Sabuni Salama Ya Kunawa Uso Unapo Kuwa Na Mimba

Sabuni Salama Ya Kunawa Uso Unapo Kuwa Na Mimba

Ni vyema kwa mama mwenye mimba kuwa makini sana na sabuni ya kunawa uso anayo yatumia. Sio vyema kutupilia mbali utaratibu ambao ulikuwa unafuata kabla ya kuwa na mimba. Ila, wakati huu unapaswa kuwa makini kwani ngozi yako ni laini na huenda ikawa na matatizo mengi. Kama vile acne, melasma ama ngozi iliyo kauka. Kuna bidhaa nyingi ambazo unaweza tumia, ila unapaswa kuhakikisha kuwa bidhaa hizi hazina athari hasi kwa afya yako na ile ya mwanao.

Unapaswa kutumia nini kunawa uso unapokuwa na mimba?

Unapaswa kutumia bidhaa zilizo kubaliwa kuuzwa madukani na shirika la afya kutoa shida zozote ulizo nazo za ngozi. Unapaswa kuwa makini sana. Usitumie bidhaa zozote. Mama mwenye mimba ana shauriwa kutengeneza orodha ya bidhaa za kunawa uso ambazo angependa kutumia na kuwasiliana na daktari wake kujua iwapo zitakuwa salama kwa ngozi yake, afya yake na ile ya mtoto wake. Utaratibu mzuri wa ngozi na uso unapokuwa mjamzito ni muhimu sana kwa mama ili kumsaidia kuwa na ngozi inayo ng'aa.

Sabuni salama za kutumia kwa mama mjamzito kusafisha uso

Unapo chagua sabuni za kutumia kunawa uso unapokuwa mjamzito, ni vyema kuchagua sabuni zilizo tengenezwa na vitu asili. Soma kijisanduku cha kila sabuni kwa makini kuhakikisha kuwa sabuni hiyo haina bidhaa za sumu ndani yake. Kwani bidhaa kama hizo huenda zika athiri maisha ya mtoto wako kupitia kwa ngozi na kisha kuingia kwa damu.

Iwapo una shaka zozote kuhusu sabuni unayo tumia kunawa uso, wasiliana na daktari wako atakaye kushauri kuhusu sabuni iliyo salama zaidi kwako. Hakikisha kuwa unaepuka kutumia bidhaa zilizo na retinoids na hydroxyl acids kwani huenda zika sababisha matatizo ya mimba na unapo jifungua.

Orodha ya sabuni ya kunawa uso yaliyo salama kwa afya yako

Unaweza pata mafuta haya popote pale ulipo. Baadhi ya ainai hizi ni maarufu sana kwani zinaisaidia ngozi yako kung'aa na kuwa laini. Unaweza zipata kwenye duka kubwa.

Ajali Black Soap and Tea Tree Organic Face Soap

face wash during pregnancy

Hii ni bidhaa bora kwa kila mama mwenye mimba. Ajali ni bidhaa ya kunawa uso inayo sifika ya kunawa uso na kukusaidia kung'aa unapokuwa na mimba. Bidhaa hii imetengenezwa na vitu asili na haina athari hasi kwa ngozi yako. Inatoa acne ya ngozi na kuisaidia ngozi yako kung'aa na kuwa laini zaidi. Iwapo unashangaa bidhaa ya kutumia kusafisha uso wako, usitafute tena kwani suluhu ndiyo hii.

Olay Foaming Face Wash

face wash during pregnancy

Mafuta haya kutoka Olay, yana paswa kuwa kwa orodha yako ya mafuta salama ya kunawa uso ukiwa na mimba. Ili ngozi yako iwe laini, bidhaa ya kunawa uso ya Olay yanapaswa kuwa kwa utaratibu wako wa kila siku wa kusafisha uso wako. Iwapo una shida ya ngozi kukauka kufuatia ujauzito, ama melasma, hakikisha kuwa unatumia mafuta haya.

Mafuta ya kunawa uso ukiwa na mimba: Mint Organic Care Liquid Wash

mafuta ya kunawa uso

Kumwaga kiwango kidogo cha mafuta haya ya uso na mwili unapo oga kutaiwacha ngozi yako ikiwa laini. Ina patikana kwa aina tofauti katika apricot, bergamot na chai nyeupe, machungwa na oatmeal. Wanawake wenye mimba wanashauriwa kutumia mafuta haya.

Matte Apothecary Liquid Black Soap

List of safe face washes during pregnancy

Sabuni hii ni laini kwa ngozi yako na ina virutubisho muhimu vinavyo isaidia ngozi yako kuwa na unyevu na kuwa safi wakati wote. Ni sabuni bora kutatua hali ya ngozi kukauka hasa unapokuwa na mimba. Inasaidia kutoa seli zilizo kufa na kuimarisha ngozi yako. Ili kupata matokeo bora zaidi, unapaswa kupaka sabuni kwa ngozi yako punde tu baada ya kuoga ngozi yako ikiwa na maji, na uiwache kwa dakika moja. Sabuni hii nyeusi ya Matte Apothecary ina asali, sharubati ya aloe vera, mafuta ya grape seed, shea butter, jojoa oil, mafuta ya palm kernel na mafuta mengineyo yanayo isaidia ngozi.

Adunni Green Tea Face Soap

mafuta ya kunawa uso

Sabuni hii ya uso ya green tea ina moringa, matcha green tea na rosemary. Vitu hivi vina linda na kuirutubisha ngozi laini ya uso wako unapokuwa na mimba. Unaweza tatua hali ya ngozi kukauka na upele wa mimba kwa kutumia sabuni hii na hii ndiyo sababu kwanini sabuni hii inapaswa kuwa katika orodha yako ya sabuni za uso ukiwa na mimba.

Una vitu zaidi unavyo tumia? Tujulishe kwa kuwacha ujumbe mfupi hapa!

Soma pia: Bidhaa Bora Za Kunawa Uso Ukiwa Na Mimba

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio