Je, ni zipi baadhi ya sheria za talaka zinazo zingatiwa nchini Kenya?

Je, ni zipi baadhi ya sheria za talaka zinazo zingatiwa nchini Kenya?

Kuna sababu tofauti zinazo sababisha upewaji wa talaka katika ndoa. Kama vile kuto suluhisha matatizo. Nchi ya Kenya ina sheria ambazo wana ndoa wanapaswa kufuata katika jambo hili.

Je, unazifahamu sheria za talaka nchini Kenya? Talaka ni idhini rasmi ya kisheria ya mume na mke walio oana kuachana. Kupelekea ndoa kuvunjika isiwepo mke ama mume kuaga dunia. Kupewa talaka katika ndoa inasababishwa na mambo tofauti. Sheria zinazo tawala hatua hii ni tofauti miongoni mwa nchi tofauti duniani. Huenda ikawa ni kupitia uamuzi wa sharia fulani, ama ukubaliano kati ya bibi na bwana. Kila nchi ina sharia zinazo dhibiti upewaji talaka. Wanasheria wanahusika kwa jambo hili ili lile rasmi. 

Maria na Tom walifunga pingu za maisha mnamo mwaka wa 2010 na wakajaliwa watoto wawili. Walipatana wakiwa na umri mchanga ambapo hakuna aliye kuwa na mali maishani. Baada ya kuona, wali kusanya pesa walizo kuwa nazo na kuanza biashara ndogo kuyakimu mahitaji yao. Walibahatika na kupitia jitahada zao, biashara yao ikanoga. Wakaweza kuwa ajiri watu kufanya kazi kwa biashara yao na wakafungua biashara nyingine. Baada ya miaka mitano ya kuishi pamoja bila matatizo. Walianza vurugu za mara kwa mara. Hadi wakati ulipofika na Maria akaamua kutoka kwa ndoa yake na kupewa talaka.

Kuharibika kwa ndoa kuna sababishwa na sababu tofauti. Kwa mfano, bwana ama bibi kutoka nje ya ndoa. Tofauti kati ya wazazi ambazo wanashindwa kuzitatua miongoni mwao. Utengano kati ya wazazi ina madhara chungu nzima kwa watoto hasa wale wenye umri mchanga.

Iwapo mmoja kati ya walio funga ndoa anataka waachane, anapaswa kupeleka nakala ya amri kwa msajili. Yeyote kati ya wawili hao anaweza kuanzisha mchakato huu wa upewaji talaka. Wanapo fanya hivi, wanahitajika kumshughulisha mwana sharia anaye na mambo ya talaka.

Talaka inatolewa ambapo wanandoa imejaribu jitahada zote zile za kurudiana zika feli. Kanisa pia imeshindwa kuregesha uhusiano kamili uliweko kati ya bibi na bwana kupitia masomo ya kikistro ama himizo za kibiblia.  Wakati mwengine, bwana na bibi wanaweza kuwatembelea wazazi na wazee wa jamii ili kupata suluhu kwa matatizo ya kindoa inayo wakumba. Marafiki wa karibu wanaweza kushughulishwa ili bibi na bwana waweze kurudiana. Iwapo njia hizi zote za kuleta utangamano kati ya wawili hawa zina kosa kufanya kazi. Kilicho baki ni wawili hawa kupewa talaka.

Sababu za upewaji talaka

Je, ni zipi baadhi ya sheria za talaka zinazo zingatiwa nchini Kenya?

  • Kutoka nje ya ndoa kwa bibi ama bwana
  • Unyanyasaji wa kimwili wa mwenzi mmoja 
  • Utengano kati yao kwa zaidi ya miaka mitatu
  • Kuto husiana tena kati ya bibi na bwana
  • Iwapo mmoja anashikwa kwa zaidi ya miaka saba ama kupewa fungu la maisha
  • Iwapo mmoja wao anakuwa mwenda wazimu
  • Kufuatia kifo cha mmoja wao
  • Kufuatia mmoja wao kuiacha familia yake kwa zaidi ya miaka mbili
  • Sababu yoyote ile korti inayo shauri sawa kupewa talaka

Korti huenda ikawahimiza wawili hawa wanao taka kupewa talaka kutumia njia isiyo husisha korti ku suluhisha matatizo yao. Wanapewa muda unaotosha ili kuona kama wana weza rudiana. Kuna nyakati hasa ya utengano inayo kubalika na korti. Iwapo juhudi hii itakosa kufanya kazi, korti haina budi ila kuwapa talaka.

Baada ya talaka kuidhinishwa, korti pia inaangalia ugawanaji wa mali kati ya wawili hawa. Sheria za Kenya hazimkubalishi mwanamke kupata ardhi baada ya utengano. Hili ni swala ambalo lime imua uingiliaji kati kutoka kwa mashirika yanayo husiana na haki za wanawake duniani kote. Suala hili lilipo pelekwa kortini ili kuidhinisha ugawanaji kati wa mali ya mke na mme baada ya talaka. Korti halikulipitisha. Ikabakia kuwa bibi baada ya kupewa talaka anapata mali aliyo kuwa nayo walipo anza ndoa. Jambo hili si sawa Kwani wanandoa wengi wana tafuta mali pamoja. Wanapo achana mali hii inafaa kugawanishwa sawa kati ya wawili hawa. Sheria za talaka nchini Kenya pia hazimruhusu mama ku ridhi ardhi baada ya kifo cha mumewe. Kwa jamii za kitamaaduni, mama aliweza kufukuzwa baada ya kifo cha mume wake. Iwapo imani za watu zimeendelea kunufaika na kugeuka kwa muda, wazee wa zamani baado waamini kuwa wanawake hawafai kuridhi ardhi. Serikali Inajaribu jitahada mbali mbali kuelimisha jamii ili ma binti pia waweze kuridhi ardhi baada ya talaka na pia ku miliki mali yao. Kufuatia talaka, watoto wanabaki na mama yao mzazi hadi wanapo fikisha umri wa kumi na nane (18) wanapoweza kuamua mzazi wanao taka kuishi naye. Iwapo mama ndiye aliye toka nje ya ndoa, korti inamkubalisha baba mzazi kubaki na watoto. Korti inaamua mzazi atakaye baki na watoto kufuatia ushahidi alio nao ili watoto wasiteseke mikononi mwa mzazi asiye faa.

Read Also: How to explain divorce to kids in a way they will understand

Written by

Risper Nyakio