Sababu Zingine Zinazo Mfanya Mwanamke Kupanga Uzazi

Sababu Zingine Zinazo Mfanya Mwanamke Kupanga Uzazi

Kuchukua tembe za kupanga uzazi hakusaidia kudhibiti mimba tu kwa mwanamke, mbali ni muhimu katika kutatua matatizo ya ngozi yanayo sababishwa na homoni.

Kuna visa ambavyo vinaweza mfanya mwanamke kutumia vidhibiti uzazi mbali na kujikinga dhidi ya kupata mimba. Mbinu za kupanga uzazi kama vile tembe huwa na homoni ya estrogen ama progesterone na zingine huwa zimechanganywa. Zinaweza saidia kutatua matatizo yanayo husika ama kusababishwa na homoni. Usiwe na shaka kutumia vidhibiti uzazi ama kupanga uzazi kuponya matatizo haya kwani utafiti unaegemeza faida zake katika kufanya hivi. Fahamu sababu zaidi za kupanga uzazi

Sababu zaidi za kupanga uzazi

sababu zaidi za kupanga uzazi

1.Mhemko wa hisia katika hedhi

Unapokuwa na kipindi chako cha hedhi, utagundua kuwa hisia zako zina badilika kwa kasi, kukasirika, kusinyika ama kuwa na mawazo mengi. Kwa kimombo kuna fahamika kama PMS (premenstrual syndrome). Huenda ukashauriwa kutotumia tembe za sukari na zinazo kuwa pamoja na tembe za kupanga uzazi. Kuchukua tembe hizi zenye homoni kuta athiri vipindi vyako vya hedhi na mabadiliko hayo kuathiri mhemko wako.

2. Kuumwa na kichwa

Kuna vyanzo vingi vya kuumwa na kichwa, lakini mabadiliko ya homoni mwilini yanaweza ongeza maumivu yako. Unaweza umwa na kichwa kabla na unapokuwa na vipindi vyako vya hedhi, kufuatia kupunguka kwa kiwango cha estrogen mwilini. Unaweza shauriwa kuendelea kuchukua tembe za kupanga uzazi ili kusawasisha viwango vya homoni mwilini.

3. Kuumwa na tumbo wakati wa hedhi

Baadhi ya mbinu za kupanga uzazi huzuia kupevuka kwa yai mwilini. Yai lisipo achiliwa kutoka kwa mirija ya uzazi, hauta hisi kuumwa.

4. Upele usoni (acne)

postpartum acne

Kuwa na upele usoni ni tatizo linalo wasumbua wanadada wengi. Kuchukua tembe za kupanga uzazi kutasaidia kupunguza idadi ya upele usoni. Fahamu kuwa hii sio dawa ama matibabu ya upele usoni. Wasiliana na daktari wako kuona tembe zitakazo ufaa mwili wako zaidi.

5. Vipindi vya hedhi vizito na visivyo vya kawaida

Mwili wako usipo kuwa na viwango tosha vya progesterone, unaweza kaa muda mrefu kabla ya kupata hedhi. Kuta za uterasi zita unga sana na unapo pata hedhi yako, utatoa damu nyingi ama kuwa na hedhi nzito. Sababu zaidi za kuchukua tembe za kupanga uzazi zilizo changanywa ni kuwa, zita sawasisha hedhi yako.

6. Kutatua PCOS

Huwezi ponya PCOS (polycystic ovary syndrome), lakini unaweza tibu ishara zake kama vile kukosa kipindi cha hedhi, upele usoni, kukua nywele nyingi. Homoni zilizoko kwenye tembe za kupanga uzazi zinaweza saidia kusawasisha homoni za kike na kiume zinazo sababisha tatizo hili katika wanawake.

Kwa sababu tembe za kupanga uzazi zina dhibiti kiwango cha damu wakati wa hedhi yako, una nafasi changa za kuugua kutokana na kukosa damu tosha mwilini ama kuwa na seli nyekundu chache mwilini.

Soma PiaKutunga Mimba Baada Ya Kutumia Mbinu Za Kudhibiti Uzalishaji

Written by

Risper Nyakio