Shinikizo la juu la damu katika ujauzito huwa na athari nyingi hasi kwa mwanamke mwenye mimba na mtoto aliye tumboni. Kwa sababu hii, ni vyema kwa mama mjamzito kuhakikisha kuwa anaenda kliniki anavyo faa na kuwasiliana na daktari wake anapo gundua kuwa kuna jambo lisilo sawa.
Baadhi ya matatizo ambayo yanaweza ibuka katika ujauzito ni kama vile, magonjwa ya mafua, maini ama moyo. Na pia damu kuganda kwenye mishipa na kifafa. Mama anapo kuwa na shinikizo la juu la damu katika mimba, ako katika hatari ya kupata placental abruption inayo mfanya kujifungua kabla ya wakati. Wanawake wengi wenye tatizo hili la kiafya huwa katika nafasi zaidi za kujifungua kupitia upasuaji wa C-section.
Matatizo ya shinikizo la juu la damu katika ujauzito kwa fetusi

Shinikizo la juu katika ujauzito hali athiri mama tu, mbali mtoto anaye kua tumboni mwake pia. Mara nyingi, tatizo hili huathiri mishipa inayo zungusha damu mwilini. Na kupunguza kiwango cha damu kinacho ifikia placenta. Kiwango cha hewa na chakula kinacho fika kwenye fetusi hupungua pia. Na kumfanya mtoto anaye zaliwa kuwa mdogo. Mwanamke ako katika hatari ya kujifungua mtoto mapema kabla ya siku anayo tarajiwa kufika.
Matibabu ya shinikizo la damu la juu kwa mama

Ni kawaida kwa wanawake wengi kupata hali hii wanapokuwa na mimba. Hali hii inapo dhibitiwa vyema, mwanamke huwa na ujauzito salama na kujifungua mtoto mwenye afya.
Kwa wanawake wanao tatizika na hali hii na wangependa kujifungua, ni vyema kupata ushauri wa daktari. Ata kushauri kuhusu unacho paswa kufanya na kufanya vipimo vinavyo faa kuhakikisha kuwa utakuwa na safari salama ya ujauzito.
Kliniki ni muhimu sana kwa mama anaye kuwa na tatizo hili katika ujauzito wake. Epuka kutumia dawa bila kushauriwa na daktari. Kuna baadhi ya dawa ambazo ni hatari kwa fetusi. Vipimo vya mara kwa mara na ultra sound zitasaidia kufahamu jinsi mtoto aliye tumboni anavyo endelea.
Soma Pia: Je. Kuna Uwezekano Wa Mayai Kupevuka Mapema Katika Mimba?