia dawa zinazosawasisha viwango vya homoni mwilini
- Kutotumia dawa za kulevya kama cocaine na marijuana
- Kufanyiwa upasuaji kutoa uvimbe kwenye matiti
Ikiwa utumizi wa dawa unahitaji, daktari atakushauri kuhusu dawa unazopaswa kuchukua ama kubadilisha. Epuka kununua dawa kwenye maduka ya dawa bila ushauri wa daktari mwenye vyeti.
Ikiwa huna mimba na wala hujajifungua hivi majuzi, ni muhimu kuwasiliana na daktari ili kufahamu sababu ya chuchu kutoa maziwa. Baada ya kufanyiwa vipimo, daktari ataweza kubaini chanzo cha hali ile. Pata matibabu mapema iwezekanavyo.
Soma Pia: Madhara Ya Tangawizi Kwa Afya Ya Mjamzito