Ni kawaida kwa mtoto aliyekuwa analala usiku kucha kuanza kulemewa na usingizi ama kushtuka shtuka usiku. Hili ni jambo ambalo hutokea kwa watoto vile tu wanavyozidi kukua. Ila, nini huwa sababu ya mtoto kushtuka shtuka usiku na mzazi anafaa kuwa na wasiwasi?
Sababu Ya Mtoto Kushtuka Shtuka Usiku

Mtoto wako anapoamka kwa sababu ya kushtuka ni vyema kwenda kumwangalia ila tu usimwongeleshe .Iwapo atakuwa ameamka ataonekana kuchanganyikiwa na pia anaweza kataa kutulizwa. Haya huwa mambo ambayo mtoto hana kumbukumbu kuhusu. Pia iwapo bado amelala usijaribu kumwamsha ama anaweza fikiria unamvamia Kumbuka bado yuko usingizi.
Jambo la msingi ambalo husababisha kushtuka kwa mtoto huwa anapovuka kutoka kwa aina moja ya usingizi hadi nyingine. Kwa kawaida binadamu hupitia aina tofauti za usingizi. Kuna usingizi ulio mzito na mtu huwa hajihisi na kuna ule wa juu juu ambao mtu anaweza kuwa anasongesha mwili wake. Mtoto anapobadilisha kutoka kwa aina moja hadi nyingine ambalo hutokea kila wakati kwa usingizi atashtuka.
Sababu nyingine ni kuwa mdogo wako anaweza kuwa anaota. Ni wazi kuwa akili za mtoto wako zinazidi kupanuka na hivyo ata kwa usingizi bado mambo yanaendelea kupanuka. Iwapo atashtuka usiku unaweza enda na kumliwaza kwa upole ili arudi usingizini. Dakika chache za kufanya hivi zinafaa kusaidia. Kaa naye mpaka arudi usingizini.
Jambo lingine ambalo linaweza kusababisha kushtuka shtuka ni ugonjwa. Ndio, hakuna kitu ambacho huwasumbua watoto kama ugonjwa na mara nyingi wanapolala. Ni vyema kuhakikisha kuwa iwapo mdogo wako anahisi vibaya amepata uchunguzi na dawa. Kuhisi vibaya kutafanya mtoto kushtuka shtuka usiku. Angalia mambo kama maumivu ama pia joto la mwilini.

Sababu ya mtoto kushtuka shtuka usiku inaweza kuwa mtoto wako hapati usingizi wa kutosha. Najua hili linaweza changanya lakini ni ukweli kuwa iwapo mtoto wako hapati usingizi wa kutosha itakuwa vigumu kwake kupata ama kulala kwa mfululizo usiku kucha. Ni vyema kuwa na ratiba yake ya kulala wakati wa mchana na pia wakati wa usiku.
Kushtuka shtuka kwa mtoto wakati wa usingizi ni jambo linalowashtua wazazi wala sio jambo linalohitaji uchunguzi wa daktari. Ni vyema kuelewa sababu ya mtoto kushtuka shtuka usiku ili unamtuliza bila ya kumwamsha. Inaweza chukua muda kwa hizi kupotea lakini pindi utakapokuwa na utaratibu wa kulala ndivyo atarejea usingizi mwanana haraka.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Mama Anapaswa Kula Nini Anaponyonyesha Mtoto Mdogo?