Mambo Ya Kufanya Katika Sherehe Ya Kutarajia Mtoto

Mambo Ya Kufanya Katika Sherehe Ya Kutarajia Mtoto

Ushawahi fikiria kuwa na sherehe ya kusherehekea ya kutarajia mtoto ila hauna uhakika kuhusu cha kufanya unapokuwa kwa sherehe hiyo? Kama na sherehe zinginezo zote, huenda ukatarajia kualika familia yako na marafiki. Bila shaka, ni vyema kuwa na sherehe na kuita watu walio karibu sana kusherehekea na wewe; kwenye mahala palipo rembeshwa na baloni za kupendeza za rangi za kuvutia. Ila inapofika wakati wa kupanga sherehe ya kusherehekea mama mjamzito, itakubidi kufikiria zaidi ya keki utakazo walisha wageni wako.

Nigerian baby shower

Kwa hivyo, unatayarisha vipi sherehe hii kwani zimekuwa maarufu sana hasa Kenya na Nigeria miongoni mwa nchi zingine.

Iwapo unashangaa jinsi utakavyo ifanya sherehe hii iwe ya kukumbukika kwa kila mtu, unapaswa kwanza kuelewa aina hii ya sherehe inamaanisha nini.

Ina maana gani kuwa na sherehe ya kutarajia mtoto?

Katika sherehe ya kutarajia mtoto mama anapokuwa na mimba, hii sio sherehe ya kawaida. Ni tofauti na sherehe za kupatia watoto majina na zinginezo kwani inafanyika kabla ya mtoto kuzaliwa. Utamaduni huu wa Umarekani unasherehekea mama anaye tarajia na mtoto. Marafiki na jamaa wa mama aliye na mimba hukusanyika pamoja kumpongeza na zawadi za mtoto.

Sherehe za kutarajia mtoto huwa za wanawake peke yake, ila siku hizi wanaume pia wanaweza hudhuria. Unaweza alika wanaume wa familia na marafiki wako iwapo wangependa kuhudhuria.

Nigerian baby shower

Sherehe ya kutarajia mtoto inafanyika lini?

Most baby showers in Nigeria happen late in the pregnancy. However, you shouldn’t discount the possibility of attending a party hosted by a friend in the early stages of pregnancy. There are no rules! The size of the pregnancy doesn’t matter, it is knowing what to do at a baby shower that counts.

Baadhi ya wamama wanapendelea sherehe hizi baada ya kuzaliwa kwa mtoto, kwa hivyo hupaswi kuwa na aibu kuwa na sherehe ya mtoto wako aliye zaliwa baada ya kila mtu kutembea na kukumpongeza kwa kujifungua.

Ni muhimu sana kupanga sherehe wakati ambao ni sawa kwa wageni wako. Iwapo inawezekana, panga sherehe ya kutarajia mtoto iwe masaa baada ya kazi ama wikendi. Ni muhimu pia kutia akilini hali ya anga ilivyo. Hutaki wageni wako wafike huku wamelowa maji.

Sherehe ya kutarajia mtoto: Sherehe tafadhali!

Sherehe za kutarajia mtoto ni kama sherehe zingine za ki Nigeria; kwani mahali pana umuhimu mwingi sawa na sherehe! Wamama wanaweza tia juhudi nyingi na kutafuta mahali pa kukodisha, shamba la kupendeza, kisima cha kuogelea na hata makanisa. Mahali pa sherehe hii pata tegemea na mada na bajeti ya wazazi watarajia. Huenda pia paka athiri mavazi ya wageni. Huku kuna maana kuwa sherehe ya kando na kisima cha kuogelea itakuwa na mada ya mavazi yatakayo kuwa bora kwa maji.

Nigerian baby shower

Nani atakaye ongea katika sherehe hii?

Sio lazima uongee kwenye sherehe yako ya kutarajia mtoto. Marafiki wa mama mjamzito wanaweza fanya majukumu haya ya kuongea. Mwana familia pia anaweza itwa kufanya jukumu hili la kuongea. Kwa mbadala iwapo watu wanao kuzingira wana aibu kuongea mbele ya watu, unaweza ajiri watu maarufu MC wa kufanya kazi hii. Anaye fanya kazi hii atajua cha kusema na kufanya katika sherehe hii na kuhakikisha watu wanafurahia.

Utaalika nani?

Huenda ikakubidi kuorodhesha watu utakao alika. Kwa bahati mbaya, huenda bajeti yako ika kosa kutoshea idadi kubwa ya wageni, kwa hivyo huenda ukapambana na watu watakao hisi kana kwamba wametupiliwa mbali. Orodha yako ya wageni itahusisha familia, wageni, marafiki wa kazi na wanao kutakia mema wanao taka kujumuika na kufurahia sherehe yako.

Utatumia pesa ngapi kwenye sherehe hii?

Pochi yako itakuwa na jibu la swali hili! Unaweza enda njia kubwa ama ndogo; uamuzi ni wako. Huenda ikawa rahisi sana kwako kuongezea bajeti yako, kwa hivyo panga kila kitu hadi kwa jambo la mwisho. Njia bora zaidi ni kufuatilia matumizi yako ya kila kitu unacho nunua cha sherehe hiyo.

Cha kufanya katika sherehe hii

Huenda chakula ila nzuri ila wageni wao wakataka zaidi ya hizo na divai pia. Iwapo ungependa sherehe isiyo sahaulika, lazima uwe na shughuli za kufurahisha. Kuna sherehe za kutarajia mtoto za kupendeza kuhakikisha wageni wako wamefurahia.

Unashangaa cha kufanya kwenye sherehe hii? Baadhi ni michezo ya kujaribu:
1. Majina ya watoto wanyama
2.  Majina ya watoto wa watu mashuhuri
3. Nini iliyoko kwenye pochi yako?
4. Majina ya watu mashuhuri
5. Mchezo wa majina
6. Kusema mada ya chumba cha mtoto
7. Kurembesha yai
8. Kumvalisha mama
9. Matakwa ya mtoto
10.Kutengeneza jina la mtoto

Mapishi ya kutayarisha kwenye sherehe

Hiari zako za chakula zitategemea na bajeti yako. Unaweza nunua vitamu tamu, vyakula vya kuoka ama keki. Pia unaweza fanya uamuzi wa kutengeneza vyakula vilivyo maarufu nchini kama vile chapati, wali na vinginevyo. Sherehe ya kutarajia mtoto ni nini bila lishe?

Kwa vinywaji, unaweza kuwa na divai, sharubati za matunda ama hata pombe. Vitu vya kufanya kwenye sherehe hii ni kula na kuwa na wakati mwema!

Jinsi ya kuchagua mada ya sherehe hii

Mada yako si lazima iwe kamili. Mada ni ya kuipa sherehe yako uhai na kuwajulisha wageni mipango yako kabla ya wakati. Mada itafunganisha kila kitu pamoja kwa sababu ina athiri mapambo, rangi ya mavazi, vyakula, muziki na mahali pa sherehe hiyo.

Kwa sasa kwani unajua cha kufanya kwenye sherehe yako, usisahau kuwa na wakati mwema!

HuffPost

Soma pia : Top baby items for new moms

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio