Kuvuja damu ni maarufu katika muhula wa kwanza wa mimba na sio chanzo cha kuwa na wasiwasi. Lakini kuvuja damu katika mimba huenda kukawa ishara ya hatari. Mwanamke mjamzito anapovuja damu anapaswa kutembelea kituo cha hospitali kufanyiwa vipimo. Kuna sababu nyingi za kuvuja damu katika mimba tunazoangazia.
Sababu Za Kuvuja Damu Katika Mimba

Damu ya implantation. Baadhi ya wanawake huvuja damu ya implantation yai linapojipandikiza kwenye kuta ya uterasi. Hufanyika siku ya 12 kutoka siku mwanamke anapojihusisha katika kitendo cha mapenzi. Iwapo mwanamke hayuko makini, huenda akadhani kuwa ni kipindi cha hedhi. Damu ya implantation ni nyepesi na haijazi pedi.
Kuharibika kwa mimba. Visa vingi vya kuharibika kwa mimba hufanyika katika muhula wa kwanza wa mimba. Kuvuja damu nyingi katika trimesta ya kwanza ya ujauzito huashiria kuharibika kwa mimba. Hat hivyo, kuna visa ambapo sio ishara ya kupoteza mimba. Unapogundua kuwa unavuja damu, ni muhimu kufanyiwa vipimo kutoa wasiwasi wa kushuhudia kuharibika kwa mimba.
Mabadiliko ya mlango wa uke. Katika safari ya mimba, damu zaidi hupita kwenye mlango wa kizazi. Kujihusisha katika kitendo cha uzazi huenda kikamfanya mwanamke atokwe na damu, katika kisa hiki, sio chanzo cha wasiwasi kwa mama.

Maambukizi. Mwanamke mjamzito anapopata maambukizi ya kingono kama vile kisonono, humfanya atokwe na damu.
Uchungu wa uzazi usiokomaa. Kuvuja damu baadaye katika safari ya mimba huenda kukawa ishara kuwa mwanamke ako tayari kujifungua. Siku chache ama wiki kabla ya uchungu wa uzazi kuanza, kamasi linalofunika mlango wa uterasi hutoka kupitia kwa uke na mara nyingi huwa na kiasi cha damu. Unapoanza kuvuja damu katika wiki ya 37 ya ujauzito, ni muhimu kuwasiliana na daktari wako.
Kuna sababu nyingi za kuvuja damu katika mimba, nyingi ya kipekee ya kuhakikisha kuwa mwanamke ako salama hata baada ya kutokwa na damu katika ujauzito ni kufanyiwa vipimo na kufanyiwa ultrasound.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Ishara Na Mabadiliko Yanayofanyika Mwilini Katika Mimba Ya Miezi Mitatu Mapacha