Je, Mwanamke Huwa Na Siku Salama Ambapo Hawezi Pata Mimba?

Je, Mwanamke Huwa Na Siku Salama Ambapo Hawezi Pata Mimba?

Hakuna siku salama baada ya hedhi kuzuia mimba dhabiti. Ni muhimu kwa wanandoa wakati wote kutumia kinga wanapo fanya mapenzi.

Kuna imani nyingi zinazo zingira siku salama baada ya hedhi kuzuia mimba. Kuna siku ambapo mwanamke anaweza fanya tendo la ndoa bila kinga na akose kupata mimba. Tuna angazia zaidi kuhusu siku za rutuba za mwanamke na mzunguko wa hedhi. Yote unayo hitaji kujua.

Siku salama baada ya hedhi kuzuia ujauzito ni zipi?

siku salama baada ya hedhi kuzuia mimba

Je, mwanamke anaweza pata mimba punde tu baada ya kipindi chake cha hedhi kuisha?

Mwanamke ana nafasi ya kutunga mimba anapo fanya tendo la ndoa punde tu baada ya kumaliza kipindi chake cha hedhi ama akiwa nacho. Kama mwanamke hatumii mbinu yoyote ile ya kupanga uzazi, ana uwezo wa kupata mimba wakati wowote katika mzunguko wake wa hedhi.

Hata kama kuna siku salama ambapo mwanamke anaweza fanya mapenzi bila kinga na asipate mimba, ni nadra. Na kwa wanawake walio na vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida, ni vigumu kubaini siku salama. Kuna siku ambapo mwanamke ana rutuba zaidi ya kutunga mimba kirahisi.

Undani wa mzunguko wa hedhi

siku salama baada ya hedhi kuzuia mimba

Ni muhimu kwa kila mwanamke kuelewa mzunguko wa hedhi ulivyo na kinacho fanyika. Mzunguko wa hedhi huanza kila siku ya kwanza ya hedhi yako hadi siku ya mwisho utakapo maliza kipindi chako cha hedhi. Siku ambayo mwanamke ana rutuba zaidi ni siku ya 14th ya mzunguko wake wa hedhi. Inayo fahamika kama siku ya kupevuka kwa yai ama kwa kimombo, ovulation. Hii ndiyo siku ambapo mwanamke ana nafasi zaidi ya kupata mimba.

Baada ya kipindi cha hedhi, kati ya siku ya 11 na ya 14, mwanamke ana nafasi kubwa ya kupata mimba. Kwa hivyo mwanamke anapo fanya mapenzi siku hizi ama chache kabla yake, anaweza tunga mimba. Kumbuka kuwa manii yanaweza dumu mwilini hadi siku tatu ama tano.

Hakuna siku salama baada ya hedhi kuzuia mimba dhabiti. Ni muhimu kwa wanandoa wakati wote kutumia kinga wanapo fanya mapenzi, iwapo hawako tayari kuwa wazazi.

Chanzo: healthline

Soma Pia:Sababu Zinazo Athiri Kuchelewa Kwa Kipindi Chako Cha Hedhi

Written by

Risper Nyakio