Nini sababu ya chuchu kuuma? Kuna sababu nyingi zinazofanya chuchu za mwanamke kuuma. Mavazi kubana, maambukizi ya bakteria na kufanyiwa upasuaji ni baadhi ya vyanzo vikuu vya maumivu kwenye maziwa ya mama. Mwanamke anapopata matatizo yoyote na chuchu, ni kawaida kupata wasiwasi. Huenda akashangaa iwapo matiti kuuma ni ishara ya mimba, ama ana saratani. Katika makala haya, tunazungumza kuhusu matatizo tofauti ya chuchu na vyanzo vyake.
Sababu Ya Chuchu Kuuma

Aina ya mavazi. Kuna baadhi ya wanawake walio na ngozi nyeti, kuvalia mavazi yasiyo ya pamba huwapa mzio na kufanya wajikune mwili na chuchu kuuma. Iwapo mwanamke ana mzio wa aina fulani ya mavazi, ni muhimu kuvalia mavazi bora kwa ngozi yake. Mwanamke anapaswa kuwasiliana na mtaalum wa afya apate dawa ya kupaka kupunguza ama kutatua mzio. Ni muhimu kuhakikisha unafua mavazi mapya vyema kabla ya kuyavalia.
Mavazi yasiyofaa. Kuvalia mavazi yanayobana ama makubwa zaidi hufanya mwanamke akose starehe. Msuguano kati ya sindiria na chuchu za mwanamke kuna sababisha uvimbe ama kuhisi kujikuna kila mara na kufanya chuchu kuuma. Mwanamke anapaswa kufahamu saizi yake ya sindiria ili kuepuka kununua mavazi makubwa ama dogo kumliko. Pia, nunua sindiria kwenye duka hasa la sindiria na sio pahali pengine.

Mimba. Mwanamke anapopata mimba, kuna mabadiliko mengi mwilini. Mojawapo ya mabadiliko haya ni ongezeko la viwango vya vichocheo mwilini. Homoni ya mimba ama hCG humfanya mwanamke kujikuna chuchu. Anapokaribia kujifungua, chuchu huuma na kuanza kutoa maziwa. Ili kupunguza maumivu haya, mwanamke anastahili kuvalia sindiria inayomfaa. Kwa sababu wakati wa mimba maziwa huongezeka kwa saizi, hakikisha unanunua sindiria saizi moja kubwa. Pia, mjamzito anaweza kupatiwa dawa za kupunguza maumivu haya kwenye kituo cha afya.

Kunyonyesha. Mama anaponyonyesha, mara nyingi mtoto humvuta chuchu na kumfanya aumwe sana. Hasa siku za kwanza baada ya kujifungua. Mama aliyejifungua anaweza kupunguza huu kwa kupiga chuchu masi kutumia maji ya vuguvugu.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Vyakula 5 Vya Kuepuka Kwa Mama Mjamzito Ili Kudumisha Afya Katika Mimba