Wanawake Zaidi Wanachagua Kutoa Pata Watoto Na Jamii Haiwau Ungi Mkono

Wanawake Zaidi Wanachagua Kutoa Pata Watoto Na Jamii Haiwau Ungi Mkono

Ni wajibu wa kila mwanamke na mwanamme kuamua aina ya maisha ambayo angependa kuishi, kupata watoto ama kubaki bila watoto.

"Sitaki kupata watoto", ni mojawapo ya kauli zinazo wafanya watu wabaki wame bubuwaa. Kauli hii inafahamika kuanzisha ama kutamatisha mazungumzo. Huku watu wengi waki wakashifu wanao sema maneno haya, ama kutaka kujua zaidi kuhusu kilicho wafanya waamue hivi. Jamii ina hisia chanya kuhusu kauli hii hasa inapo toka kwa mwanamke. Kwani kwa muda mrefu, kupata watoto na kuwa mama imedhibitishwa kuwa mojawapo ya majukumu ya mwanamke. Na asipo pata mtoto ama bwana na familia, jamii inaanza kumkashifu.

Watu wata sikika wakimshauri mwanamke kuwa atabadili mawazo yake baada ya muda. Kulingana na wanawake walio amua kuto pata watoto, jambo la jamii kuto tenganisha kuwa mwanamke na kuwa mama ni kero kubwa. Kulingana na Shirika la Takwimu la Australia, katika mwongo ujao, idadi ya wanawake wasio na watoto itapiku nambari ya wanandoa walio na watoto. Kumaanisha kuwa wanawake zaidi wana fanya uamuzi wa kutopata watoto.

Kwa nini wanawake wana amua kutopata watoto

kutopata watoto

Mwanamke asiye taka kupata watoto haimaanishi kuwa hayuko tayari kusaidiana kulea mtoto na mwanamme ama kuwa mama wa kambo ama hata kuwasaidia marafiki wake kulea. Ila yeye mwenyewe hataki kujifungua kufuatia mambo tofauti kama vile ugumba ama hali zingine za kiafya.

Mbali na fedha, mwili wako kubadilika na kuwa, watoto ni jukumu kubwa, kuna wanawake wanao kerwa na viwango visivyo aminika vya kuwa mama. Sababu kama zinazo wafanya wanawake kubaki bila watoto ni kama vile:

  • Mambo kubadilika
  • Idadi kubwa ya watu duniani na mabadiliko ya hali ya anga
  • Kukosa hisia za kuwa mama
  • Afya
  • Na kutaka kuwa huru

Kuna imani kuwa una jipenda kwa sababu umeamua kuto pata watoto, kulingana na mwanamke mmoja aliye chapisha kitabu kuhusu uamuzi wake wa kutopata watoto.

Na kuna aina ya ukweli katika wazo hilo kwani unapo amua kupata watoto lazima uwapatie kila kitu. Lakini kama unapata watoto ili wakutunze unapo zeeka, huko ni kujipenda zaidi. Hakuna ushahidi kuegemeza kuwa watu hawajipendi wanapo kuwa wazazi.

Maisha lazima yabadilike unapo kuwa mzazi

kutopata watoto

Lazima utupilie mbali vitu na mitindo fulani ili upate na unapo pata watoto, maisha yako lazima yabadilike. Kwa watu wanao penda kusafiri sana, utalazimishwa kubaki mahali pamoja kwa muda ukiwatunza wanao ama unapo kuwa na mimba.

Bila watoto, wanandoa wanaweza fanya kazi zao kama ilivyo kawaida yao, kupata usingizi tosha usiku, kupumzika, kusafiri na kula vyakula vya aina yoyote.

Ni wajibu wa kila mwanamke na mwanamme kuamua aina ya maisha ambayo angependa kuishi, kupata watoto ama kubaki bila watoto. Bila kuhisi shinikizo na kutwikwa lawama kufuatia uamuzi wowote aliofanya.

Chanzo: WebMD

Soma Pia: Je, Unafahamu Mbinu Hatari Ya Ulezi Ya Sharenting?

Written by

Risper Nyakio