Orodha Ya Shule Bora Za Bweni Za Watoto Wako Lagos

Orodha Ya Shule Bora Za Bweni Za Watoto Wako Lagos

Kuna shule nyingi za bweni Lagos ambazo unaweza chagua mojawapo. Ila, uamuzi huu si rahisi kwani masomo na usalama wa mwanao unahusika. Kama mzazi ama mlezi, huenda ikakukwaza kiakili kufanya uamuzi wa shule bora za bweni zinazo wafaa watoto wako.

Hii hasa ni kweli wakati ambapo mtoto anaye taka kujiunga na shule ndiye mtoto wako wa kwanza kujiunga na shule ya sekondari kati ya ndugu zake. Iwapo kuna ndugu wakubwa walioko kwenye shule za mabweni, hakutakuwa na tatizo lolote.

Mambo ya kuangalia unapo chagua shule bora za bweni Lagos

shule bora za bweni

1. Rekordi ya afya njema na usalama

Umefanya kazi njema ya kumchunga mtoto wako kwa muda huu wote na shule njema inapaswa kuchukua usukani wa kumchunga mtoto wako. Mtoto huyo atatumia muda wa miezi tisa shuleni kila mwaka, na unapaswa kuhakikisha kuwa shule itaendelea kutimiza majukumu yako usipokuwa.

Kabla ya kumsajili, unapaswa kuangalia:

 • Kuwa shule hiyo ina zahanati iliyo na vifaa vyote na wauguzi walio na maarifa
 • Huduma za dharura zinazo fanya kazi, iwapo mwanafunzi anahitaji kukimbizwa hospitalini.
 • Mazingara yaliyo salama na safi
 • Maji safi
 • Walimu wanao wahudumia an wanao jali
 • Bweni zilizo na nafasi na kupitisha hewa tosha
 • Jiko iliyo safi na vyakula kutayarishwa kwa usafi inavyo faa

2. Viwango vya juu vya masomo

Kwa sasa kwani unafikiria kuwa shule itakuwa nafasi bora na salama kwa mtoto wako, unahitaji kuhakikisha kuwa viwango vyao vya masomo vinatosha. Unaweza:

 • Hakikisha kuwa walimu wao wana vyeti vinavyo faa
 • Angalia iwapo mfumo wao wa masomo ni sawa
 • Mambo ya ziada wanayo fanya kama michezo
 • Cha muhimu zaidi, angalia alama za wanafunzi wao kwa mitahani ya shuleni na kati ya shule zingine

Orodha yetu ya shule za bweni bora zaidi Lagos

shule bora za bweni

1. Greensprings Schools

Greensprings Schools ni mojawapo ya shule zilizo maarufu zaidi Nigeria. Wana utendaji mwema wa kimasomo ambao una watreni wanafunzi kufuzu Nigeria na duniani kote. Shule hii inazingatia mfumo wa masomo wa Britain na kuifanya kuwa mojawapo ya shule za kidunia Nigeria.

2. Rainbow College

Rainbow College ni mojawapo ya shule za bweni zilizo bora zaidi Lagos kwa sababu ya shule hii kuwa nia ya kuwasaidia wanafunzi kufuzu. Shule hii ina nia ya kuwa kama nyumbani kwa wanafunzi pamoja na timu yao ya walimu na wafanayakazi walio na vyeti vinavyo hitajika.

3. White Dove Schools

Kulingana na tazamio ama misheni ya shule, WDS inakusudia kupatia wanafunzi wake masomo bora yanayo hitajika katika dunia hii inayo songa kwa mwendo wa kasi. Njia bora zaidi ya kufanya hivi ni kwa kuwafunzia watoto kwa mazingara sawa, ambayo WDS inawapatia. Wafanyakazi walio treniwa vyema na kuhakikisha kuwa watoto wanapata huduma bora katika nyanja zote.

4. Holy Child College

Shule hii ilianzishwa mwaka wa 1945 na The Society of the Holy Child of Jesus. Shule hii ya Holy Child College inawapatia wasichana masomo ya juu katika mazingara ya kimasomo na safi. Wana amini katika:

 • Kuwa funza wasichana watakao kuwa hai kwenye jamii ya kidunia
 • Kuwafunza wasichana jinsi ya kuita mwito wa kushindana na kuuliza maswali kwa heshima
 • Kuwaongoza wasichana na kuwaonyesha jinsi ya kuwa na fizikia njema na yenye afya, kuingiliana vyema kijamii na kiroho.
good boarding schools in lagos

The right boarding schools will provide a safe space for your child

5. Apata Memorial School

Apata Memorial School ina vifaa vya shule za bweni za kisasa zinazo wafaa watoto. Iwapo unatafuta shule ya bweni Lagos iliyo na historia na rekordi ya kufanya vyema kimasomo, unapaswa kuangazia AMS. Kwa sababu ya nia yao ya kutoa huduma za kipekee za masomo ya kidunia kwa wote.

6. Loral International School

Wanafunzi wa shule ya kidunia ya Loral International Schools wame fuzu kwenye mashindano ya Nigeria na ya kidunia. Nia na matakwa ya shule ni:

• Kuwa na mazingara bora ya kuwasaidia wanafunzi kufikia malengo yao

• Kuwa treni wanafunzi kuwa bora na hata kwa nyanja zingine mbali na masomo ili kuwa mtu bora kwa jamii

7. Apostolic Faith Secondary School

Shule hii ni ya The Apostolic Faith Ministries. Shule hii ya AFSS ina lengo la kuwa tayarisha wanafunzi kufuzu kwenye mambo wanayo kusudia kuyafanya maishani. Ili wanafunzi wapate himizo wanalo faa ili kujaribu yote waliyo funzwa. Pia, AFSS ina shikilia kwa vikuu uaminifu, na kuwa wazi katika yote uyafanyayo.

Iwapo unatafuta shule ya bweni ya kikristo Lagos, hii ndiyo shule unayo tafuta, Apostolic Faith Secondary School kwani inafunza maadili mema na njia zifaazo za kuishi.

Wazazi kila mahali wana uwoga kuhusu watoto wao kwenda shule zinazo faa. Ni matumaini yetu kuwa orodha hii ya shule za bweni za Lagos itakusaidia kujua mahali pa kuanza.

Vyanzo: Encyclopaedia Britannica 

Soma piaHomeschooling vs. traditional schooling in Nigeria: How to make the choice

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye na kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio