Hakikisha Kuwa Sahani Ya Mlo Ya Mama Mwenye Mimba Ina Chakula Hiki!

Hakikisha Kuwa Sahani Ya Mlo Ya Mama Mwenye Mimba Ina Chakula Hiki!

Maarufu kama kibohidrati ni muhimu sana katika kuupa mwili nguvu. Hakikisha kuwa unakula chakula kutoka kwa nafaka zisizo kobolewa

Tunapo zungumza kuhusu lishe katika mimba, ni vyema kwa mama mjamzito kujua jinsi sahani ya mlo ya mama mjamzito inavyo paswa kuwa. Na kiwango kinacho shauriwa cha kila aina ya chakula kutoka kwa jamii tofauti. Sahani ya mlo kulingana na wataalum wa lishe kutoka Chuo Kikuu cha Afya ya Jamii, sahani inapaswa kuwa na chakula cha afya. Mama mwenye mimba huwa na hamu ya kula vyakula tofauti na huenda baadhi ya vyakula hivi vikawa ni vitamu tamu visivyo kuwa na faida zozote za kiafya. Kwa sababu hii, mama mjamzito ana shauriwa kuwa na ratiba ya lishe ambayo atakuwa anakula kila siku. Kwa kufanya hivi, ana uhakika hatapata jaribio la kula vyakula visivyo kuwa na virutubisho.

Sahani ya mlo ya mama mjamzito

1/2 ya sahani - mboga na matunda

sahani ya mlo ya mama mjamzito

Tofauti na mazoea ya watu ambapo sehemu kubwa ya sahani huwa kibohidrati, katika ujauzito, nusu ya sahani inapaswa kuwa mboga na matunda. Pia, hakikisha kuwa unachagua matunda na mboga za rangi tofauti. Mboga ambazo unashauriwa kula ni kama vile mchicha, kunde, mrendaa, malenge, saga na brokoli.

1/4 ya sahani - protinisahani ya mlo ya mama mjamzito

 

Protini ni muhimu sana katika ujenzi wa mwili. Hata hivyo, vyanzo vya protini kama vile samaki na nyama nyekundu hubeba vimelea. Kwa hivyo, hakikisha kuwa vimepikwa vikapikika kuepuka kuathiriwa afya. Una shauriwa kuepuka protini inayo tokana na wanyama kwa viwango vikubwa. Punguza ulaji wa nyama nyekundu na nyama zilizo sindikwa kama soseji na beconi. Kunde, maharagwe, mbaazi na kadhalika.

1/4 ya sahani - nafaka ama wanga

Maarufu kama kibohidrati ni muhimu sana katika kuupa mwili nguvu. Hakikisha kuwa unakula chakula kutoka kwa nafaka zisizo kobolewa. Nafaka hizi ni kama vile mchele wa hudhurungi, mtama, sima.

Viowevu

maji tosha mwilini ukiwa na mimba

Maji ni muhimu sana katika kutengeneza placenta inayo mlinda mtoto. Hakikisha unakunywa maji kila siku. Wataalum wa afya wana shauri kutoka glasi nane za maji kila siku. Punguza kiwango cha kahawa na sukari unayo kunywa. Soda na sharubati ya kununua hazisaidii mwili, kwa hivyo epuka kuzinywa. Kama lazima unywe, tengeneza sharubati kutoka kwa matunda uliyo nayo jikoni mwako. Maziwa ni nzuri kwa afya yako na ya mwanao.

Mazoezi

Watu wengi hupuuza mazoezi wanapo tunga mimba na kulegea. Kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu huku ukizidi kula kutafanya uwe na uzani wa juu. Mazoezi yanasaidia damu kuzunguka vyema mwilini na pia kudumisha kinga yako ya afya. Hakikisha kuwa una wasiliana na mtaalum mwenye vyeti vya mazoezi unapo fanya mazoezi. Fanya mazoezi mepesi ili usi hatarishe maisha ya mtoto anaye kua tumboni mwako.

Soma piaKeto Kwa Watoto: Je, Lishe Ya Keto Ni Salama Kwa Watoto?

Written by

Risper Nyakio