Ufanisi katika kushika mimba huathiriwa pakubwa na kufanya tendo la ndoa katika wakati unaofaa. Kufahamu na kuzingatia siku za kupata mimba kunaimarisha nafasi za wanandoa kupata mimba kirahisi. Kufanya tendo la ndoa katika siku ya kupevuka kwa yai ama siku tatu kabla ya siku hii, kunawasaidia wanandoa kufanikiwa katika lengo lao la kuwa wazazi.
Siku Za Kupata Mimba

Mwanamke anapokuwa katika siku yake ya kupevuka kwa yai, yai huachiliwa kutoka kwa ovari na kuingia kwenye mirija ya ovari. Yai huwa na uwezo wa kubaki hai kwa muda wa kati masaa 12 hadi 24. Katika kipindi hiki, yai likipatana na manii ya kiume hurutubishwa na mwanamke kutunga mimba. Tofauti na yai, manii yana uwezo wa kubaki hai kwa siku tano. Kwa hivyo kufanya mapenzi bila kinga siku tatu kabla ya siku ya kupevuka kwa yai kunamweka mama katika nafasi ya kushika mimba.
Siku ya kupevuka kwa yai

Mwanamke anapaswa kufahamu siku ya kuengua kwa yai. La kwanza ni kufahamu mzunguko wa hedhi, na iwapo ni wa kawaida ama unabadilika. Kwa wanawake walio na mzunguko wa kawaida, ni rahisi kujua siku ya kupevuka kwa yai. Mara nyingi huwa siku ya 14 ya mzunguko wao wa hedhi. Hata hivyo, mwanamke na huathiri na vitu vingi na huenda kipindi chake cha hedhi kikabadilika na kufanya siku ya ovulation ibadilike. Kuna baadhi ya wanawake ambao huenda wakawa na siku za ovulation mbili kwa mwezi. Walio na mzunguko mfupi.
Kwa kuangalia mabadiliko yanayofanyika mwilini, mwanamke anaweza kujua siku ya ovulation. Baadhi ya ishara zinazomdokezea mwanamke kuwa anakaribia siku za hatari za kupata mimba, ni kama vile:
- Uchafu wa uke kuwa mweupe sawa na yai, laini na unaonyooka
- Kuumwa na upande mmoja wa tumbo. Upande unaouma unaashiria ovari iliyoachilia yai
- Mabadiliko ya temprecha mwilini. Mwanamke anapokaribia kuovulate, temprecha mwilini huongezeka
- Kutumia kit ya kutabiri siku ya ovulation. Inamsaidia mwanamke kufahamu wakati bora wa kushika mimba kwani inadhihirisha siku za hatari kupata mimba zinapoanza.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Ongeza Nafasi Zako Za Kupata Mimba Kwa Kutumia Kalenda Ya Ovulation