Vidokezo Vya Kuwa Mama Mwema Kwa Watoto Wako: Sifa 5 Za Mama Mwema

Vidokezo Vya Kuwa Mama Mwema Kwa Watoto Wako: Sifa 5 Za Mama Mwema

Ulezi bila shaka sio jambo rahisi, ila kuna mambo unayo weza kufanya ili uwe mzazi mzuri zaidi kwa watoto wako. Tazama sifa za mama mwema.

Ulezi na kuwa mzazi ni kazi ngumu. Hakuna mwongozo wa kukusaida kujua unacho paswa kufanya, kwa njia gani na wakati upi. Ila, unahitajika kufanya kila kitu na kwa njia inayo faa wakati wote. Bila shaka sio rahisi kuwa mama, ila kuna baadhi ya mambo ambayo unaweza kuyafanya ili kuwa mama mzuri zaidi kwa watoto wako. Haya ni mambo ambayo unaweza kujifunza pole pole. Ni vyema kutia akilini kuwa kila mama huwa na mbinu yake tofauti na mama mwingine na kila mama ndiye anaye wafaa watoto wake. Ila ni vyema kuhakikisha kuwa una angalia kasoro zako na kuzirekebisha. Mama ni binadamu wa kawaida na huenda akafanya makosa zake mara kwa mara. Tazama sifa za mama mwema.

Sifa Za Mama Mwema Ni Zipi? Tazama Orodha Yetu!

sifa za mama mwema

  1. Mvumilivu

Hiki ndicho kitu cha kwanza ambacho mama husoma, hasa ikiwa yeye ni mama wa mara ya kwanza. Watoto hulia kila mara, kuangusha vitu kila mahali, kuvunja vifaa vyako na hata wanapokuwa wakubwa, wanamea pembe na hawafuati maagizo yako. Kwa hivyo ni muhimu sana kwa mama kuwa na uvumilivu.

Hata kama sio rahisi, hasa watoto wanapo fanya kinyume na unayo taka wafanye, ni vyema uendelee kuwa shauri na uwe mvumilivu nao.

2. Kusamehe

Ni tabia ya watoto kufanya makosa mara kwa mara. Wazazi pia huwakosea watoto wao. Wazazi wana jukumu la kuwa mfano wa kuigwa kwa watoto wao. Njia pekee ya kuwa mfano mwema ni kwa kuwaonyesha watoto wao jinsi ya kusamehe wengine. Watoto wanapo kukosea, wasamehe, kwa njia hii watelewa umuhimu wa kuwa samehe wengine. Lakini hata unapo wasamehe mara kwa mara, ni vyema kuwa adhibu mara kwa mara ili wajue kuwa sio vyema kufanya vitu visivyo faa. Kwa njia hii, utakuza tabia nzuri kwao.

watu mashuhuri kenya na mama zao

 

3. Jasiri

Unapo jifungua, huenda ukakosa kujua kuwa wewe ni jasiri, ila kuwa mama kuna hitaji uwe jasiri kuzidi ulivyo dhani unaweza. Unahitajika kuwalinda watoto wako dhidi ya mambo mengi yanayo endelea duniani. Utaratibu wa kuwa na ujasiri huanza na kujifungua. Hii ni safari ndefu na isiyo rahisi na kufanikiwa kuna maana kuwa wewe ni jasiri. Pia inapo fika katika safari ya kuwapeleka watoto shule, unapaswa kuwa na ujasiri kwani sio rahisi kuwaacha watoto waende na huku ulikuwa umezoea kukaa nao kila siku.

4. Mwenye maarifa

Watoto huwa na maswali mengi na wao huuliza kuhusu mada tofauti. Kwa hivyo, ni vyema kuwa na maarifa ya mambo tofauti. Kuna vifaa vingi sana ambavyo vinaweza kusaidia kupata maarifa kuhusu mambo hasa yanayo wahusu watoto. Soma vitabu vya watoto na huenda ukapata busara kuhusu baadhi ya maswali watakayo kuuliza. Pia mtandao wa YouTube una mengi ambayo unaweza kujifunza. Kuwa sikiza watoto kutakuongezea maarifa yako. Hakikisha kuwa una zungumza nao mara kwa mara. Huwezi jua kila kitu.

sifa za mama mwema

5. Rafiki mwema

Hii ni mojawapo ya sifa bora zaidi katika orodha yetu ya sifa za mama mwema. Unapaswa kuwa rafiki mwema kwa watoto wako. Kwa njia hii, wanapo kumbana na tatizo lolote, wanajua kuwa wanaweza kwambia jambo lolote linalo wasumbua.

Soma piaWamama Hawa Wa Mashuhuri Wa Kenya Wanafanya Ulezi Uonekane Rahisi Zaidi

Written by

Risper Nyakio