Shirika La Afya Duniani Latangaza Janga La Covid-19 Duniani Kote

Shirika La Afya Duniani Latangaza Janga La Covid-19 Duniani Kote

Mkuu wa Shirika La Afya Duniani Daktari Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema kuwa visa vya ugonjwa huu nje ya nchi ya Uchina vimeongeza mara 13 kwa muda wa wiki mbili zilizo pita. Aliendelea kusema kuwa alikuwa na shaka kwa kufuatia viwango vya juu vya kutoshughulika na janga la COVID-19. Mkuu huyu alizidi kusema kuwa hata kama ugonjwa huu ulipewa alama ya janga, Shirika La Afya Duniani halibadili msimamo wake kuhusu jinsi nchi zinavyo paswa kufanya kukumbana na ugonjwa huuu.

Nchi zote zina zidi kupewa mwito wa kubadili jinsi wanavyo kumbana na janga hili na kuwa na juhudi zaidi kutumia njia zilizo dhitishwa kuwa za haraka zaidi. Nchi nyingi zimedhihirisha kuwa ugonjwa huu unaweza kudhibitiwa kwa kufuata njia zifaazo. Ila tatizo liliko ni kwa nchi hizi kukabiliana na kusambazwa kwa ugonjwa huu kupitia kwa muingiliano wa kijamii.

Huenda tukawa na maswali mengi kama vile, janga ni nini hasa? Janga ni ugonjwa unao tamba katika nchi nyingi kwa mwendo wa kasi kwa wakati ulio sawa.

kukaguliwa ugonjwa wa corona virus

Picha shukrani kwa: China Daily

Watu wengi hasa wanamuziki wame ingilia kati na kughairi kuwa na sherehe za kimuziki walizo kuwa wamepanga ili kupunguza visa vya watu wengi kupata maradhi haya. Kwani virusi hivi husambazwa kwa wingi panapokuwa na umati wa watu. Sherehe maarufu kama vile Coachella zime ahirishwa hadi mwezi wa kumi. Na matumaini kuwa ugonjwa huu utakuwa umeisha na mambo kurudi kawaida.

Michezo mingi imeghairiwa na kuahirishwa ili kuhakikisha kuwa kuambukizwa kwa ugonjwa huu kupitia kwa watu wengi kumepunguzwa.

Kadri nchi 100 duniani kote zinasemekana kuathirika na ugonjwa huu. Idadi ya watu walio adhirika na ugonjwa huu nchini Ujerumani vimeongezeka kutoka 1,296 hadi 1,567, Italy zaidi ya kesi 12,000 vimeripotiwa na watu walio kufa kutoka na virusi hivi ni takriban 631. Na watu zaidi ya 900 walikuwa wanachungwa na kupatiwa matibabu maalum. Nchini Iran, visa 9,000 vimeripotiwa na takriban vifo 354 kushuhudiwa.

nchi nyingi kuwa na waathiriwa wa ugonjwa wa corona virus

Picha shukrani kwa CNN

Kuzuka kwa virusi vya Corona ama COVID-19 kumetangazwa kama janga la duniani kote na Shirika la Afya Duniani. Hii ni baada ya virusi hivi kuathiri nchi nyingi duniani kote. Virusi hivi vili ibuka mkoa wa Wuhan nchini Uchina na kisa cha kwanza kuripotiwa mnamo tarehe 31 mwezi wa December mwaka wa 2019. Na tarehe 30 mwezi wa Januari mwaka 2020 kusemekana kuwa tatizo la dharura la kiafya. Tarehe ya kwanza mwezi wa Februari, virusi hivi vilipewa jina mpya na kuitwa COVID-19.

Kufikia tarehe 7 Mwezi wa tatu mwaka wa 2020, kumekuwa na visa 100,000 vilivyo ripotiwa vya ugonjwa huu katika nchi tofauti. Huku kila nchi ikifanya juu chini kuhakikisha kuwa inafanya vyote iwezavyo kuepuka wananchi wake kuugua virusi hivi na pia kupunguza idadi ya watu walio na virusi hivi. Baadhi ya juhudi hizi ni kama vile kughairi usafiri wa ndege kwenda kwa nchi zilizo semekana kuwa na waadhirika wa virusi hivi. Nchi nyingi zimeghairi safari za ndege kwenda nchini Uchina. Jambo ambalo lime kandamiza biashara nyingi kwani nchi ya Uchina ni tasnia la biashara nyingi. Pia tasnia ya kusafiri imeadhirika pakubwa kwani kufuatia uwoga wa kuambukizwa na ugonjwa huu, wasafiri wengi wame ghairi usafiri wao kwa nchi za kitalii. Na hivi kusababisha uchumi wa nchi nyingi kudidimia.

maski za uso dhidi ya covid-19

Nchi nyingi duniani kote zinaendelea kujitayarisha kukumbana na janga hili. Nchi za bara la Africa zinasemekana kuwa zimejitayarisha asilimia 66 kukumbana na janga la COVID-19. Wananchi wana shauriwa kuzingatia kuwa makini sana na kuepuka mahali kuliko na umati wa watu. Pia safari kwa nchi zilizo na visa vya ugonjwa wa corona virus zimeghairiwa.

Written by

Risper Nyakio