Ishara Na Vyanzo Vya Kuharibika Kwa Mimba

Ishara Na Vyanzo Vya Kuharibika Kwa Mimba

Ni vyema mama aliye na mimba kuwa makini na vitu anavyo kula na kufanya anapo kuwa na mimba. Tuna angazia sababu za kuharibika kwa mimba. Soma zaidi ujue jinsi unavyo paswa kusalamisha mimba yako!

Kuharibika kwa mimba ni nini hasa?

Kuharibika kwa mimba ni pale ambapo mwanamke mwenye mimba anapoteza fetusi yake katika wiki za kwanza 20 za ujauzito. Huenda hali hii ikasababishwa na matatizo ya kiafya, na pia mtindo wa maisha unayo ishi pia huenda ukasababisha kuharibika kwa mimba.

sababu za kuharibika kwa mimba

Ishara za kuharibika kwa mimba

Kuna ishara nyingi ambazo zinaweza ashiria kuharibika kwa mimba. Hata kama ume angazia vitu vyote unavyo paswa ili kuepuka kupoteza mimba yako na uone ishara zifuatazo, hakikisha kuwa unamwona daktari ili adhibitishe iwapo umepoteza mimba.

1. Kuonekana

Kuonekana kwa kamasi la pinki kuna ashiia kuwa mwanamke ako karibu kushuhudia uchungu wa mama. Ukishuhudia hii kabla ya kufikisha wiki 20 za ujauzito, huenda ikawa ni ishara ya kupoteza mimba.

2. Kuumwa na tumbo

Sawa na uchungu wa mama, kuumwa na tumbo unapokuwa na kipindi chako cha hedhi huwa katika sehemu ya chini ya tumbo na mgongo na huenda ukadhani ni kuumwa na kiuno.

things to avoid during pregnancy that cause miscarriage

3. Kutokwa na damu

Kutokwa na damu kiasi ama kwa viwango vingi. Unapo anza kushuhudia kutoka damu inayo tiririka sana, unapaswa kumtembelea daktari wako ili ufanyiwe vipimo kudhibitisha iwapo ume poteza mimba.

4. Joto jingi na uchovu

Joto jingi pekee sio ishara ya kupoteza mimba, ila iki andamana na mojawapo ya ishara hizi, mwanamke anapaswa kuwa na shaka.

Vyanzo vya kuharibika kwa mimba

Hapa chini kuna sababu ambazo zinaweza sababisha kupoteza mimba. Hata kama vitu hivi haviwezi dhibitika na mwanamke mwenyewe, anaweza soma jinsi ya kukumbana nazo iwapo zina tokea.

sababu za kuharibika kwa mimba

Fibroids

Fibroids ni ukuaji usio wa kawaida kwenye uterasi ya mwanamke. Ikiwa fibroid iko katikati mwa uterasi ya mwanamke, kuna nafasi za juu kuwa mwanamke huyo anaweza shuhudia kupoteza mimba. Pia, saizi ya fibroid inaweza ika athiri ujauzito.

Iwapo una fibroids, unapaswa kumwona daktari wako unapo panga kupata mtoto. Fibroids huandamana na kipindi cha hedhi chenye uchungu na cha muda mrefu ikilinganishwa na vipindi vya kawaida na uchungu wa mgongo. Iwapo una shuhudia mojawapo ya ishara hizi, ni vyema kuwasiliana na daktari wako kabla ya kufanya uamuzi wa kupata mtoto.

Ni vyema kufahamu kuwa, baadhi ya wakati, fibroids hurithiwa kutoka kwa familia. Kwa hivyo iwapo una mwana familia aliye kuwa na ugonjwa huu, ni vyema kufanyiwa vipimo vifaavyo.

Maambukizi

Baadhi ya maambukizi kama toxoplasmosis, rubella, chlamydia huenda ikasababisha kupoteza mimba. Baadhi ya maambukizi haya huja na ishara na mengine hayana ishara. Ni vyema ukienda kufanyiwa vipimo mara kwa mara.

Joto jingi

Iwapo una ugua, ambako hutendeka miezi ya kwanza mitatu ya mimba na una joto jingi, tafadhali mwone daktari wako. Joto ya zaidi 38.90c huenda ika athiri mtoto wako.

Maradhi

Walio na magonjwa ya moyo, figo, maini, kisukari, uzito mwingi wa mwili na shinikizo la damu la juu na kadhalika, huenda waka athiriwa na kupoteza mimba. Iwapo una mojawapo ya magonjwa haya na una panga kupata mimba, hakikisha una fanyiwa vipimo mara kwa mara.

Ili kuhakikisha kuwa mtoto wako haathiriwi na hali yako.

Umri

Mwanamke aliye na miaka zaidi ya 35 ako katika hatari ya kupoteza mimba zaidi, hakikisha kuwa una mtaalum wa afya anaye kuangalia mara kwa mara.

Kupoteza mimba hapo awali

Mama aliye poteza mimba hapo awali ako katika hatari ya kupoteza mimba tena. Kwa sababu hii, anapaswa kuangaliwa kwa makini.

Vitu unavyo paswa kuepuka vinavyo sababisha kuharibika kwa mimba huenda vikahusisha mitindo ya maisha na chakula. Hapa kuna baadhi ya vitu ambavyo huenda vikasababisha kuharibika kwa mimba.

Kutumia mihadarati

Utumiaji wa madawa ya kulevya kama vile cocaine, marijuana na heroine huenda yaka sababisha kuharibika kwa mimba. Sio vyema kutumia dawa hizi unapo kuwa na mimba.

Kuvuta sigara

Kuvuta sigara huenda kukaharibu mimba. Uvutaji wa sigara katika trimesta ya kwanza huenda kukasababisha matatizo ya chromosomes na kupoteza mimba.

Chakula ambacho hakija iva

Chakula ambacho hakija iva hasa nyama huenda ikawa na bakteria ya listeria. Bakteria hii huenda ikasababisha kuharibika kwa mimba.

sababu za kuharibika kwa mimba

Vileo

Pombe ni mojawapo ya vitu vinavyo paswa kuepukwa kabisa unapokuwa na mimba ili kuepuka kuharibika kwa mimba.

Fikira nyingi

Wanawake wenye mimba wanapaswa kupumzika sana. Fikira nyingi ni mbaya kwa afya ya mama na mtoto anaye kua tumboni.

Kuto kuwa na nafasi tosha kati ya kuzaa watoto

Kuwacha wakati mwingi sana ama mdogo sana kutoka kwa kujifungua mtoto mmoja na mwingine huenda kukasababisha kuharibika kwa mimba. Nafasi ndogo sana kama vile miezi mitatu kutoka kwa kujifungua mara ya kwanza, mwili wa mama hautakuwa umepata mapumziko tosha kutoka kwa kujifungua kuliko pita. Mwili ume choka na huenda mama akapoteza mimba. Pia, mama anahitaji kupona kabisa baada ya kupoteza mimba kabla ya kujaribu kutunga mimba tena.

Kuchafuliwa kwa hewa na hali za mazingira zilizo chafuliwa

Kunusa hewa iliyo chafuliwa sana, kama nitrogen dioxide inayo tokana na kuchoma mbao ni mojawapo ya sababu za kuharibika kwa mimba. Hakikisha kuwa una ishi mahali ambapo kuna hewa tosha inayo ingia. Epuka mazingira ambayo sio safi ili usipate maambukizi.

Kumbukumbu: WebMD

Soma pia: What Causes Multiple Miscarriages: Tests, Risk Factors And Treatment

Written by

Risper Nyakio