Sabrina Elba ako Kenya!
Sabrina ambaye ni mke wake Idris Elba mwigizaji mashuhuri anayejulikana kwa sinema kama The Wire, Luther na Nelson Mandela.
Picha: Sabrina Elba Instagram
Kwenye kurasa yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram, Bi. Elba aliandika kuwa ana furaha kuwa Kenya. Kama balozi wa UN wa IFAD, anatembelea miradi ambayo shirika hili limewekeza. Alipatana na wanaume na wanawake wanaojitahidi kila siku kukuza chakula kinachowalisha wananchi. Hata hivyo, wakaazi wa eneo la Embu ni baadhi ya watu walioathiriwa zaidi na athari za mabadiliko ya hali ya hewa. Alisikiliza hadithi kuhusu changamoto zao, matumaini na kujitahidi walizomwelezea.
Picha: Sabrina Elba Instagram
Familia ya Sabrina Elba
Sabrina Dhowre Elba ni mtoto wake Marya Megal ambaye ni mzaliwa wa Somalia. Mnamo Aprili tarehe 25 mwaka wa 2020, Sabrina Elba aliteuliwa kuwa balozi wa UN wa IFAD. Lengo likiwa kuwawezesha wanawake na wasichana vitongojini.
Marya alipokuwa miaka 16, alitoka nchini Somalia na kuenda Canada kuanza maisha upya. Dhidi ya kuenda nchi geni, Marya alifanya juu chini kuhakikisha kuwa watoto wake wanafahamu lugha yao ya mama, kisomali, wanazifahamu tamaduni zao na njia ya maisha ya watu wa Somalia.
Kila alipoweza, alihakikisha kuwa amewapeleka kuzuru Somalia. Jambo ambalo Sabrina alisema ni muhimu wa utambulisho wake. Kuzuru Somalia kulimfanya akaipenda nchi ile, ngamia za huko, joto ya jua na watu wa Somalia.
Kulingana na Sabrina, mamake alimfunza umuhimu wa maendeleo ya kilimo, hasa unapotegemea shamba kuishi. Anafahamu jinsi kisima na umwagiliaji maji unaweza kubadilisha maisha. Na kuwa pia alifahamu jinsi wanawake kutoka bara la Afrika wanahangaika. Sabrina aliandika kwenye kurasa yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram.
Kujumuika na IFAD
Picha: Sabrina Elba Instagram
Marya ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kuwajuza Sabrina na Idris Elba kuhusu shirika kubwa linalo wasaidia watu masikini vijijini na kuwa ingekuwa bora kwao kuhusika.
Sabrina alitaja kuwa kuna bilioni 1.7 ya wanawake na wasichana vijijini waliohitaji matumaini. Aliapa kuwatumikia heshima, bidii, na kwa kujitolea. Kisha kumshukuru mamake kwa kumtia msukumo wakati wote na kutumaini kuwa angemfanya aone fahari.
Picha: Sabrina Elba Instagram
Sabrina Elba ako Kenya ambapo anapatana na wakulima wa nchi na pia kuweza kuona jinsi michakato ya UN kwa IFAD inavyowasaidia wanawake na wasichana masikini huko vijijini.
Chanzo: Africaparent
Soma Pia:Rihanna Atangaza Kuwasilisha Bidhaa za Fentybeauty na Fentyskin Africa