Vitu Muhimu Vya Kusoma Kutoka Kwa Sinema Ya The Lion King

Vitu Muhimu Vya Kusoma Kutoka Kwa Sinema Ya The Lion King

Ni yapi ya kusoma kutoka kwa sinema hii ya The Lion King? Soma zaidi...

Mojawapo ya sinema za kupendeza zaidi za wanyama zilizo tengenezewa Disney land ni sinema ya The Lion King iliyo shuhudiwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1994 na ya kwanza iliyo dhibitika kuwa hadithi ya kweli. Somo muhimu kutoka kwa sinema ya The Lion King zinazo funzwa kwa watoto zitasaidia pakuu katika maisha yao.

Sinema hii inaeleza kuhusu Simba, mtoto wa simba anayepaswa kutawala baada ya babake, Mufasa, kama mfalme wa Pride Lands. Baada ya mjomba wake kumwua babake, simba huyu mdogo alipitia changamoto nyingi kutafuta takdiri yake kama mfalme. Simba lazima aelewe 'Duara Kubwa Ya Maisha', inayo unganisa viumbe wote.

Sinema hii ya mwezi huu kutoka Disney land ilikuwa na waigizaji Beyonce, Donald Glover na Chiwetel Ejiofor. Ila hadithi ni ile na masomo yake bado yana onekana.

lion kinglessons taught

Wakati huu unapo peleka watoto kuona sinema hii mpya ya The Lion King, weka akilini somo hizi muhimu. Waeleze watoto wako, na pia usome jambo moja ama mawili. Baada ya yote, mambo tunayo ona kwa sinema ni tabiri ya yanayo endelea kwa dunia yetu.

Somo kutoka kwa sinema ya The Lion King

lion kinglessons taught

1. "Ji amini na siku itafika ambapo wengine hawatakuwa na hiari ila kuamini nawe." Mufasa

Hili ni jambo ambalo kila mtoto anapaswa kusoma mapema. Katika dunia hii ya mambo yasiyo eleweka, ni muhimu kujua wewe ni nani. Watoto wanapaswa kusoma kutosheka jinsi walivyo, na kujua kuwa wanatosha. Ni hatua ya kwanza ya kuwafanya wengine wakuamini na wakuthamini.

2. "Angalia zaidi ya uonacho." Rafiki

Wafunze watoto wako kuona zaidi ya yanayo onekana hadi kwa yanayo wezekana yasio onekana kwa dunia kwa macho. Hakuna kitu kisicho wezekana, na uwezo wa kuota yasiyo wezekana ndiyo watu wakuu wanatengenezwa kutoka.

3. "Kuna zaidi ya kuwa mfalme zaidi ya kupata vitu kwa njia yako wakati wote." Mufasa

Watoto wanataka kitu, na wanakitaka wakati huu. Ila maisha hayatupi kila tunacho taka. Kuwafunza watoto wako ukweli kutawasaidia kuwa na uwezo wa kuishi unaohitajika kwa dunia.

lion kinglessons taught

4. "Mabadiliko ni mema." Rafiki

Mabadiliko ni mojawapo ya vitu tusivyo weza kuhepa maishani, na wakati wote sio mabaya. Somo hili la maisha litasaidia watoto wako kupambana na nyakati zinazo badilika na majira ya maisha.

5. "Kila kitu unacho ona kinaishi kwa pamoja na usawa. Kama mfalme, unahitaji kuelewa kuwa usawa na heshima kwa viumbe wote, kutoka kwa siafu wanao tambaa hadi kwa chui." Mufasa

Dunia yetu husonga kwa njia fulani. Kila kitu kinahusika kwa njia fulani. Tunapata oxygeni safi kutoka kwa miti ya kijani, na tunaipa carbon dioxide. Mazingira yana sawasisha kila kitu. Hii ndiyo sababu kwa nini watoto lazima wasome kushukuru na kuheshimu yote wanayo kumbana nayo. Hata ikiwa wana tofautiana, sisi sote ni spesheli. Hili ni somo muhimu maishani.

Mada zaidi za kusoma kutoka kwa The Lion King

lion king

6. "Kutoka kwa majivu ya ajali hii, tuna ibuka kusalimia kucha kwa majira mapya." Scar

Hayaja isha hadi yaishe kabisa. Na yanapo isha, baadhi ya wakati, mwisho wa kitu unakupa nafasi ya kuumba mwanzo wa kupendeza zaidi. Kwa hivyo, hakuna sababu ya kukata tamaa. Somo hili ni muhimu sana maishani na litasaidia watoto wako kuto kata tamaa na sisi sote tunahitaji kuwa hivi.

7. "Ni nyakati kama hizi, rafiki yangu Timon husema: lazima uweke maisha yako ya awali nyuma yako." Pumba

Wacha watoto wasome kuwacha maisha ya hapo awali nyuma yao. Hakuna haja ya kushikilia yaliyo pita kwani hayatawahi rudi. Yaliyo kwa sasa na ya hapo usoni, ndiyo yana maana. Hayo ndiyo tunapaswa kuangazia.

lessons taught

8. "Nina ujasiri tu ninapo paswa kuwa nao. Kuwa jasiri hakuna maana ya kuenda kutafuta shida. " Mufasa

Kuwa mtoto jasiri sio sababu ya kuwa dhalilisha watu wengine. Ujasiri wa mtoto wako unapaswa kumsukuma kufuzu shuleni na kujaribu vyeo vya uongozi. Sio sababu ya kuwavuta wengine chini.

9. "Hadithi yoyote inayo faa inaweza hadithiwa mara mbili." Rafiki

Watoto wanapaswa kusoma umuhimu wa kuishi ukweli wao, na kusema ukweli wakati wote. Katika dunia hii leo, kuna mambo mengi sana na watu wanajaribu kuhakikisha kuwa hawana usemi. Ila ni muhimu tukose kuwakubalisha.

Zaidi ya yote, The Lion King inatufunza kuwa tunaweza kushinda changamoto zote tunazo kumbana nazo, tusipo kubalisha shaka zitupiku. Mada ingine muhimu ya kusoma kutoka kwa sinema hii ni kuwa mamlaka yanaweza kufunga macho.

Hakuna Matata.

Goalcast

Soma pia: Beyoncé Speaks As Nala In New Lion King Movie Trailer

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Ayeesha kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio