Kuavya ama kutoa mimba ni tendo la hiari la kukomesha ukuaji wa mimba tumboni mwa mwanamke. Sababu tofauti zinamfanya mama kufika kwenye uamuzi huu. Kuna mbinu tofauti zinazotumika kufanya hili, kama kutumia sindano ya kutoa mimba, na kutumia tembe za kutoa mimba.
Sheria za Utoaji Mimba Nchini Kenya

Utoaji wa mimba nchini Kenya umepigwa marufuku ila katika visa ambapo mama alibakwa, ama mimba inapohatarisha maisha yake. Kuavya mimba kwa njia zisizo salama ni chanzo kikuu cha vifo na matatizo ya kiafya kwa wanawake wengi nchini Kenya. Kutumia njia hatari kutoa mimba kunamweka mama katika hatari ya kuvuja damu kupindukia na kupoteza maisha yake ama kuharibika kwa uterasi yake.
Kulingana na katiba ya Kenya Makala 26(IV), utoaji wa mimba haukubaliki usipofanywa na mtaalum wa afya aliye na maarifa ya kufanya kitendo hicho, hali ya matibabu ya dharura ama maisha ya mama yamo hatarini.
Njia salama za kuavya mimba
- Kutumia vifaa vya upanuaji na ukwanguaji
Kifaa kinachofahamika kama curette kilicho sawa na kijiko kidogo kimetengenezwa maalum cha kuingizwa kwenye tumbo la uzazi. Kinatumika kukwangua mimba. Kinapanua mlango wa uzazi ili kiweze kufika kwenye tumbo la uzazi. Mbinu hii ya utoaji wa mimba huwa na uchungu mwingi.
Dawa za kutoa ujauzito hufanya kazi kwa kubana kisha kutoa mimba nje. Dawa hizi zilizo kwa aina ya tembe humezwa ama kuingizwa kwenye uke. Inapotumika kwa njia sahihi, huwa na ufanisi mkubwa. Ndani ya masaa matatu, mwanamke huwa ameanza kuvuja damu. Hata hivyo, mbinu hii ya kuavya mimba humweka mwanamke katika hatari ya kupata maambukizi na anapaswa kuchukua dawa za antibacterial kumlinda dhidi ya kuugua. Dawa hizi hupatikana kwenye vituo vya hospitali peke yake.

Ujauzito hutolewa kwa kunyonywa kutumia sindano maalum inayoingizwa kwenye mlango la uzazi hadi kwenye tumbo la uzazi. Huwa bora mbinu hii inapofanyika kwa ujauzito ndani ya miezi mitatu, baada ya hapo, mama huwa katika hatari. Mwanamke aliyejaribu kutoa mimba kisha utaratibu huo kutomalizika ifaavyo, mbinu hii inatumika kutoa mabaki.
Mbinu yoyote ile ya kutoa mimba inapaswa kufanyika kwenye kituo cha hospitali na mtaalum mwenye mafunzo ya kufanya kitendo hicho. Kutumia dawa za kutoa mimba kama mifepristone na misoprostol bila ushauri wa daktari kuna hatari kubwa.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Jinsi Ya Kutumia Vidonge Kutoa Mimba Na Athari Kwa Mwanamke