Kuinua vitu nzito na kufanya kazi usiku kumehusishwa na uzalishaji wa chini katika wanawake, kulingana na utafiti mpya. Kulingana na ripoti hiyo, kazi inayohitaji nguvu zako za kifizikia ama ratiba za kazi za muda mrefu. Wanandoa hukumbwa na shaka kuhusu uzalishaji baada ya kujaribu kwa muda mrefu bila mafanikio.
Kutatua Shaka Kuhusu Uzalishaji

Kulingana na daktari Kaushiki Dwivedee aliye mkubwa wa idara ya Gynecology na Obstetrics, kujishinikiza kifizikia na kufanya kazi kwa masaa marefu ni baadhi ya vitu vinavyo ongeza mawazo tele. Fikira nyingi huathiri na kupunguza uzalishaji. Pia, homoni nyingi zinazo husika na uzalishaji huathirika kufuatia mtindo wa kulala ulio badilika kufuatia kufanya kazi kwa masaa marefu.
Hili ndilo somo la kwanza kupima iwapo sababu za kikazi zinaathiri uwezo wa kibiolojia wa mwanamke kupata mtoto, kulingana na ripoti hii. Utafiti huu uliangazia ovarian reserve ya mwanamke, ambayo ni idadi ya mayai ya mwanamke na kiwango cha kichocheo cha follicle stimulating hormone(FSH). Kichocheo hiki huongezeka japo mwanamke anavyozidi kuzeeka.
Wanawake waliona kazi zinazo tarajia nguvu nyingi za kifizikia walioingia katika IVF walikuwa na nambari ya chini ya mayai. Na nambari ya chini ya mayai yaliyo komaa. Sawa na wanawake wanaofanya kazi wakati wa usiku. Umri wa mama huchangia pakubwa katika uwezo wake wa kutunga mimba. Mbali na kuvuta sigara, unywaji wa pombe, kuongeza uzito, na matibabu ya saratani. Wanandoa wanaweza zingatia mtindo wa maisha wenye afya ili kuongeza nafasi zao za kutunga mimba. Kama vile kujitenga na uvutaji wa sigara, usiku wa maanani na kuhakikisha kuwa wanalala kwa masaa 8 kila siku, na kuzingatia lishe bora. Wanawake waliokatika umri wa miaka 30' wanaweza kuhifadhi mayai yao. Kwa wanandoa wanaofikiria kuhusu njia ya IVF kupata watoto, wanapaswa kuangazia:

Pumzika: Kitu muhimu sana kwa wanawake wanaotaka kufanya IVF ni kupumzika na kuhakikisha kuwa hawana mawazo zaidi. Usijikwaze kifizikia, ama kimawazo.
Mazoezi mepesi: Ni muhimu kwa wanawake kufanya mazoezi mepesi bila kuushinikiza mwili, kwani kufanya hivi kuna athiri kipindi cha hedhi. Kufanya mazoezi kwa masaa marefu kunafanya kujipandikiza kwa yai kuwe kugumu. Badala yake, wanawake wanastahili kufanya mazoezi mepesi kama vile yoga.
Ni muhimu kwa wanandoa kushauriana na mtaalum wa afya kama ya kuanzisha utaratibu wowote wa uzalishaji.
Soma Pia: Njia 5 Za Kuboresha Mfumo Wa Uzazi Katika Wanawake