Kwa Nini Una Harakisha Kufunga Ndoa?

Kwa Nini Una Harakisha Kufunga Ndoa?

Hakuna tetezi kuwa harusi zina pendeza na ndoa inaweza kuwa tamu na kufaulu. Tumeona watu wengi walio funga ndoa na kuishi maisha mazuri na wachumba wao. Kufanya harusi yenu ipendeze ni rahisi sana. Unacho hitajika kufanya ni kumtafuta mtaalum wa sherehe na kupanga matukio na hilo litakuwa lime tatuliwa. Walakini, kuwa na ndoa yenye fanaka ni suala tofauti na hauwezi mlipa mtu yeyote kufanya ndoa yenu iwe bora zaidi. Hii ndiyo sababu kwa nini sio vyema kuharakisha kufunga ndoa.

Sababu Za Kuharakisha Kufunga Ndoa

kuharakisha kufunga ndoa

Haijalishi muda mlio chumbiana kabla ya kuingia katika ndoa, lakini mara tu mnapo funga pingu za maisha, kuna jambo linalo badilika. Kwa watu walio na uhusiano mzuri kabla ya ndoa, huenda maisha yao hayatabadilika pakubwa, ila ni vigumu kuto ona mabadiliko haya.

Kwa ndoa ambazo bado wachumba wako pamoja hata kama mapenzi yameisha, huenda wakawa wanafanya hivi kwa sababu kama vile kuwepo kwa watoto ama kuto haribu picha ya 'ndoa isiyo na doa'.

Familia na Jamii

Katika jamii tunayo ishi, ndoa imepatiwa kipau mbele sana na nina uhakika kuwa hasa katika kipindi hiki cha krismasi, wazazi wengi wana wangoja watoto wao wawaletee wachumba wao. Huku wengine waki teta kuwa watoto wao wanaendeleza masomo na kutafuta kazi na bado hawana wachumba. Kuwashinikiza wawaletee wachumba wao kisha wapate watoto.

how to get married in nigeria legally

Marafiki

Marafiki sio tofauti na wavyele wetu. Baada ya marafiki wachache kufunga pingu za maisha, wataanza kukuuliza siku yako itakuwa lini. Hata kama mara nyingi wao hufanya hivi na nia njema, na wakati ambapo wengine watakufanya uone aibu kwa kuto kuwa umeoleka, wengine hawana njama ya kukuumiza.

Watu wengine pia wamejulikana kujiwekelea shinikizo binafsi ya kufunga ndoa. Halafu kuna mitandao, umri, wanafamilia ambao hawawezi maliza muda mrefu bila kukukumbusha kuwa hauna wakati mwingi ulio salia kupata mchumba na kisha watoto.

Vikundi hivi vyote vya shinikizo la kufunga ndoa havielewi kuwa kila mtu ana wakati wake maalum wa kufanya kitu. Na kinacho kutendekea ni tofauti na kitakacho tendekea mwingine. Malengo ya watu maishani pia ni tofauti. Wakati ambapo mmoja anataka kuanzisha familia, wengine wanataka kutimiza malengo yao kwanza.

Na kukimbilia ndoa bila uwezo wa kifedha, kiakili na kihisia kutafanya madhara zaidi kuliko faida. Hakikisha kuwa unaweza jitunza vyema kabla ya kukimbilia ndoa. Hakikisha kuwa shinikizo kutoka kwa watu wengine halitakufanya uingie kwa ndoa kabla ya kuwa tayari vyema.

Soma Pia: Koma Kuwaambia Wasichana Kuwa Ndoa Ni Tuzo Kwa Kuwa Na Tabia Nzuri

Written by

Risper Nyakio