Sababu Kwanini Unashuhudia Maumivu Ya Kichwa Asubuhi

Sababu Kwanini Unashuhudia Maumivu Ya Kichwa Asubuhi

Ushawahi shangaa kwanini unaamka huku ukihisi maumivu ya kichwa, hata wakati ambapo hauko mgonjwa? Sababu za maumivu ya kichwa asubuhi mara kwa mara ni nyingi. Kuanzia siku na hisia njema kutakupatia nishati inayofaa siku yote, ila maumivu ya kichwa asubuhi huenda yakakuharibia siku yako. Maumivu ya kichwa asubuhi sio ya kushangaza kwa njia yoyote ile. Iwapo umekuwa ukishuhudia maumivu haya, hauko peke yako. Kuna watu wengi wanao shuhudia maumivu haya.

 

causes of frequent morning headaches
Mama akishuhudia maumivu ya kichwa [ece-auto-gen] 

Maumivu haya ya kichwa hutendeka kufuatia baadhi ya mabadiliko ya kifizikia mwilini mwako. Maumivu yako ya kichwa asubuhi huenda yakawa sio kawaida, ila, utawezaje kukabiliana na jambo hili iwapo hujui kisa na sababu ya maumivu haya.

Makala haya yatakuonyesha sababu kwanini unashuhudia maumivu ya kichwa asubuhi.

1. Kukosa usingizi

causes of morning headaches

[Fab Magazine]

Unapo kosa kulala vyema usiku, maumivu ya kichwa hayawezi epukika. Utafiti umethibitisha kuwa matatizo ya kulala kama vile kukosa kulala ni mojawapo ya sababu kuu za maumivu ya kichwa asubuhi. Iwapo unatatizika kulala karibu kila siku, utashuhudia maumivu ya kichwa mara kwa mara. Pata matibabu yafaayo ya kukosa usingizi na utaweza kulala vyema.

2. Kutumia mto usiofaa

headaches

[ece-auto-gen]

Kitu rahisi kama vile kutumia mto usiofaa huenda kukawa chanzo kikuu cha maumivu ya kichwa asubuhi. Wakati ambapo misuli ya ngozi ya shingo imekazwa kwa nafasi moja kwa muda mrefu, huenda ukashuhudia maumivu ya kichwa. Njia bora ya kukabiliana na jambo hili ni kutafuta mto unao shikilia shingo yako kwa nafasi iliyo sawa kuepuka maumivu ya kichwa.

3.  Usingizi uliotatizika

causes of frequent morning headaches

Sleep apnea is a serious condition that causes people to stop breathing in their sleep [ece-auto-gen]

Hii ni hali mahututi ambayo hufanya watu kuwacha kupumua katika usingizi wao mara baada ya nyingine. Utafiti umethibitisha kuwa maumivu ya kichwa asubuhi katika kesi hii, ni kufuatia kukosa hewa na ongezeko la shinikizo ambalo huenda likatokea kichwani mwako kufuatia hali hii.

Watu ambao hutoa sauti wanapolala huwa na hali hii na ni njia ya kipekee ya kujua ni iwapo mtu atakuangalia unapolala. Iwapo una hali hii, unahitajika kumtembelea daktari wako.

Makala haya yalichapishwa mara ya kwanza na Pulse. NG kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio