Kipindi cha hedhi cha kila mwezi huwa ishara ya hadhi ya mwanamke. Mwanamke anapokosa kupata hedhi, ni kawaida kuwa na mawazo mengi. Na mara nyingi kushangaa iwapo ana tatizo la kiafya ama ana mimba. Kukosa hedhi na kuwa na vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida sio jambo geni kwa wanawake. Hata hivyo, ni vyema kuwasiliana na daktari wako unaposhuhudia jambo hili. Je, sababu za kukosa hedhi ni kama zipi?
Utaratibu wa kushuhudia hedhi

Kila mwezi, mwanamke hutoa ovari kutoka kwa mirija ya ovari. Mzunguko wa kawaida huwa kati ya siku 25 hadi 28. Yai linapokutana na mbegu za kiume, lina rutubishwa na fetusi kuumbwa. Yai la mwanamke lisipo kutana na manii, ukuta wa ndani ya uterasi huporomoka na mwanamke kupata hedhi. Mwanamke anapokosa kupata hedhi, ni ashirio kuwa huenda akawa na mimba ama matatizo mengine ya kiafya. Kukosa kupata hedhi kuna mweka mama katika hatari ya kutatizika kutunga mimba.
Kukosa hedhi mara nyingi husababishwa na kuvurugika kwa vichocheo mwilini. Njia ya kufahamu iwapo vichocheo mwilini vimevurugika ni kwa kuzingatia kuoa dalili hizi. Kuhisi uchungu mwingi unapokuwa na hedhi, kukosa kupata hedhi, kuchelewa kupata hedhi na kuwa na hedhi inayopitiliza wiki moja.
Sababu za kukosa hedhi
Baadhi ya sababu zinazomfanya mwanamke kukosa kupata vipindi vyake vya hedhi ni kama vile:
Kusongwa na mawazo
Unapokuwa na mawazo mengi, utendaji kazi wa kawaida mwilini hudhoofika, na kufanya kupevushwa kwa yai kuwa ngumu. Utoaji mdogo wa kichocheo cha estrogen hufanya iwe vigumu kupata hedhi.
Uzito mdogo wa mwili
Kuwa na uzito mdogo wa mwili huwafanya wanawake wakatatizika kupata vipindi vyao vya hedhi. Kwani uzalishaji wa homoni ya hedhi, estrogen, huwa duni na kufanya iwe vigumu kupata hedhi.
Lishe duni

Lishe isiyo na chakula kutoka vikundi vyote ikiwemo mboga, matunda na madini hufanya tezi za adrenal kufanya kazi nyingi kuliko inavyo stahili. Kichocheo kinachotolewa mwilini cha cortisol hufanya iwe vigumu kwa mwili kuzalisha homoni ya estrogen inayo husika na kusababisha hedhi kutendeka.
Mbinu za uzazi wa mpango
Kuna baadhi ya mbinu za kupanga uzazi zinazo mfanya mwanamke kutopata hedhi. Kumeza tembe za dharura baada ya kufanya ngono isiyo salama humfanya mwanamke kupata hedhi siku baada ya wakati anapotarajia. Mbinu za kupanga uzazi zinazokuwa na homoni huathiri hedhi ya mwanamke.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Sifa Za Hedhi Baada Ya Mimba Kutoka Ikilinganishwa Na Hedhi Ya Kawaida