Jinsi ya Kumweleza Binti yako Kuhusu ya Sehemu za Siri za Kiume

Jinsi ya Kumweleza Binti yako Kuhusu ya Sehemu za Siri za Kiume

One day she's going to ask you. So it's best you are prepared...

Nimezoea kuona sehemu za siri za kiume karibu nami. Najua unachofikiria lakini tafadhali usinitafsiri vibaya. Mimi ni mama wa watoto wawili wa kiume.

Katika wakati wangu kama mama wa watoto wawili wa kiume, nimegundua kuna jambo la kushangaza juu ya sehemu za siri za kiume kwa wenyewe. Watoto wangu watashikilia sehemu zao kama zitaanguka iwe wana wasiwasi, wana furaha, wana huzuni ama wanataka kwenda kujisaidia.

Bila kujali adabu, watajikuna ama fumbata sehemu zao za siri wanapokula chakula ama kutazama runinga.  Hawahitaji fursa (kama vile kuoga) kuwa uchi na kujivuna.

Kwa ufupi: sehemu za siri za kiume zinafaa kubadilishiwa jina kuwa “sehemu za umma za kiume”.

Huku kugawa na umma kitu ambacho ni cha siri kilinifanya kuwaza: kina mama wa watoto wa kike wafaa kuwaelezea je sehemu za siri za kiume? Kwa vile hatimaye, unajua, msichana wako mdogo ataja kukuuliza juu yake. Labda atamwona babake akibadilisha nguo.  Ama kaka yake akioga. Na maswali yataulizwa.

Kwa hivyo, badala ya kutokuwa bayana na kupiga kitembe( na kutamani dunia kupasuka na kukumeza) kama mama wa vijana, hivi ndivyo napendekeza uendelee kwa njia mantiki na ya ukweli.

masomo kuhusu sehemu za siri

Be honest and truthful with your daughter, and you’ll be rewarded with open communication channels with her.

Kuwaelezea watoto wako wa kike kuhusu ya sehemu za siri za kiume: vidokezo kwa wasiofahamu

  1. Usilifanye kuwa jambo kuu

Jinsi unavyomwelezea kuhusu maumbile na kazi ya uke wake, vivyo hivyo unaweza kumweleza juu ya kazi ya uume lini na pindi anapouliza. Ukizingatia miaka ya msichana wako, unaweza kufanya hivi kwa wepesi au undani. Iwapo mtoto wako wa kike ama miaka mingi, unaweza kumweleza kwa undani.  Kumbuka kuwa hafai kuwa haihusu uzingatiifu kwani mzazi akimwelimisha msichana wake kuhusu anatomia ni sawa kabisa. Ni vile tu mtoto aliye mdogo kwa umri hataelewa maelezo magumu.

2. Tumia majina sahihi

Watoto wa kike wana uke ilihali wa kiume wana uume – ni virahisi hivyo. Kwa kukwepa kutumia majina ya “kuvutia” kama vile “wee-wee”, unamfunza msichana wako kuwa hakuna aibu kuwa na mazungumzo ya wazi juu ya viungo vya uzazi.

Ni sehemu ya anatomia, baada ya yote. Lakini cha muhimu unamsaidia mtoto wako kujikinga kutokana na washumbulizi wa kingono walio na uwezo wa kutaja sehemu zote za mwili.

Kwa vile washambulizi wa kingono wanaweza rudi nyuma wakimpata mtoto anayetumia majina sahihi  kutaja sehemu zake za mwili, wakidhani kuwa hawa wototo hawataogopa kuwaambia wazazi iwapo watanyanyashwa.

Jinsi ya Kumweleza Binti yako Kuhusu ya Sehemu za Siri za Kiume

3. Uume na uke: sawa lakini tofauti

Njia moja ya kuvunja machachari ni kumwambia msichana wako uume kwa kijana ni kama uke kwa msichana. Ni njia moja ya kutofautusha kati ya msichana na mvulana. Pia, kazi mbili kuu za uume zinaweza kuelezewa ikizingatiwa miaka na uwezo wa msichana wako wa kuelewa..

4. Usiwe rasmi

Iwapo utayafanya mazungumzo kuwa mazito, msichana wako anaweza kuanza kuhisi haya. Unaona, kumwelezea msichana wako kuhusu sehemu za siri za kiume ni zaidi ya kumwelimisha tu juu ya madhumuni la kibiolojia na kazi za sehemu hio. Pia inafungua mlango wa baadaye wa mazungumzo ya wazi juu ya ngono.  Kwa hivyo, tumia toni nyepesi na ya kuelimisha na uweke mifumo ya mazungumzo ikiwa wazi.

Jinsi ya Kumweleza Binti yako Kuhusu ya Sehemu za Siri za Kiume

5. Mwambie uume pia ni sehemu za siri

Kama jinsi alivyo na sehemu zake za siri, pia vijana wana zao. Mkumbushe kuwa sababu sasa amesoma hafai kwenda shuleni siku inayofuata na kuuliza kuona ama kuguza uume wa kijana. Na pia hafai kulazimishwa kuona ama kumshika mmoja. Na hapa, unaweza kuendelea na mazungumzo juu ya “mguzo mzuri na mbaya”, ambapo mtoto anaelimishwa tofauti kati ya hayo mawili ili kumkinga kutokana na wanyanyasaji.

Kwa hivyo, utakapoulizwa swali kuhusu ya uume na msichana wako, ni matumaini yangu hivi vidokezo vitakusaidia kujibu kwa busara. Kumbuka kutazama ishara za kuonyesha msichana wako anahisi haya. Iwapo ziko, simamisha mazungumzo. Kutakuwa na maswali mengi usoni na unaweza kuyajibu huko.

Read also: Why you should call your child’s private parts by their actual names

Written by

Risper Nyakio