Jinsi Ya Kuimarisha Uzazi Wako Kwa Kutumia Scent Leaf (Sweet Basil Herb)

Jinsi Ya Kuimarisha Uzazi Wako Kwa Kutumia Scent Leaf (Sweet Basil Herb)

ama ilivyo, mmea wa sweet basil una majukumu mengi zaidi kuliko kuiongeza ladha kwenye vyakula vyako tu. Kiungo hiki kinakusaidia kuongeza nafasi zako za kutunga mimba.

Je, ulisikia nini kuhusu scent leaf na uzazi? Ama scent leaf katika ujauzito na scent leaf na kutunga mimba? Ni kweli kuwa scent leaf linaweza kufanyia mengi katika uzazi na kutunga mimba. Je, ulijua kuwa mmea wa ladha wa Sweet Basil ndio unao julikana kama scent leaf huko Nigeria? Bila shaka kwa sababu ya harufu yake kali ambayo inatumika katika supu na vitoweo vingi. Soma na upate kugundua kuhusu matumizi ya scent leaf katika kupata mtoto.

Scent Leaf na Kutunga Mimba Iwapo Una Matatizo ya Uzazi

scent leaf and conception

Wanawake wengi huwa na ndoto ya kupata watoto wengi. Kwa bahati mbaya, sio kila mtu anayeweza kutimiza ndoto zao. Kulingana na utafiti, asilimia 15 ya wanandoa hutatizika kutunga mimba. Na kati ya nusu ya visa hivi, kisa ni upungufu wa uzazi wa mwanadada; mwili wa mwanamke kushindwa kutunga mimba na kupata watoto. Hili ni jambo la dharura linalo adhiri uwezekano wa kutunga mimba.

Kuhusu Scent Leaf

Scent leaf kwa kawaida lina julikana kama efirin na wana Yoruba; tawi la nchanwu na wa Igbo na daidoya na wana Hausa. Jina lake la kisayansi ni Ocimum gratissimum. Ni mmea wa familia ya Labiatae. Ni mmea unaokuzwa wa kinyumbani na kutumika kama kiungo cha kupika vyakula kufuatia harufu yake ya kuvutia ya kipekee.

Matawi yake yana kiwango cha juu cha kalisi, phosphorus, iron, potassium, carbon na vitamini A. Scent leaf pia ina uwingi wa kemikali za mimea. Mafuta kutoka kwa matawi yana saidia kukumbani dhidi ya bakteria na uyoga. Iwapo unauliza maswali kuhusu scent leaf na uzazi, endelea kusoma upate majibu.

Scent Leaf na kutunga mimba: Baadhi ya faida za kiafya

scent leaf na kutunga mimba

Ili mwanamke ajifungue, lazima awe na uzazi mwema. Je, sweet basil inaifanyia nini uzazi wako? Tazama orodha ya umuhimu wa uzazi hapa chini:

  • Scent leaves zina wingi wa vyuma na madini ya boron.
  • Pia yana uwezo wa kuanzisha homoni ya estrogen.
  • Yana Eugenol ambayo ina uwezo wa kuua viini vinavyo sababisha uchafu wa uke.
  • Pia yana stigmasterol ambayo inahimiza ukuaji wa yai.
  • Tannin na zinc zinapunguza utoaji wa unyevu wa uke.
  • Pia matawi haya yana tryptophan ambayo huenda ika chelesha umri wa kilele cha kujifungua na kufanya scent leaves moja ya mimea ya uzazi baada ya umri wa miaka zaidi ya 40.
  • Kuongeza, iwapo unatafuta mmea wa kukusaidia kupata mimba kwa kasi; mmea wa uzazi wa kujifungua mapacha; scent leaf na kutunga mimba hausifiwi zaidi ya upasavyo. Pia inaongezwa kwenye chai za mimea kuongeza uzazi na kutunga mimba kwa asili kwa kinyumbani.

Athari hasi na mambo ya kujua

scent leaf na kutunga mimba

Iwapo unashangaa kuhusu scent leaf katika ujauzito, cha muhimu ni kujidhibiti. Usiile ikiwa peke yake, ama kuikuna upate sharubati. Itumie kuongeza chakula chako ladha. Kula kwa uthibiti kwa sababu huenda ikasababisha kupoteza mimba hasa katika hatua za mapema za ujauzito. Kwa sasa kwani unafahamu athari zake hasi wakati wa ujauzito, ina umuhimu pia.

Wanawake wajawazito mara nyingi hushuhudia kuumwa na tumbo. Scent leaf inaweza saidia na tatizo hili, kwani ina uwezo wa kutuliza maumivu ya hedhi. Tatizo lingine linalo athiri wanawake wajawazito ni maumivu ya kichwa. Scent leaf inaweza saidia na tatizo hili pia.

Pia inatumika kama matibabu ya kikohozi na baridi; inatibu joto jingi na malaria; inaua viini. Na pia inasaidia kuponya matatizo ya kuto chakata chakula; kupunguza sukari ya damu; kuponya kiungulia na ni nzuri kwa mtima wenye afya.

Mwishowe, sweet basil ama scent leaf ni nzuri kwa wanaume pia.

Iwapo unajaribu kupata mtoto, angalia kwa kina na umakini scent leaf ama kiungo cha sweet basil. Ila, usifanye chochote bila kuongea na daktari wako kwanza. Twakutakia yote mazuri!

Guardian NG

Also read: Coping With Infertility-Related Depression

Makala haya yaliandikwa kwa mara kwa kwanza na Ayeesha kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio