Hizi Ni Sababu Kwa Nini Wanawake Hawa Hawataki Kupata Watoto

Hizi Ni Sababu Kwa Nini Wanawake Hawa Hawataki Kupata Watoto

Kuna watu wengi huko nje wasio taka kupata watoto na wana uwoga wa kusema kwa kuwa na hofu ya kusemwa vibaya.

Kwa watu wengi, kupata watoto ni hatua maishani. Ni jambo ambalo unapaswa kufanya. Kama kuolewa. Watu watakuuliza unapo panga kuolewa, na baada ya kuolewa, kila mtu anatarajia mtoto kufuata. Ni jambo la asili kabisa. Haijalishi iwapo wanandoa hao wana tatizika kujilisha. Haijalishi kuwa hawana nafasi tosha ya kulelea mtoto. Haijalishi iwapo hawana uwezo wa kihisia. Wana tarajiwa kupata mtoto haijalishi hali yao ya maisha, fedha ama hisia. Na kuto pata watoto kuna zua mijadala tofauti.

Kilicho kibaya zaidi katika upande huu wa dunia ni kuwa watu wachache sana hutayarisha kupata watoto jinsi wanavyo tayarisha sherehe ya harusi. Kupata mtoto kwa njia yoyote ile ni jambo asili hivi kwamba unapo sema kuwa huna mtoto unaangaliwa kwa shaka nyingi. Ni kiumbe cha aina gani kisicho taka mtoto? Kujibu hilo, mtu mwaminifu na mwenye mapenzi mengi. Chaguo la kuto taka watoto huja na kuhukumiwa kwingi. Watu hudhania kuwa unajaribu sana kuwa wa kipekee. Wengine wata kujulisha kuwa utabadili mtazamo wako kadri miaka inavyo songa. Wengine huenda waka kubandika jina, "anaye chukia watoto".

Kwa nini watu wana amua kuto pata watoto wao?

Hizi Ni Sababu Kwa Nini Wanawake Hawa Hawataki Kupata Watoto

Utafiti ulifanyika na professa wa saikolojia Leslie Ashburn-Nardo. Utafiti huo uli husisha watu walio zungumza kuhusu hisia zao na watu wa kubuni wasio na watoto ama wenye watoto wawili.

"Watu hupitia kejeli nyingi kutoka kwa jamii wanapo enda mrama na tabia inayo tarajiwa, 'kitu tunacho hitajika kufanya' kwa sababu ya tunacho ona kama kina faa," Ashburn-Nardo aliandika alicho gundua.

"Wazo la kupata watoto limeishi kunitia kiwewe kutoka miaka yangu ya ujana. Naona mambo yakienda mrama na kuto tosheleka. Kujua hivi, nili ishi kujiambia kuwa nilihitaji watoto. Kwa sababu wazo la kuto taka watoto halikuonekana kama kawaida. Ninge taja kwa kupuuza kwa familia kisha wangeuliza kwa nini. Ninge sema sababu zangu kwa kindani ndani. "Lakini katika miaka ya hivi karibuni, kusoma kuwa watu wengine hawataki watoto kwenye mtandao, sauti yangu imekuwa ikiongezeka niki taja sababu zangu.

Chini ya shinikizo linalo zidi la kuwapatia wazazi wajukuu, Shallon Lester alisema, "Nimeishi kuamini kuwa hakuna mtoto hata mmoja anaye paswa kuzaliwa ulimwenguni kama sehemu ya ajenda: sio kutatua ndoa, wala kulazimisha mtu kukua, na sio kutimiza matakwa ya nyanya."

kuto pata watoto

Wakati ambapo Laura Miller ali ashiria utu wake na kazi kama sababu zake za kuto taka kupata watoto. Aliandika, "Nakubali kwa uwazi kuwa sina watoto kwa sababu mimi ni mzembe sana na najipenda. Sina uwezo wa kulea. Sitaki kumchukua yeyote kutoka shuleni kila alfajiri ama kutafuta njia ya kulipa karo ya shule ama kuajiri mtu wa kunichungia watoto ili nitafute njia za kutazama sinema wiki fulani ijayo. Sitaki kuongelelea, kuangazia mahitaji ya, ama kukubali kitu kingine hadi pale ninapo taka." Sababu zangu sio mbali na za wanawake nilio soma kuhusu, sababu kuu ikiwa kuwa natatizika kujitunza mwenyewe na sina uvumilivu unao hitajika kulea mtoto.

Jambo la kukumbuka

Kuna watu wengi huko nje wasio taka kupata watoto na wana uwoga wa kusema kwa kuwa na hofu ya kusemwa vibaya. Popote ulipo, unapaswa kujua kuwa chaguo lako ni halali. Haijalishi sababu zako.

Soma piaOngezeka Nafasi Zako Za Kupata Mimba Kwa Kutumia Kalenda Ya Ovulation

Written by

Risper Nyakio